Orchestra Maquis Original "ogelea piga mbizi" ilivyowatesa Watanzania

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
22,773
20,019
...
MAQUIS du ZAIRE ni bendi ambayo ‘iliwatesa’ Watanzania kwa kuwaporomoshea burudani za muziki wa dansi maridhawa katika kumbi mbalimbali hapa nchini Kwa wale waliokuwa vijana kati ya miaka ya 1970 na 1990, katu hawawezi kuisahau bendi hiyo ambayo iliingia hapa nchini kwa kishindo kikubwa ikitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Zaire) wakati huo. Mwaka 1981, niliwahi kufanya mahojiano maalumu na mmoja wa viongozi wa bendi hiyo Chimbwiza Mbangu ‘Nguza Vicking’ ambaye alinipa wasifu wa bendi hiyo ya Maquis du Zaire.Kwa kuwa wasifu huo uandikwa na kuchapishwa katika gazeti la serikali la Nchi Yetu la kila mwezi, ambalo lilikuwa likuzwa kwa senti 30, likitolewa na mwajiri wangu wakati huo, Idara ya habari (MAELEZO).

Hivyo basi si vibaya nikirejea kuwapasha wale ambao hawafahamu na kwa waliosahau, nichukue muda wenu kwa kuwapa wasifu wa bendi hiyo tangia ilivyoanzishwa hadi kutoweka kwake katika taswira ya muziki. Historia ya bendi hiyo inaanzia mwaka 1960 kwa waliokuwa vijana wa wakati huo katika mji wa Kamina huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Zaire), walioungana na kuunda bendi yao wakaiita Super Theo.

Bendi hiyo ilitoa burudani tosha kwa wapenzi wa muziki wa Kamina na vitongoji vinavyouzunguka mji huo, baadaye wakaibadilisha jina kuwa Super Gabby.Katika kile kilichoelezwa na uongozi wa Super Gabby kuwa ni kuleta mageuzi katika muziki, bendi hiyo mwaka 1972, ilibadili jina rasmi na kuwa Maquis du Zaire.

Maquis du Zaire iliingia hapa Tanzania mwaka huohuo wa 1972, kwa mwaliko wa mfanyabishara maarufu Mzee Batengas. Walianza kutumbuiza kwa mkataba katika ukumbi wa Mikumi Tours uliokuwa maeneo la Tazara Buguruni, jijini Dar es Salaam. Baada ya kumaliza mkataba wao waliachana na Mzee Batengas, wakaenda kupiga muziki katika Klabu ya Hunters kwa kipindi kifupi. Kisha viongozi wa bendi hiyo wakafanya mazungumzo na mfanyabiashara Hugo Kisima aliyekuwa akimiliki wa ukumbi wa Safari Resort maeneo ya Kimara.

Mnamo mwaka 1977 Maquis du Zaire waliamua kuongeza nguvu kwa kuimarisha kikosi chao. Hivyo uongozi huo ulimtuma Tchibangu Katayi ‘Mzee Paul’ kwenda Congo kutafuta wanamuziki wapya.‘Mzee Paul’ alibahatika kuwachukuwa akina Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’, Kanku Kelly, Ilunga Banza ‘Mchafu’, Mutombo Sozy na mnenguaji Ngalula Tshiandanda. Wakati huo walikuwa wakicheza katika mtindo wa ‘Chakula Kapombe’ ambao kwa watanzania ulikuwa mpya na ukapendwa mno na mashabiki.Kufika kwa wanamuziki hao kulileta mabadiliko makubwa sana katika muziki husuani tungo nzuri za Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ ambaye yaelezwa kuwa ndiye aliyeleta mapinduzi makubwa ya muziki hapa nchini Tanzania.

Maquis du Zaire wakaazisha mtindo mwingine wa ‘Kamanyola’, mtindo uliowapagaisha wapenzi na wadau toka pembe zote za jiji la Dar es Salaam. Mpulizaji wa Tarumbeta Mwema Mudjanga ‘Mzee Chekecha’ alikuwa akiwahamasisha wapenzi wake akitoavibwagizo vya “cheza Kamanyolaa.. ,cheza ukijidai’ cheza Kamanyola bila jasho…”

Mwaka huo wa 1977 mwishoni Maquis walimaliza mkataba na wakaondoka kwa Hugo Kisima. Bahati nyingine ikawaangukia tena kwani walisaini mkataba mwingine na Mzee Makao aliyekuwa akimiliki ukumbi wa Savannah, maeneo ya Ubungo. Wakiwa Savannah, walianzisha mitindo ya Sanifu na Ogelea piga mbizi baadaye ukumbi huo ukaitwa White House. Ikumbukwe kwamba wakati huohuo Maquis pia ilikuwa ikipiga kwenye ukumbi wa Mpakani, maeneo ya Mwenge. Ukumbi wa Mpakani baadaye ulibadilishwa jina kuwa Silent Inn. Kisha kuishia kuwa Kanisa.

Mwishoni mwaka 1978 waliamua kuimarisha tena kikosi chao kwa kuwaleta wanamuziki wengine wapya kutoka Congo ambao ni akina Kabeya Badu, Kalala Mbwebwe, Ngoyi Mubenga na Khatibu Iteyi Iteyi.Maquis du Zaire ilikuwa ikiongozwa na wanahisa akina Chinyama Chiyaza ‘Chichi’, Chibangu Katayi ‘Mzee Paul’, Chimbwiza Mbangu Nguza ‘Nguza Vicking’, Mutombo Lufungula ‘Audax’ na Mbuya Makonga ‘Adios’.

Chini ya uongozi huo miaka ya 1980 mafanikio makubwa yalionekana. Mojawapo ni lile la kuanzisha Orchestra Maquis Company (OMACO). Kampuni hiyo ilikuwa ikimiliki shamba la matunda, wakilima kwa kutumia matreka yao maeneo ya Mbezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mazao yao walikuwa wakiyapeleka na kuuza katika Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam.OMACO pia ilimiliki mradi mwingine wa viwanja tisa na nyumba kadhaa maeneo ya Sinza na pia waliwahi kuingia mkataba wa kuitangaza kampuni ya magari makubwa ya SCANIA.

Vijana wa wakati huo watakumbuka jinsi ukumbi wa White House ulivyokuwa ukifurika watu kila siku za Jumamosi, kuwashuhudia vijana wa Maquis du Zaire waliokuwa watanashati na nidhamu ya hali ya juu wakiwa jukwaani wakifanya vitu vyao.Enzi hizo ilikuwa ukiingia katika ukumbi huo wa White House, mbele yako macho lazima yakutane na mbao zilizo nakshiwa kwa maandishi ya majina ya wanamuziki wote na kukomelewa juu ya mwembe uliokuwa katikati ya ukumbi huo.

Maquis du Zaire ambayo ilikuwa ikipiga muziki mara moja kwa wiki, ilikuwa ikifika usiku wa manane, wanasisitisha muziki kwa muda na kusikika kipaza sauti kikiuliza “Wapenzi mumekuja na miswakii? Wapenzi walikuwa wakijibu “ndiyooooo…” Wanaelezwa dawa ya meno ipo hapo. Watu wengi hawakuwa na haja ya kuchukua teksi kurudi nyumbani kwani muziki wa Maquis du Zaire ulikuwa unarindima hadi alfajiri, muda ambao mabasi ya UDA ya Ikarus yalikuwa yameanza kazi.

Bendi hiyo ikiwa hapa nchini ilikuwa ikipiga na kucheza katika mitindo mbalimbali kwa nyakati tofauti. Mitindo hiyo ilikuwa ya Chakula kapombe, Kamanyola, Bishe Bishe, Zembwela, Chekecha na Ogelea Piga mbizi.Mwema Mudjanga ‘ Mzee Chekecha’ ndiye aliyekuwa akinogesha zaidi mitindo hiyo. Alikuwa kivutio kikubwa ukumbini licha ya kazi yake ya kupuliza tarumbeta, aliweza kuwainua vitini wapenzi kwenda kucheza, akitumia vibwagizo vya “Chekeee…. Chekechaaa” “Tusangalaa”, “Aima imaa”, ‘Bishe bishee”, “Saa… Sanifuu”, “cheza Kamanyolaa” “cheza kwa maringo”, “ Cheza ukijidai” na mengine mengi Maquis du Zaire wakati huo ilikuwa imesheheni wanamuziki zaidi ya 40 wenye vipaji vilivyopishana. Kwa idadi hiyo, laiti kama wangelikuwa na tamaa, wangeliweza kupiga muziki katika kumbi tatu tofauti kwa wakati mmoja.

Nina uhakika kwamba msomaji wangu unashauku ya kujua au kukumbushwa kikosi kamili kilichokuwa kinatengeneza Maquis du Zaire wakati huo. Nikianza na safu ya waimbaji walikuwepo akina Mbuya Makonga ‘Adios’, Mutombo Lufungula ‘Audax’, Mukumbule Lolembo ‘Parashi’, Kabeya Badu, Kalala Mbwebwe, mapacha Kassalo Kyanga na Kyanga Songa. Wengine walikuwa Kiniki Kieto, Abubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’, Mbombo wa Mbomboka, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’, Tshimanga Kalala Assosa, Kabeya Badu, Masiya Radi ‘Dibakuba kuba’, Issa Nundu na waimbaji wa kike Tabia Mwanjelwa, Rahma Shaari na Anna Mwaole.

Wapiga gita la solo alikuwepo Chimbwiza Nguza Mbangu ‘Nguza Vicking’ ambaye kwa umahiri wake wa kulicharanza gita hilo, wapenzi walimpachika cheo cha juu kabisa jeshini cha ‘Field Marshal’ Wengine katika gitaa hilo walikuwa akina Ilunga Lubaba, Dekula Kahanga ‘Vumbi’ na Mbwana Suleiman ‘Mbwana Cox’.Gitaa la rhythm walikuwepo Mulenga Kalonji ‘Vata’, Omari Makuka na Steven Kaingilila Mauffi. Bila kuwashau akina Mbambu Kazadi, Mondo Mondonde na Nawayi Kabwila. Gitaa zito la besi lilikuwa likiungurumishwa na Ilunga Banza ‘Banza Mchafu’ ambaye aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kulicharaza gita hilo akiwa kajitwisha kwenye upara uliozungushiwa simbi kichwani kwake. Wengine walikuwa Ibrahimu na Mujos wa Bayeke.

Kama nilivyokujuza hapo awali kwamba bendi hiyo ilikuwa imejaza mseto wa vipaji mbalimbali. Kwa upande wa wapuliza Saxophone ‘mdomo ya bata’ walikuwepo akina Mafumu Bilali ‘Bombenga/‘Super Sax’, Khatibu Iteyi Iteyi, Kalamzoo, Alex Kanyimbo, Akulyake Suleimani ‘King Mallu’, Roy Mukuna ‘Mukuna wa Mukuna’, Chibangu Katayi , Comson Mkomwa na Majengo Selemani Wapuliza tarumbeta walikuwepo akina Mwema Mudjanga ‘Mzee Chekecha’ Nkashama Kanku Kelly, Mioma wa Mwamba ‘Mzee Tito’, Kayembe Ndalabuu ‘Trumbloo’, Mpoyo Kalenga, Berry Kankonde, Kaumba Kalemba, Ngoi Mubenga, Ilunga Ngoi ‘Bizos’, Morgan Machege na Ngenda Kalonga.

Madoido na mbwembwe hizo, ziliwavutia wapenzi wengi na kupenda kuhamishia viti vyao wakisogea sehemu iliyokuwa karibu, ili kushuhudia vijana hao wakifanya maajabu ya kuchezea vyombo hivyo.Pamoja na uimbaji Mbuya Makonga ‘Adios’ alikuwa mbonyezaji wa kinada huku Mutombo Sozzy akizicharaza drums akisaidiana na Matei Joseph. Tumba zilikuwa zikigongwa na Siddy Morris ‘Super Konga’ na Pulukulu Wabandoki Motto.Walikuwepo na wanenguaji mahiri ambao walikuwa wakitoa burudani za pekee akina ‘Washa Washa’, Dulla ‘Panga Panga’, Wandema Rashid, Anna Mganga, Kinacho, Mwajuma, Frida Shirima, Zuwena na Ngalula Tshiandanda, wakiongozwa na Nkulu Wabangoi.

Ikiwa White House bendi hiyo ilitoka na vibao vingi vikiwemo vya Double double, Clara, Kyembe, Maiga, Mpenzi Luta, Mwana yoka ya Babote, Ngalula, Nasononeka, Nimepigwa ngwala, Promotion, Ngalula, Karubandika na Noelle Bonane wimbo ambao ulikuwa ukipigwa mahsusi nyakati za Krimasi na mwaka mpya. Zingine zilikuwa Dora mtoto wa Dodoma, Balimwacha, Malokelee, Promotion, Seya, Sophia, Sumu ya mapenzi, Sababu ya nini, Zowa, Uba, Safari ya Mbeya, Wakati nikiwa mdogo na nyingine nyingi zisizo idadi.

Kuna msemo usemao “Cha kuazima hakistiri maungo” msemo huo uliisibu bendi ya Maquis du Zaire baada ya kiungia katika maelewano ‘hafifu’ na mmili wa ukumbi wa White House hadi kulazimika kuondoka wakiacha ukumbi huo ukibadilishwa kuwa gereji hadi leo.Baadaye bendi hiyo ikabadilishwa jina na kuwa Maquis Original wakipiga muziki katika kumbi za Wapiwapi’s pale maduka mawili, Chang’ombe na CCM Kata ya 14 Temeke, kabla ya kuhamia ukumbi mpya kwa wakati huo wa Lang’ata pale Kinondoni Maquis Original ilileta wanamuziki wengine toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo muda mfupi kabla ya mpiga gitaa la solo, Dekula Kahanga ‘Vumbi’ kuondoka kwenda Stockholm nchini Sweden.

Wanamuziki hao walikuwa Kivugutu Motona Chatcho (Solo), na waimbaji Freditto Butamu na Luhembwe Mwahitwa ‘Bobo Sukari’.Walitikisa ukumbi wa Lang’ata kwa nyimbo zao kali za Mangolibo, Mayanga, Makumbele, zikisindikizwa na wimbo wa Ngalula ambapo wakati wa chorus katika wimbo huo, Tshimanga Assosa alikuwa akimpandisha mori mpiga gita la solo Dekula Kahanga ‘Vumbi’ akimwita “vumbiii… Vimbiiii… Vumbiii…” Nyimbo za Maquis Original zilikuwa zikipigwa na kutamba kwa staili za ‘Washawasha’ na ‘Sendema’.

Maquis Original ikiwa Lang’ata, kuna shabiki mmoja aliyejulikana kwa jina la ‘Magoma moto’ ambaye alikuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa Maquis. Alikuwa akiachwa uwanja akionehsa uhodari wake wa kucheza mtindo wa ‘Sendema’ huku akiwa kajitwisha chupa yenye Bia juu ya kichwa chake.

Ni miaka takriban 23 toka jina la Maquis litoweke masikioni mwa wadau na wapenzi wa muziki wa dansi baada ya kusambaratika katika miaka ya 1990, ikiwaachia simanzi na majonzi wapenzi wake yasiyokwisha hadi leo. Lakini Tshimanaga Kalala Assosa ‘mtoto mzuri’ baadaye alitumia weledi wake katika muziki kwa kuienzi jina la Maquis kwa kuanzaisha bendi ya ‘Bana Maquis’ ambayo hupiga na kukumbushia nyimbo zilizopigwa na Maquis du Zaire na Maquis Original.

Ikumbukwe kwamba idadi kubwa miongoni mwa wanamuziki wanaotajwa humu, wameshatangulia mbele za haki.Wengine ni wale wanaumwa maradhi mbalimbali akina Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’, Mbombo wa Mboka na Mutombo Lufungula ‘Audax’

Mungu aziweke roho zao pahala pema peponi waliotangulia mbele za haki na awape tahfifu wanaoumwa, Amen

KASONGO+&+NGUZA.jpg

Nguza Vicking akilicharaza gita la solo na nyuma yake ni Kasongo Mpnda 'Clayton' mwimbaji wa bendi hiyo.

MCHAFU+-+DEKULA.jpg

Wapiga magita Dekula Kahanga 'Vumbi' na Ilunga Banza 'Mchafu' (kushoto) wakionesha manjonjo ya kupiga gita sakafuni.

KASALOO,KASONGO+&+KYANGA.jpg

Waimbaji wa Maquis du Zaire Kasongo Mpinda (katikati) na mapacha Kasalo Kyanga na Kyanga Songa (kulia)

SIDY+MORRIS.jpg

Mpiga tumba Sidy Morris 'Super Konga' akionyesha mbwembwe za kupiga tumba hizo kwa mikono na mguu

Kanku+Saxophone.jpg

Mpulizaji wa Tarumbeta wa Maquis du Zaire, Nkashama Kanku Kelly akifanya vitu v
CHINYAMA+CHIYAZA.jpg

Kiongozi wa Maquis du Ziare, Chinyama Chiyaza akicheza katika mtindo wa 'Chakula kapombe' unavyochezwa

vumbi+4+DEKULA.jpg

Wanamuziki wa bendi ya Maquis du Zaire wakiwa katika picha ya pamoja. Toka kushoto ni Suleiman Mbwana' Cox', Mbuya Makonga 'Adios', Mujos wa Bayeke, Steven Kaingila Mauffi na dekula Kahanga 'Vumbi'. Wengine ni Issa Nundu, Mukumbule Lolembo 'Parashi' na Roy Mukuna 'Mukuna wa Mukuna.

maquis+dodoma.jpg

Aiseeh !!!

Mlimani.jpg

....Mbali sana !!!

Shukrani mingi sana papaa Kiyungi Mutu ya watu !!
 
Mlifaidi sana enzi zenu,mimi si wa enzi hizo lakini mpenzi mkubwa wa nyimbo za zamani,kipindi ambacho muziki ulikuwa muziki,nilishuhudia onyesho la bendi ya Mashujaa daah ni mikelele tu,...mkuu hivi Mzee Hugo Kisima yu hai?...
 
Kweli inakumbusha mbali. Hao waliowekewa X bila shaka wametangulia mbele za haki, ni akina nani?
 
Kuna wimbo mmoja naukubali sana kwa hawa jamaa walong kidogo unaitwa kiongo
Bass alipiga ilunga lubaba
Solo nguza viking
Waimbaji kasongo na wengine
 
...
MAQUIS du ZAIRE ni bendi ambayo iliwatesa Watanzania kwa kuwaporomoshea burudani za muziki wa dansi maridhawa katika kumbi mbalimbali hapa nchini Kwa wale waliokuwa vijana kati ya miaka ya 1970 na 1990, katu hawawezi kuisahau bendi hiyo ambayo iliingia hapa nchini kwa kishindo kikubwa ikitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Zaire) wakati huo. Mwaka 1981, niliwahi kufanya mahojiano maalumu na mmoja wa viongozi wa bendi hiyo Chimbwiza Mbangu Nguza Vicking ambaye alinipa wasifu wa bendi hiyo ya Maquis du Zaire.Kwa kuwa wasifu huo uandikwa na kuchapishwa katika gazeti la serikali la Nchi Yetu la kila mwezi, ambalo lilikuwa likuzwa kwa senti 30, likitolewa na mwajiri wangu wakati huo, Idara ya habari (MAELEZO).

Hivyo basi si vibaya nikirejea kuwapasha wale ambao hawafahamu na kwa waliosahau, nichukue muda wenu kwa kuwapa wasifu wa bendi hiyo tangia ilivyoanzishwa hadi kutoweka kwake katika taswira ya muziki. Historia ya bendi hiyo inaanzia mwaka 1960 kwa waliokuwa vijana wa wakati huo katika mji wa Kamina huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Zaire), walioungana na kuunda bendi yao wakaiita Super Theo.

Bendi hiyo ilitoa burudani tosha kwa wapenzi wa muziki wa Kamina na vitongoji vinavyouzunguka mji huo, baadaye wakaibadilisha jina kuwa Super Gabby.Katika kile kilichoelezwa na uongozi wa Super Gabby kuwa ni kuleta mageuzi katika muziki, bendi hiyo mwaka 1972, ilibadili jina rasmi na kuwa Maquis du Zaire.

Maquis du Zaire iliingia hapa Tanzania mwaka huohuo wa 1972, kwa mwaliko wa mfanyabishara maarufu Mzee Batengas. Walianza kutumbuiza kwa mkataba katika ukumbi wa Mikumi Tours uliokuwa maeneo la Tazara Buguruni, jijini Dar es Salaam. Baada ya kumaliza mkataba wao waliachana na Mzee Batengas, wakaenda kupiga muziki katika Klabu ya Hunters kwa kipindi kifupi. Kisha viongozi wa bendi hiyo wakafanya mazungumzo na mfanyabiashara Hugo Kisima aliyekuwa akimiliki wa ukumbi wa Safari Resort maeneo ya Kimara.

Mnamo mwaka 1977 Maquis du Zaire waliamua kuongeza nguvu kwa kuimarisha kikosi chao. Hivyo uongozi huo ulimtuma Tchibangu Katayi Mzee Paul kwenda Congo kutafuta wanamuziki wapya.Mzee Paul alibahatika kuwachukuwa akina Kikumbi Mwanza Mpango King Kiki, Kanku Kelly, Ilunga Banza Mchafu, Mutombo Sozy na mnenguaji Ngalula Tshiandanda. Wakati huo walikuwa wakicheza katika mtindo wa Chakula Kapombe ambao kwa watanzania ulikuwa mpya na ukapendwa mno na mashabiki.Kufika kwa wanamuziki hao kulileta mabadiliko makubwa sana katika muziki husuani tungo nzuri za Kikumbi Mwanza Mpango King Kiki ambaye yaelezwa kuwa ndiye aliyeleta mapinduzi makubwa ya muziki hapa nchini Tanzania.

Maquis du Zaire wakaazisha mtindo mwingine wa Kamanyola, mtindo uliowapagaisha wapenzi na wadau toka pembe zote za jiji la Dar es Salaam. Mpulizaji wa Tarumbeta Mwema Mudjanga Mzee Chekecha alikuwa akiwahamasisha wapenzi wake akitoavibwagizo vya cheza Kamanyolaa.. ,cheza ukijidai cheza Kamanyola bila jasho

Mwaka huo wa 1977 mwishoni Maquis walimaliza mkataba na wakaondoka kwa Hugo Kisima. Bahati nyingine ikawaangukia tena kwani walisaini mkataba mwingine na Mzee Makao aliyekuwa akimiliki ukumbi wa Savannah, maeneo ya Ubungo. Wakiwa Savannah, walianzisha mitindo ya Sanifu na Ogelea piga mbizi baadaye ukumbi huo ukaitwa White House. Ikumbukwe kwamba wakati huohuo Maquis pia ilikuwa ikipiga kwenye ukumbi wa Mpakani, maeneo ya Mwenge. Ukumbi wa Mpakani baadaye ulibadilishwa jina kuwa Silent Inn. Kisha kuishia kuwa Kanisa.

Mwishoni mwaka 1978 waliamua kuimarisha tena kikosi chao kwa kuwaleta wanamuziki wengine wapya kutoka Congo ambao ni akina Kabeya Badu, Kalala Mbwebwe, Ngoyi Mubenga na Khatibu Iteyi Iteyi.Maquis du Zaire ilikuwa ikiongozwa na wanahisa akina Chinyama Chiyaza Chichi, Chibangu Katayi Mzee Paul, Chimbwiza Mbangu Nguza Nguza Vicking, Mutombo Lufungula Audax na Mbuya Makonga Adios.

Chini ya uongozi huo miaka ya 1980 mafanikio makubwa yalionekana. Mojawapo ni lile la kuanzisha Orchestra Maquis Company (OMACO). Kampuni hiyo ilikuwa ikimiliki shamba la matunda, wakilima kwa kutumia matreka yao maeneo ya Mbezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mazao yao walikuwa wakiyapeleka na kuuza katika Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam.OMACO pia ilimiliki mradi mwingine wa viwanja tisa na nyumba kadhaa maeneo ya Sinza na pia waliwahi kuingia mkataba wa kuitangaza kampuni ya magari makubwa ya SCANIA.

Vijana wa wakati huo watakumbuka jinsi ukumbi wa White House ulivyokuwa ukifurika watu kila siku za Jumamosi, kuwashuhudia vijana wa Maquis du Zaire waliokuwa watanashati na nidhamu ya hali ya juu wakiwa jukwaani wakifanya vitu vyao.Enzi hizo ilikuwa ukiingia katika ukumbi huo wa White House, mbele yako macho lazima yakutane na mbao zilizo nakshiwa kwa maandishi ya majina ya wanamuziki wote na kukomelewa juu ya mwembe uliokuwa katikati ya ukumbi huo.

Maquis du Zaire ambayo ilikuwa ikipiga muziki mara moja kwa wiki, ilikuwa ikifika usiku wa manane, wanasisitisha muziki kwa muda na kusikika kipaza sauti kikiuliza Wapenzi mumekuja na miswakii? Wapenzi walikuwa wakijibu ndiyooooo Wanaelezwa dawa ya meno ipo hapo. Watu wengi hawakuwa na haja ya kuchukua teksi kurudi nyumbani kwani muziki wa Maquis du Zaire ulikuwa unarindima hadi alfajiri, muda ambao mabasi ya UDA ya Ikarus yalikuwa yameanza kazi.

Bendi hiyo ikiwa hapa nchini ilikuwa ikipiga na kucheza katika mitindo mbalimbali kwa nyakati tofauti. Mitindo hiyo ilikuwa ya Chakula kapombe, Kamanyola, Bishe Bishe, Zembwela, Chekecha na Ogelea Piga mbizi.Mwema Mudjanga Mzee Chekecha ndiye aliyekuwa akinogesha zaidi mitindo hiyo. Alikuwa kivutio kikubwa ukumbini licha ya kazi yake ya kupuliza tarumbeta, aliweza kuwainua vitini wapenzi kwenda kucheza, akitumia vibwagizo vya Chekeee. Chekechaaa Tusangalaa, Aima imaa, Bishe bishee, Saa Sanifuu, cheza Kamanyolaa cheza kwa maringo, Cheza ukijidai na mengine mengi Maquis du Zaire wakati huo ilikuwa imesheheni wanamuziki zaidi ya 40 wenye vipaji vilivyopishana. Kwa idadi hiyo, laiti kama wangelikuwa na tamaa, wangeliweza kupiga muziki katika kumbi tatu tofauti kwa wakati mmoja.

Nina uhakika kwamba msomaji wangu unashauku ya kujua au kukumbushwa kikosi kamili kilichokuwa kinatengeneza Maquis du Zaire wakati huo. Nikianza na safu ya waimbaji walikuwepo akina Mbuya Makonga Adios, Mutombo Lufungula Audax, Mukumbule Lolembo Parashi, Kabeya Badu, Kalala Mbwebwe, mapacha Kassalo Kyanga na Kyanga Songa. Wengine walikuwa Kiniki Kieto, Abubakar Kasongo Mpinda Clayton, Mbombo wa Mbomboka, Kikumbi Mwanza Mpango King Kiki, Tshimanga Kalala Assosa, Kabeya Badu, Masiya Radi Dibakuba kuba, Issa Nundu na waimbaji wa kike Tabia Mwanjelwa, Rahma Shaari na Anna Mwaole.

Wapiga gita la solo alikuwepo Chimbwiza Nguza Mbangu Nguza Vicking ambaye kwa umahiri wake wa kulicharanza gita hilo, wapenzi walimpachika cheo cha juu kabisa jeshini cha Field Marshal Wengine katika gitaa hilo walikuwa akina Ilunga Lubaba, Dekula Kahanga Vumbi na Mbwana Suleiman Mbwana Cox.Gitaa la rhythm walikuwepo Mulenga Kalonji Vata, Omari Makuka na Steven Kaingilila Mauffi. Bila kuwashau akina Mbambu Kazadi, Mondo Mondonde na Nawayi Kabwila. Gitaa zito la besi lilikuwa likiungurumishwa na Ilunga Banza Banza Mchafu ambaye aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kulicharaza gita hilo akiwa kajitwisha kwenye upara uliozungushiwa simbi kichwani kwake. Wengine walikuwa Ibrahimu na Mujos wa Bayeke.

Kama nilivyokujuza hapo awali kwamba bendi hiyo ilikuwa imejaza mseto wa vipaji mbalimbali. Kwa upande wa wapuliza Saxophone mdomo ya bata walikuwepo akina Mafumu Bilali Bombenga/Super Sax, Khatibu Iteyi Iteyi, Kalamzoo, Alex Kanyimbo, Akulyake Suleimani King Mallu, Roy Mukuna Mukuna wa Mukuna, Chibangu Katayi , Comson Mkomwa na Majengo Selemani Wapuliza tarumbeta walikuwepo akina Mwema Mudjanga Mzee Chekecha Nkashama Kanku Kelly, Mioma wa Mwamba Mzee Tito, Kayembe Ndalabuu Trumbloo, Mpoyo Kalenga, Berry Kankonde, Kaumba Kalemba, Ngoi Mubenga, Ilunga Ngoi Bizos, Morgan Machege na Ngenda Kalonga.

Madoido na mbwembwe hizo, ziliwavutia wapenzi wengi na kupenda kuhamishia viti vyao wakisogea sehemu iliyokuwa karibu, ili kushuhudia vijana hao wakifanya maajabu ya kuchezea vyombo hivyo.Pamoja na uimbaji Mbuya Makonga Adios alikuwa mbonyezaji wa kinada huku Mutombo Sozzy akizicharaza drums akisaidiana na Matei Joseph. Tumba zilikuwa zikigongwa na Siddy Morris Super Konga na Pulukulu Wabandoki Motto.Walikuwepo na wanenguaji mahiri ambao walikuwa wakitoa burudani za pekee akina Washa Washa, Dulla Panga Panga, Wandema Rashid, Anna Mganga, Kinacho, Mwajuma, Frida Shirima, Zuwena na Ngalula Tshiandanda, wakiongozwa na Nkulu Wabangoi.

Ikiwa White House bendi hiyo ilitoka na vibao vingi vikiwemo vya Double double, Clara, Kyembe, Maiga, Mpenzi Luta, Mwana yoka ya Babote, Ngalula, Nasononeka, Nimepigwa ngwala, Promotion, Ngalula, Karubandika na Noelle Bonane wimbo ambao ulikuwa ukipigwa mahsusi nyakati za Krimasi na mwaka mpya. Zingine zilikuwa Dora mtoto wa Dodoma, Balimwacha, Malokelee, Promotion, Seya, Sophia, Sumu ya mapenzi, Sababu ya nini, Zowa, Uba, Safari ya Mbeya, Wakati nikiwa mdogo na nyingine nyingi zisizo idadi.

Kuna msemo usemao Cha kuazima hakistiri maungo msemo huo uliisibu bendi ya Maquis du Zaire baada ya kiungia katika maelewano hafifu na mmili wa ukumbi wa White House hadi kulazimika kuondoka wakiacha ukumbi huo ukibadilishwa kuwa gereji hadi leo.Baadaye bendi hiyo ikabadilishwa jina na kuwa Maquis Original wakipiga muziki katika kumbi za Wapiwapis pale maduka mawili, Changombe na CCM Kata ya 14 Temeke, kabla ya kuhamia ukumbi mpya kwa wakati huo wa Langata pale Kinondoni Maquis Original ilileta wanamuziki wengine toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo muda mfupi kabla ya mpiga gitaa la solo, Dekula Kahanga Vumbi kuondoka kwenda Stockholm nchini Sweden.

Wanamuziki hao walikuwa Kivugutu Motona Chatcho (Solo), na waimbaji Freditto Butamu na Luhembwe Mwahitwa Bobo Sukari.Walitikisa ukumbi wa Langata kwa nyimbo zao kali za Mangolibo, Mayanga, Makumbele, zikisindikizwa na wimbo wa Ngalula ambapo wakati wa chorus katika wimbo huo, Tshimanga Assosa alikuwa akimpandisha mori mpiga gita la solo Dekula Kahanga Vumbi akimwita vumbiii Vimbiiii Vumbiii Nyimbo za Maquis Original zilikuwa zikipigwa na kutamba kwa staili za Washawasha na Sendema.

Maquis Original ikiwa Langata, kuna shabiki mmoja aliyejulikana kwa jina la Magoma moto ambaye alikuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa Maquis. Alikuwa akiachwa uwanja akionehsa uhodari wake wa kucheza mtindo wa Sendema huku akiwa kajitwisha chupa yenye Bia juu ya kichwa chake.

Ni miaka takriban 23 toka jina la Maquis litoweke masikioni mwa wadau na wapenzi wa muziki wa dansi baada ya kusambaratika katika miaka ya 1990, ikiwaachia simanzi na majonzi wapenzi wake yasiyokwisha hadi leo. Lakini Tshimanaga Kalala Assosa mtoto mzuri baadaye alitumia weledi wake katika muziki kwa kuienzi jina la Maquis kwa kuanzaisha bendi ya Bana Maquis ambayo hupiga na kukumbushia nyimbo zilizopigwa na Maquis du Zaire na Maquis Original.

Ikumbukwe kwamba idadi kubwa miongoni mwa wanamuziki wanaotajwa humu, wameshatangulia mbele za haki.Wengine ni wale wanaumwa maradhi mbalimbali akina Aboubakar Kasongo Mpinda Clayton, Mbombo wa Mboka na Mutombo Lufungula Audax

Mungu aziweke roho zao pahala pema peponi waliotangulia mbele za haki na awape tahfifu wanaoumwa, Amen

KASONGO+&+NGUZA.jpg

Nguza Vicking akilicharaza gita la solo na nyuma yake ni Kasongo Mpnda 'Clayton' mwimbaji wa bendi hiyo.

MCHAFU+-+DEKULA.jpg

Wapiga magita Dekula Kahanga 'Vumbi' na Ilunga Banza 'Mchafu' (kushoto) wakionesha manjonjo ya kupiga gita sakafuni.

KASALOO,KASONGO+&+KYANGA.jpg

Waimbaji wa Maquis du Zaire Kasongo Mpinda (katikati) na mapacha Kasalo Kyanga na Kyanga Songa (kulia)

SIDY+MORRIS.jpg

Mpiga tumba Sidy Morris 'Super Konga' akionyesha mbwembwe za kupiga tumba hizo kwa mikono na mguu

Kanku+Saxophone.jpg

Mpulizaji wa Tarumbeta wa Maquis du Zaire, Nkashama Kanku Kelly akifanya vitu v
CHINYAMA+CHIYAZA.jpg

Kiongozi wa Maquis du Ziare, Chinyama Chiyaza akicheza katika mtindo wa 'Chakula kapombe' unavyochezwa

vumbi+4+DEKULA.jpg

Wanamuziki wa bendi ya Maquis du Zaire wakiwa katika picha ya pamoja. Toka kushoto ni Suleiman Mbwana' Cox', Mbuya Makonga 'Adios', Mujos wa Bayeke, Steven Kaingila Mauffi na dekula Kahanga 'Vumbi'. Wengine ni Issa Nundu, Mukumbule Lolembo 'Parashi' na Roy Mukuna 'Mukuna wa Mukuna.

maquis+dodoma.jpg

Aiseeh !!!

Mlimani.jpg

....Mbali sana !!!

Shukrani mingi sana papaa Kiyungi Mutu ya watu !!
HABARI HII NI KTK HABARI ZISIZO NA MAANA YYTE. WEKA HABARI ZENYE MANUFAA KWA JAMII.
 
Hivi naomba kujua kama huyu Mutombo Sozzy wa Marquiz du Zaire ndiye pia anaitwa Thomas Mutombo Kayembe (Toma)
 
Way back
 
Back
Top Bottom