Mzee Mwanakijiji, niliwahi kusema mahali kwenye post fulani kuwa JK ni kiongozi dhaifu, he is weak at character and coward in making serious decisions. Niliposema haya, kuna members humu walinishukia kuwa natumia lugha isiyo ya kistaarabu ku address rais. Mimi nilisisitiza weakness is a state and a fact, ukishutumiwa kuwa dhaifu, unaweza kuprove wrong kwa kuonyesha makali in acting the otherwise kwa kufanya maamuzi magumu na kuwa mkali. Mimi nilimuelezea JK ni dhaifu na nikasisitiza udhaifu wake ni mpaka 'upstairs'!.
Kitendo cha CCM kujivua gamba, its just a game, Mukama, Chiligati na Nape, wanapiga tarumbeta. Jana nimemsikia Mukama akisema eti watawapa barua wajitoe wenyewe, wasipo jitoa, basi CCM itawafukuza!. Yoye haya yanatokea kwasababu top leader wao ni weak, simply dhaifu!.
Kwa vile hao ni watu wake, ametoka nao mbali, wamensaidia kufika hapo alipofika, anakunywa nao chai na wote ni wapenzi na washirika kwenye kale kamchezo ! (totos), kama angekuwa imara with strength of character, alitakiwa waite siku nyingi, awaambie, Rafiki zangu, mmenyooshewa vidole, japo hakuna uthibitisho wowote kuhusu tuhuma zenu, kitendo tuu cha kunyooshewa vidole, kinatosha. Nawaombeni tubaki marafiki, lakini kwenye uongozi wa chama, nawaombeni sana mnipishe, ili boti yetu isizame.
Kitendo cha kushindwa kufanya hivyo on time, kumeicost CCM kwenye uchaguzi uliopita, kwa kuogopa boti yao isizame kabisa 2015, sasa ndio wameibuka na hii falsafa ya kuvua gamba. Kama Mwenyekiti, alitakiwa kule kule ndani ya CC, awaulize Chenge na Rostam wawajibike kwa kunyooshewa tuu kidole, hivyo kukichavua chama, ameshindwa humo ndani ya vikao halali, anamsukumia Mukama, Chiligati na Nape ili kuonyesha yeye bado ni rafiki, ila mambo ya chama ni ya chama. Hayo alitakiwa afanya yeye kuwaambia marafiki zake.
Kwa vile NEC haikuweka bayani wanataka nini haswa kifanywe na viongozi wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wajiondoe kwenye uongozi, au wajiondoe ndani ya chama. Kjiondoa ndani ya uongozi wa chama, hili linawezekana kwa sababu wote waretain viti vyao vya ubunge na EL atawaendesha sana kupitia kofia yake ya M/K ya Mambo ya nje Ulinzi na Usalama, Mzee wa Vijisenti atamuendesha puta AG kilaza aione kazi yake ngumu, na RA ataendeleza ule ule utaratibu wake wa kupenyeza rupia kwa kuwatumia wabunge wanaondekeza njaa na wale walamba viatu, kuipa serikali wakati mgumu bungeni mpaka ijute kwa nini iliwaondoa kwenye uongozi wa chama.
Kama lengo ni kuwaondoa kabisa ndani ya chama, inamaana watapoteza ubunge wao na majimbo yao yatafanya uchaguzi mdogo. Kwa vile kwenye siasa, hakuna perment friends na permenent enemies, hawa jamaa watajinga Chadema na Chadema watawapokea kwa mikoni miwili na kuwasafisha, na hapa ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa CCM. Chadema wasipowapokea watajiunga hata TLP au vywama vyovyote vidogo. Kele kwao hawa ni muingu watu, wanapendwa kuliko, hata wakijiunga chama mfu, wote watayarejesha majimbo yao tena kwa ushindi wa kishindo.
EL atatoa siri ya kujiuzulu kwake uwaziri mkuu na kubainisha wazi ni kumkingia kifua JK who had a cut kwenye Richmond. RA atatoa siri ya fictitious names kwenye umiliki wa Dowans na matumizi ya El Adawi, kumbe mmoja wa wamiliki ni mwanafamilia wa magogoni!. Chenge ndie pekee hatatoa siri ya Rada maana SFO wanaweza kumshukia tena, kwani master mind ni marehemu (Balali) na among benefisharies ni watu wa magogoni wa wawakati ule.
Kusema ukweli hii ni sinema nzuri inayotaka kuanza, ndio maana nikashauri, Chadema, wajikalia tuu pembeni na pop corn zao, waki watch hii vita vya panzi, na baada ya hapo, ndipo waje na hiyo listi ya ziada ili CCM waendelee ku dance Chadema tune!.
Kwanza wote watapewa sala ya toba na kutoa ushuhuda role yao ilikuwa ni nini, pili wataiboa CCM up, down, left, right and centre