Mkuu Mkandara,
Ninakusoma sana na kukuelewa vyema na ninakubaliana na hoja zako. Mahali ambapo ninatofautiana na wewe ni sehemu moja tu, JK ndiye top wa CCM na ndiye mwenye final say kwenye maamuzi yaliyo mengi yawe ni ya CC au NEC. Mapungufu ya JK ni kwamba hana ujasiri wa kuwaweka kando hao jamaa zake. Ndiyo maana Lowassa alishasema kwamba urafiki wake na JK hawakukutana barabarani. Kilichopelekea mpaka JK kufika hapo alipo ni pressure kutoka ndani ya chama kwamba jamaa waondoke.
Nimejitahidi kufuatilia kwa ukaribu mjadala wa yaliyojiri kwenye CC na NEC, hakuna mahali JK alifungua mdomo kutaja mafisadi na ilihali anajua kila kitu kilichotokea. Cha maana alichosema ni kwamba watu wasimung'unye maneno, waseme kwa uwazi bila kuogopa. Hiyo ina maana kwamba alikuwa anakwepa lawama ili asije akaonekana ni mbaya. Swali langu ni hili: kwanini anawaogopa? Kama kweli yeye kashika mpini na ndiye Rais wa nchi kwanini awaogope?
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alishawahi kutamka wazi kwamba mafisadi inabidi serikali iende nao taratibu maana wana ukwasi mkubwa sana na kama wakiendewa kwa pupa nchi inaweza isitawalike. Maneno yanayofanana na hayo yalitamkwa na IGP. Sasa kama Waziri Mkuu na IGP wanawaogopa mafisadi, hao mafisadi wana nini haswa ambacho kinaitisha serikali?
Kwa hiyo pamoja na kwamba CCM ndio chama tawala na ndio kimeshika mpini, mwenyekiti wake hana ujasiri wa kuwatosa hao jamaa. Hivyo ninaungana na wale wanaosema jamaa wakomae ndani ya chama tuone watafanywa nini.
Lowassa na Rostam hawana incentive ya kutoka kwenye chama kwa kuwa kuwepo kwao ndani ya chama kunawahakikishia usalama wao na mali zao. Wakikubali kutoka sidhani kama wataendelea kuwa salama, na hawawezi kuwa nguvu ambazo wamekuwa nazo miaka yote ya utawala wa JK. Kinachonifurahisha ni kitendo cha Nape Nnauye kuendelea kuwasema, nasubiri mzee wa kususa (Lowassa) aje aseme amedhalilishwa sana kwenye majukwaa kwamba yeye ni fisadi.
Kinachoendelea ndani ya CCM ni mtaji kwa wapinzani na utakuwa mtaji mkubwa sana iwapo hao mafisadi watagoma kuondoka kwenye chama.