Orodha ya wasanii wa Bongofleva walioingiza pesa nyingi 2015

bidam90

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
273
193
Top 10 Wasanii wa Bongofleva matajiri mwaka 2015..

Kama kuna kitu ambacho unaweza kukitofautisha wakati mziki wa bongofleva unaanza hadi leo basi bila shaka ni thamani ya mziki ho kuongezeka mara dufu. Ni juzi tu hapa alikiba alihojiwa na kudai aliuza copy milioni 2 za album yake ya kwanza ya Cinderella na kuambulia shilingi 200 kwa kila copy .

Hivi sasa mziki umebadilika na Bongoweekly tumeamua kukaa mezani na kupiga hesabu ya wasanii matajiri kutokana na kazi zao wanazofanya katika mziki wa Bongo fleva na mikataba mbalimbali ya kibiashara. Twende kazi..

10. Joh Makini
Kama unadhani Joh Makini hana pesa basi ?Don?t bother? . Ni juzi tu hapa ametoka kushot video aliyomshirikisha AKA huko nchini Afrika Kusini ambayo iliyomgharimu milioni 32 za kitanzania . Kabla ya hapo Joh Makini aliingia gharam nyingine huko huko SA kushoot video ya ?Nusu nusu ? . Ni wazi kama kuna mwaka ambao umemtajirisha mwamba wa kaskazini basi ni mwaka 2015 kwani anatarajiwa kutoa audio na video na Davido ambayo ni wazi itamgharimu sana.

09. Linah
Nani atasahau mwanzoni mwa mwaka mwanadada Linah alipotoa Dola 47,000 , zaidi ya milioni 100 za bongo kwenda Afrika Kusini kutengeneza video ya Ole Themba . Pia Linah aliteuliwa kua balozi wa kinywaji cha Jebel kitu ambacho tkimemuongezea kipato. Mwaka 2015 linah ameweza kutengeneza pesa za kutosha kupitia mziki kiasi cha kustahili kuingia kwenye hii listi.

08. Jux
Baada ya kuachia ngoma ya ?Uzuri wako? , maisha ya kimziki ya jux hajarudi nyuma tena na mwaka huu jux ameweza kuingiza pesa za kutosha kupitia mziki wake. Ni juzi juzi hapa jux alipost picha la begi likiwa na noti za pesa za kimarekani huku akiandika kwamba aliona milioni 200 alipokua na miaka 22 . Ukiachana na hizo pesa za instagram , mpenzi huyu wa mwanadada Vanessa Mdee mwaka huu ameweza kuporomosha bonge moja la ikulu lenye hadhi ya kistaa lina studio ya kurekodi, Gym kwa ajili ya mazoezi na Bwawa la Kuogelea ndani.

07. Shettah
Unaweza kumuita shikorobo master . Shetta naye ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri mwaka huu na kuingiza pesa za kutosha hasa kutokana na show zake za nje na Biashara. Juzijuzi Alizushiwa kwamba anauza Unga Afrika Kusini kutokana na kwenda mara kwa mara na kukanusha kwa kuwaambia mashabiki wake kwamba anaingiza pesa kupitia mziki na kutumia pesa hizo kufanya biashara nyingine.

06. Nay wa Mitego
Kati ya wanamuziki wafanyabiashara na wanaojua kuwekeza kwenye Mziki basi huwezi kumuacha Nay wa Mitego . Mwaka 2015 ameendelea kujitajirisha kupitia mziki wake na mikataba ya kibiashara hususani na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel.

05. Professor Jay
Mmbunge mteule wa mikumi hakusikika sana kwenye mziki mwaka huu lakini bado ameweza kuendeleza utajiri wake kupitia uwekezaji kwenye vitu kadhaa kama Studio. Baada ya kupata ubunge , Professor Jay ameahidi kuendeleza kasi yake katika mziki huku akiwa anaingiza mkwanja wa kutosha kila siku akizama mjengoni.

04. AY
Kwasasa anatamba na ngoma yake ya ?Zigo? , AY anaingiza pesa nyingi kupitia mikataba mbalimbali ya kibiashara na kampeni mbalimbali za kimataifa kama Balozi. Mwaka Jana akiwa na wasanii wenzake 9 alitembelea Ikulu ya Marekani. Pia mwishoni mwa mwaka Jana aliachia ngoma ya "Touch Me" aliyomshirikisha Sean Kingston hivyo kujipanulia wigo la ukuaji wake kiuchumi.

03. Ali Kiba
Ndio, Kama kuna mtu ambae ameshawahi kukutana na Ali kiba laivu basi atakubaliana na mimi kua sio mtu anayeonyesha kua ana pesa lakini hali hio haimfanyi kutokua namba 3 kwani ukiacha namba 1 kwenye list hii , Ali Kiba ndio msanii aliyejitajirisha mwaka huu kupitia mziki. Amefanya show nyingi sana nje na ndani ya nchi , amesaini mikataba ya kibalozi ya kutosha na gharama zake kwa show moja ni balaa mfano mzuri ni ile karatasi ya CCM iliyovuja ikionyesha pesa watazopata wasanii kwenye kampeni ambapo ali kiba alikua wa pili akipata milioni 60 kwa show 4 .

02. Lady Jaydee
Unaweza kumuita malkia wa mziki wa Bongo Fleva . Mwaka huu aliweza kuachia ngoma na video kadhaa japokua sio sababu yupo namba 2 kwani tayari alikua anaendeleza utajiri aliyokwisha jikusanyia miaka na miaka.

01. Diamond Platnumz
Kuna mtu anabisha ?? nadhani huyu amepitwa bila kupingwa . Muite Mfalme wa Bongo Fleva kwasasa na sio tu ni namba moja kwenye list hii bali hata ukitengeneza ya Afrika unaweza usimkose mzee mwenyewe Platnumz . Mwaka 2015 umezidi kumtajirisha Platnumz huku akimalizia Ikulu / Nyumba yake ya 10 kuijenga ikiwa na choo chenye Dhahabu , thamani yake ikiwa milioni 70 . Ebwanae , hicho choo wasiingize kila mtu maana usawa wenyewe huu?.Diamond ameweza kujiongezea mikataba kibao na makampuni ya ndani na nje ya nchi na mwisho wa siku pesa yake kubwa inaingia kupitia mauzo ya muziki wake na show huku akiwa ndio msanii ghali Tanzania.

Chanzo: Bongo Weekly
 
Hii list imeandaliwa vijiweni. Vielelezo havijitoshelezi, vilivyopo havina maana.

Studio ya Professor Jay imerekodi nyimbo ngapi, na mafanikio ya hizo nyimbo ni yapi? Ubunge wenyewe ndio kwanza kaapishwa.
 
Hii list imeandaliwa choon ndo ikaletwa hapa aliyoaanda mwenyewe shabiki wa flan
 
List ni ya kitu kingine kabisa, na yeye anaongelea vitu vingine kabisa kwenye justification ya position alizowapa hao watu kama kushoot video kiasi ful?ni, anaweza akawa ameshoot kwa kukopa au kurudisha gharama baada ya mwezi au mwingine katengeneza pesa ila hajashoot video ya gharama

Kuna watu ambao walitakiwa kuwepo hapo ambao wamekusanya pesa ndefu

+Kati ya wasanii waliopiga show nyingi zaidi mwaka huu basi Yamoto band wanaweza wakawa wanaongoza, na wastani wa gharama yao ni millioni kumi (10 mil) kwa show.. Hawa madogo wameingiza pesa nyingi zaidi ya linah na sheta.. Linah hakufanikiwa kuwa na show nyingi kiivo mp?ka kampeni zilivyoanza, na shetta ilipofika mwezi wa 4 dau lake kwa show rasmi ilikuwa dollar 5000 (wastani wa mil 10) na ubalozi wa startimes, ila bado haimfanyi kuwaficha yaamoto

+Kwenye top spots namba mbili ninawasiwasi nayo, lady j dee anamkwanja mrefu sana ila unaposema walioingiza pesa nyingi zaidi kw mwaka huu hastahili hiyo nafasi,,

Alikiba nae nafasi ya tatu haimfai kabisa, kuna walipata mkwanja zaidi yake akiwemo ommy dimpoz na AY.. Alikiba hajapata endorsement deal ya ubalozi wowote (Ubalozi wa wildlife ni wakujitolea, kama kuna pesa basi ni ya maji ya kunywa tu) kwa show analipwa 15 mil na shows hajafanya nyingi kiivo kumfanya aingie kwenye top 3

Huyo namba moja wamuache kama alivyo, mtu mbaaaaya sana huyo.. Show zake nne tu za tanzania zinamfanya aongoze list, ukizungumzia mwaka mzima bado mauzo ya nyimbo zake miito, youtube, hatimiliki (kama ilivyotoka kenya kaongoza hadi wakenya wenyewe) bado ubalozi DSTV, Mziiki, ametishaa..!
 
Nadhani hii orodha imeandaliwa kwa kuangalia habari ambazo sio rasmi. Utasemaje Jux ametengeneza pesa nyingi kisa tu alionesha begi la pesa katika akaunti yake ya Instagram?
Unasemaje Joh Makini na Linah wameingiza pesa nyingi kwa kigezo cha kutengeneza video za gharama? Vipi return ya uwekezaji wap iko sawa?
Unamuwekaje Professor Jay kwa kutumia kigezo cha kipato cha ubunge? Kama ni kigezo hicho basi Sugu naye angekuwa juu zaidi maana hata pensheni za ubunge walilipwa zaidi ya Milioni 200.
 
List ni ya kitu kingine kabisa, na yeye anaongelea vitu vingine kabisa kwenye justification ya position alizowapa hao watu kama kushoot video kiasi ful?ni, anaweza akawa ameshoot kwa kukopa au kurudisha gharama baada ya mwezi au mwingine katengeneza pesa ila hajashoot video ya gharama

Kuna watu ambao walitakiwa kuwepo hapo ambao wamekusanya pesa ndefu

+Kati ya wasanii waliopiga show nyingi zaidi mwaka huu basi Yamoto band wanaweza wakawa wanaongoza, na wastani wa gharama yao ni millioni kumi (10 mil) kwa show.. Hawa madogo wameingiza pesa nyingi zaidi ya linah na sheta.. Linah hakufanikiwa kuwa na show nyingi kiivo mp?ka kampeni zilivyoanza, na shetta ilipofika mwezi wa 4 dau lake kwa show rasmi ilikuwa dollar 5000 (wastani wa mil 10) na ubalozi wa startimes, ila bado haimfanyi kuwaficha yaamoto

+Kwenye top spots namba mbili ninawasiwasi nayo, lady j dee anamkwanja mrefu sana ila unaposema walioingiza pesa nyingi zaidi kw mwaka huu hastahili hiyo nafasi,,

Alikiba nae nafasi ya tatu haimfai kabisa, kuna walipata mkwanja zaidi yake akiwemo ommy dimpoz na AY.. Alikiba hajapata endorsement deal ya ubalozi wowote (Ubalozi wa wildlife ni wakujitolea, kama kuna pesa basi ni ya maji ya kunywa tu) kwa show analipwa 15 mil na shows hajafanya nyingi kiivo kumfanya aingie kwenye top 3

Huyo namba moja wamuache kama alivyo, mtu mbaaaaya sana huyo.. Show zake nne tu za tanzania zinamfanya aongoze list, ukizungumzia mwaka mzima bado mauzo ya nyimbo zake miito, youtube, hatimiliki (kama ilivyotoka kenya kaongoza hadi wakenya wenyewe) bado ubalozi DSTV, Mziiki, ametishaa..!

sasa Alikiba inamfaa namba ngapi? naona wewe na mtoa mada hamna kitu
 
Lina alilipiwa video na management yake pesa yoote. tumia vigezo vya assets, deals, shows wanazopata c kuangalia gharama za video au nn"
 
We jamaa ni MUONGO SANA.
 
Kwenye hiyo list mbona Shilole ujamuweka? Shishi baby mwaka huu 2015 kapiga show nyingi za ughaibuni mpaka BASATA wamembania.
 
sasa Alikiba inamfaa namba ngapi? naona wewe na mtoa mada hamna kitu
Ali Kiba alistahili namba 6 au 5 kama ingewekwa kwa kufuata kwa jinsi walivyoingiza pesa kwenye vyanzo vyao vya mapato kwa uhalisia maana hiyo namba moja iko mbali sana sana kwa sasa uwezi kumlinganishia na wasanii watz kawaacha mno.
 
mimi sijamringanisha na namba moja huyo. kwa aliyetoa hii list haeleweki
 
Ali kiba ameshapata pakukaa au bado yupo kwa mama yake?? Maana alipokuwa anakaa kunduchi alifukuzwa na mwenye nyumba yule dada alokuwa anamlea. Na wabongo mnamwita milionea.
 
Hii list hujaitendea haki bila kumuweka Shilole humu. Angalia nyomi hiyo kwenye shoo zake

DSC_0434.JPG

DSC_0437.JPG

DSC02050.jpeg
 
Back
Top Bottom