Optimal Profit Margin for Grain Milling Business in Tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Optimal Profit Margin for Grain Milling Business in Tz

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by allan, Aug 15, 2012.

 1. allan

  allan Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Habarini wana bodi!

  Tafadhalini rejea kichwa cha habari hapo juu.

  Hivi karibuni nimekutana na tathmini ya biashara moja ya kukoboa na kusaga mahindi iliyopo mkoa wa jirani na Dar inaonyesha kuwa wana profit margin ya 98% katika mwaka wa kibiashara uliopita. Nikajaribu kudadisi zaidi kwa biashara nyingine zinazofanana na hizo nikakuta wenyewe wanarange 10% hadi 65%.

  Nikabaki na maswali mengi najiuliza ina maana biashara ya kusaga na kukoboa nafaka inaweza ikawa na profit margin kubwa kiasi hicho kwa mwaka uliopita ukiachilia mbali changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta hii ikiwemo ya umeme usioaminika na bei yake kuwa juu au kuna ka uchakachuaji katika zoezi la kuandaa hizo taarifa?!

  Naombwa kujuzwa wakuu, kwa wenye ujuzi na uzoefu wa hii kitu je inaweza kuwa kweli kwa mazingira yetu haya ya kibiashara humu nchini kuwa na profit margin hiyo kwa biashara ya kusaga na kukoboa nafaka (mahindi)? Na je kwa mliobahatika kuona / kupitia / kuandaa taarifa kama hizo range ya profit margin ilikua ngapi kwa maeneo hayo?

  Naomba kuwakilisha na karibuni kwa michango yenu!
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Profit margin ya 98% sounds very unrealistic kwa mazingira yetu! Gharama ya umeme,mafuta, wafanyakazi etc
   
 3. allan

  allan Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Ndicho nilichokiwaza mkuu SMU, vp we kwa uzoefu wako PM kwa biashara hizo huwa inarange ngapi kwa maeneo uliyopo?
   
 4. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu naona unafanya kautafiti kidogo, na pengine wanajamvi tunajibu questioner zako bila kujua. Anyway hebu jaribu kupitia hiyo report vizuri maana nafaka hapa kwetu haina kodi na hii inaweza kua moja ya incentive kusukuma profit margin lakini sio kwa asilimia hizo tajwa,
  Kuna makampuni kama Azania wanaagiza ngano kutoka Russia wanaikoboa na kupaki unga wanauuza hapa nchini na nje ila hakuna kodi, hata mkopo waliowezeshwa na mkulu hawana mpango wakurudisha. Sasa sijui profit margin zao zikoje hawa.
   
 5. allan

  allan Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Mwanahisa, sipo kwenye kautafiti mkuu. Ingekua ni kautafiti ningemwomba Invisible aniwekee link ya questionnaire yangu hapo juu ili kila mdau atakaeguswa achangie mawazo!! Najaribu tu kupata uzoefu na mawazo ya wadau ili niondoe huu wasiwasi niliokua nao.

  Enewei, nimeipata point yako mkuu. Ila kwa hawa wenye biashara za kiwango cha chini na cha kati huwa wanalipa ushuru wa mazao wanapofata malighafi sokoni + kodi ya mapato. Kwa hao wakubwa nafikiri ni muendelezo wa udahifu wa sirikali yetu ndo maana nchi haimbulii chochote kwenye biashara zao.

  Vipi kwa eneo ulilopo PM za wale wenye biashara hizi katika small scale na medium zinarange ngapi?
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Labda kuna kitu tukiweke sawa kwanza kabla hatujaendelea. Hii biashara ya 'kukoboa na kusaga' tunayoizungumzia, ile ya wewe kununua mazao, kuyakoboa/kusaga, na kisha kuuza (products only) au ni biashara ambayo wewe unamiliki mashine tu za kukoboa na kusaga na kutoa huduma hiyo kibiashara kwa watu wengine (services only) au ni both?
   
 7. allan

  allan Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Hii biashara tunayoizungumzia ni ile ya mtu kumiliki mashine ya kukoboa na kusaga, either akiwa anafanya toll milling (kutoa huduma) au anafanya resale (ananunua mzigo - mahindi na kuuza unga) au anafanya zote.
   
Loading...