Kwa jinsi ninavyoona mimi nahisi(kama ni kweli TBC wamekatisha nao mkataba) nahisi Management ya sasa ya TBC itakuwa ina matatizo ama wanataka waondokane na mikataba yote ambayo iliingiwa wakati wa TIDO/kuondoa program zilizoanzishwa enzi za TIDO.....
Vipindi vingi vya burudani vilivyoanzishwa enzi za TIDO havipo sasa.....Mfano Bongo Dar es Salaam, Burudani ni Nyumbani, Orijino Komedi Show, Boda 2 Boda na hata matangazo ya Live ya michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza......Kwa ujumla TBC kwa sasa inarudi nyuma kwa kasi badala ya kuendelea mbele...
Kiukweli hauwezi ukawalinganisha Ze Comedy wa EATV na Orijino Komedi.....Wale wa EATV ni bure kabisa,hawana jipya zadi ya kuwaiga Orijino Komedi.....Hata Futuhi ina uafadhali.....
Kwangu mimi VITUKO SHOW ya Channel Ten ndio Mwanzo mwisho......King Majuto, Onyango, Mwita Maranya, Sharo Milionea, Masele Chapombe, Mzee Pembe, Mzee Toffi, Asha Boko, Shangazi/Madoido, Senga, Chilli, Mkono,Kingwendu, Erick na wengine.....Hawa jamaa wako juu kuliko maelezo