Watu wengine bana sasa wanaomshangilia Lowassa wanafanya hivyo kwa sababu ya mawazo yao?
Tukitaka mabadiliko ambayo ni perfect itatubidi tusubiri miaka kama mia tano kutoka sasa.
Kama ilivyo kwa amani, ili kufikia amani kuu tunahitaji amani ndogo kwanza.
Ili kufikia elimu kubwa tunahitaji elmu ndogo kwanza.
Vivyo hivyo ili kufikia mabadiliko makuu na ya kweli tunahitaji mabadiliko madogo na ya kati.
Mwanzoni sikuelewa EL alpoamia CDM lakini kilicho wazi ni kuwa akiwa rais maana yake atapitia kwenye coridor tofauti na zile zilizozoeleka kwa miaka 50, yaani za Lumumba. Na wanazi, wanafiki, wachawi tofauti.
Maana yake ni kwamba hata Magufuli atajaribu hayo mabadiliko lakini ataishia 15% lakini Lowassa anaweza kutufikisha hata 65% ambayo ni bora zaidi! Tatizo mnataka mtuaminishe kuwa inadidi afikie 100% kwa ubora kitu amabcho hakijawahi kuwepo duniani.
Haya Makamanda kumekucha tena.
Tunaamini kabisa kuwa hata bila Lowassa CHADEMAilikuwa na nafasi kubwa na nzuri zaidi ya kuing'oa CCM madarakani na badoikabakia na sura yake kama chama chenye kutaka na kusimamia uadilifu, utawalabora, maono bora kwa taifa na uongozi bora.
Kamari hii ya kisiasa yaani ‘political gamble' imeweka hatima za Mbowe naLowassa kisiasa na hata kiuongozi kwenye sanduku la kura ifikapo Oktoba 25.
Inawezekana basi – na uwezekano huu ni vigumu kuupinga kwa hoja – madazote na mazungumzo yote yaliyofanywa na viongozi kama Mbowe, Lissu, Mnyika nawengine juu ya kuhusisha ufisadi na uongozi wa Lowassa yalikuwa ni geresha tuya kumchagua ili CCM imkate ili wao wampate! Kwamba, yote yaliyokuwa yakisemwajuu ya Lowassa na kuitwa "ushahidi" yalikuwa ni ulaghai usio kifani uliokuwa nalengo la kumfanya Lowassa asiaminike na asikubalike na wenzake CCM chamaambacho kilimlea na kumjenga kisiasa ili hatimaye aje upande huu.
Kamari hii hata hivyo ilifanya makosa makubwamawili ambayo kwa hakika yatamnyika Lowassa ushindi, kuleta mgogoro mkubwaCHADEMA na washirika wake na hatimaye kufunika hatima za kisiasa za Mbowe nakundi la wale walioungana naye kumleta Lowassa nyumbani.
Kosa la kwanza, ni kuwa walitegemea kuwa ujiowa Lowassa ungeigawa CCM pande mbili na kuidhoofisha. Badala yake CCMhaikumeguka kama ilivyotarajiwa. Hadi hivi sasa hakuna kiongozi yeyote wa CCMaliyeondoka kwenda CDM ambaye alikuwa bado na nafasi CCM!
Ana kutaka kuendelea na utawala wa CCMiliyomeguka chini ya mgombea Magufuli (au mwingine yeyote) au kumfuata Lowassaalipo na kundi la watu kama milioni moja wenye kumuamini au kumfuata kiongoziambaye tayari amejionesha ni mwanameguezi wa kweli, na ambaye ameshalipagharama kubwa ya kukiandaa chama na uchaguzi huu mkuu. CHADEMA isingekuwaimegawanyika ingekuwa moja, ingepata kura za wananchi ambao tayari wanaiungamkono n ahata wana CCM ambao hawakuwa tayari kuendelea na CCM wala kumfuataLowassa aliko.
Upande mmoja ni Magufuli na taasisi ya CCM namifumo yake yote na upande mwingine Lowassa – peke yake; hana taasisi –akitegemea nguvu ya jina lake tu wala siyo historia yake au maono yake kamakiongozi wa upinzani.
Ni vigumu kuona ni jinsi gani Lowassaanashinda ati kwa vile watu wanataka tu ashinde au wanaamini watu wameichokaCCM! CCM hii ambayo sasa inaonekana imepewa uhai mpya kwa kuondokewa na watuwake waliokuwa matata sana ina nafasi kubwa zaidi ya kushinda kuliko CDM ambayoilijivuruga yenyewe kw akutafuta njia ya mkato kutaka ushindi.
Kamari haitalipa; Lowassa atagaragazwa nakuvuruga kwa muda mrefu ujao harakati za mabadiliko ambazo nusura zingezaamatunda mwaka huu.