Operesheni tokomeza ujangili haitafanikiwa kamwe mpaka operesheni tokomeza CCM itakapofanikiwa!

g riot master

Senior Member
Dec 15, 2013
103
7
Ndg wanajamvi,
Kama kuna tukio kubwa lililotisha taifa letu mwishoni mwa mwaka 2013 basi ni yale madhila yaliyotokana na OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI. Kimsingi hii ni operesheni sahihi kabisa ili kuweza kunusuru mali asili ya taifa letu. Lakini operesheni iliendeshwa bila kugusa wahusika wenyewe na pengine wasingegusika maana ndio washika dola. Ebu tafakari watuhumiwa wafuatao waliotajwa na vyombo mbalimbali wa habari ktk nyakati tofauti:

1. IKULU
Toyota Land Cruiser mali ya ikulu iliyowahi kukamatwa na shehena ya meno ya tembo baada ya kupata ajali maeneo ya Kibiti

2. JESHI LA WANANCHI (JWTZ)
Gari la JESHI LA WANANCHI (JWTZ) lililowahi kukamatwa na shehena ya meno ya tembo maeneo ya Ikwiri- Rufiji

3. MAKADA WA CCM
Imekuwa kama kawaida makada wa chama hiki kutajwa kuwa wahusika wakuu katika ujangili wa wanyama wetu na ndio maana haikushangaza moja ya order iliyotolewa kwa kikosi cha operesheni wakati wa operesheni tokomeza ni kutokamata viongozi wa chama. (Rejea taarifa ya kamati ya uchunguzi ya Bunge chini ya m/kiti Lembeli)
source: Raia Mwema Jan 1-Jan 7 2014 pp. 12-13

Wanajamvi tupime kwa pamoja kama serikali ya ccm ndio wahusika wakuu nani atatokomeza ujangili? Jibu ni wazi ni WANANCHI KUTOKOMEZA CCM ili mipango ya kweli ya kutokomeza ujangili ifanikiwe.

MANTIKI NI RAHISI:
TOKOMEZA CCM = WANYAMA WAPONE au
OKOA CCM = WANYAMA WAISHE! Haya kazi kwetu.
 
...naunga mkono hoja mia kwa mia,operation tokomeza ccm...
 
Umesema kweli kabisa watatokomezaje watu wanakamata majangiri ya kichina na meli zao na kuwaachia baada ya kupigiwa simu toka sehemu sehemu
 
Back
Top Bottom