Operator wa mitambo: Heavy Duty equipments!

Operator wa mitambo: Heavy Duty equipments!

New Rider

Senior Member
Joined
Jun 29, 2021
Posts
131
Reaction score
269
Habari wakuu, Mimi ni operator wa mitambo ya kutengeneza barabara , nimesomea chuo cha mitambo cha Veta Shinyanga , Nina cheti na leseni pia.

Ni operator wa mitambo ya Motor Grader, Hydraulic Excavator na wheel loader. Fresh from college.

Kama mnavyojua siku hizi bila connection kupata ajira/ kibarua inakuwa ngumu sana. Baada ya kumaliza chuo nimezunguka kwenye makampuni mbalimbali ya kutengeneza barabara civil construction companies lakini inabaki kuwa ahadi tu, utaacha copies za vyeti, cv's nk lakini kuitwa ni majaliwa.

Nimepita pia kwenye miradi mbalimbali ya ujenzi inayohusisha mitambo hiyo.

Naomba mwenye connection au njia yoyote ya kunifanikisha kwenye hitaji langu hili nitamshukuru sana. Naishi kurasini, Dar.Tusaidiane wandugu.

√niko tayari hata kujitolea kwa muda fulani wakiona nafaa basi watanichukua rasmini.

Shukrani sana!
 
Vyetu tupia sandukuni tu havina maana sana huku kitaa, beba leseni zungukia site. Pia usifika site ukawambia umetoka chuo ama ukaleta pigo za chuo maop wenzio wanaweza kukutenga.
 
peleka maombi yako katika camp za SGR fasta utapata km upo compitent.
Sgr nilishapeleka mkuu,,, tatizo kuitwa! Bila "connection" inakuwa ngumu, unasubiri sana kuitwa bila mafanikio! Nilipeleka kwa mkono na via e-mail pia.

Shukrani kwa ushauri.
 
Vyetu tupia sandukuni tu havina maana sana huku kitaa, beba leseni zungukia site. Pia usifika site ukawambia umetoka chuo ama ukaleta pigo za chuo maop wenzio wanaweza kukutenga.
Nikweli mkuu Patra31 usemacho ni hakika!

Kuna siku nilipeleka maombi kampuni mmoja ya kichina CRSG na kutoa vyeti vyangu, maoperator wengine wakashangaa! Mchina alinikubali sana sema mradi ulikuwa ndio umefika mwisho, akanipa namba yake nae akachukua yangu!

Nikweli sio vizuri sana kuonyesha vyeti ovyo ovyo bora kutembea na licence tu mpaka wahitaji vyeti. Uko sawa.
 
Vyetu tupia sandukuni tu havina maana sana huku kitaa, beba leseni zungukia site. Pia usifika site ukawambia umetoka chuo ama ukaleta pigo za chuo maop wenzio wanaweza kukutenga.
Hawawezi kumtenga sana wata mzarau tu maana inajulikana wanao toka veta wanakua hawana uzoefu kabisa,itabidi ajishushe awaombe msaada,ili kama kuna nafasi awe anaenda site kimya kimya kujifua zaidi,kwa maelezo yake inaonesha katoka chuo hajawahi kufanya kazi hata mwaka mmoja.
 
Kweli mkuu, shukrani kwa ushauri!
 
Back
Top Bottom