Organic Farming (Kilimo Hai)

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Jul 3, 2015
608
1,263
Kilimo hai au organic farming ni aina ya kilimo kinachozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo. Kilimo hicho kinatumia mbolea na madawa yasiyotengenezwa viwandani na kinazingatia utunzaji wa mazingira kwa ajili ya manufaa kwa jamii, kiuchumi na kiafya.

Tumeirithi ardhi kutoka kwa vizazi vilivyotangulia ikiwa na ubora wa asili, lakini kutokana na matumizi ya muda mrefu, ardhi huzeeka na kushindwa kutoa mazao bora, hivyo kumfanya binadamu kutafuta namna nyingine ya kuifanya ardhi hiyo itoe mazao mengi ambapo moja ya mbinu hizo ni kutumia mbolea za viwandani ambazo zikitumika muda mrefu hupunguza kabisa rutuba ya udongo.

Baada ya kuona ardhi imechoka Wakulima wengi huamua kutafuta maeneo mengine yaliyo bora na kuanza kuyatumia. Wakati mwingine hulazimika kufyeka misitu ili kupata mashamba mapya, hali ambayo siyo tu inaharibu mazingira, lakini pia inaweza kututia umaskini wa milele kwa sababu ardhi iliyoachwa awali huwa haitafutiwi njia muafaka ya kuifanya irejee kwenye ubora wake.

Lakini jambo la kuzingatia kwa sasa, kila mtu anatakiwa kuvuta kumbukumbu zake kulingana na umri alioishi na kuangalia yafuatayo: Hali ya udongo enzi zile na sasa ikoje? Kiwango cha maradhi wakati ule na sasa kikoje? Uwezo wa udongo kuzalisha kwa sasa upoje

Inaonyesha kuwa mbolea za chumvichumvi zimechakaza udongo na hivyo kufanya uzalishaji upungue. Hata mazao yanayotokana na matumizi ya mbolea hizo yamekosa ubora wa asili unaotakiwa.

Vilevile magonjwa yamekuwa mengi mengi yakihisiwa kutokana na kemikali za madawa yanayonyunyuziwa katika mazao, mfano cancer na mengine mengi

Ni muda muafaka wa wakulima na wadau wa sekta hii kujikita katika kilimo hai kwa faida ya afya zetu, Ardhi na mazingira kwa ujumla.

#OrganicFarmingIsAwayToGo
#organicAgricultureAmbassador

AgriGanic Tanzania
P. O. Box 2021,
Dodoma, Tanzania

Kwa ushauri kuhusu kilimo hai, tuandikie kupitia email-Pnairah@gmail.com
 
Nimenuia kufanya kilimo hai, ninazo ekari 3 za ardhi kwa ajili ya mbogamboga na matunda, gharama za mbolea na dawa asili ni kubwa na upatikanaji wake ni adimu kiasi wakati kwa masoko ya ndani walaji hawajui kutofautisha, ili nimejipanga kufanya promo ya kutosha nikiamini wenye uelewa watapenda niwalishe mazao salama kwa afya zao. Sina taaluma ya kilimo isipokuwa ninakipenda toka moyoni na ndiyo maana nimeamua kuwekeza kwacho na kwa sababu nataka kuwa tofauti na wengine ndiyo maana nimeamua kufanya Organic Farming. Mwenye ushauli upande wa madawa asili ya ukungu naomba anisaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibu sana, nitakutumia mawasiliano yangu pm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom