Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
inasikitisha kuona mambo ya msingi kama suala la radar raisi alilipuuzia.
na mwandishi wetu
23rd june 2011
b-pepe
chapa
maoni
mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru), dk. Edward hoseah
vijana wanaojiita wazalendo wa umoja wa vijana wa ccm (uvccm) wanaosoma katika chuo kikuu cha dar es salaam wamemuandikia barua mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru), dk. Edward hoseah, na kumpa siku 14 kuhakikisha watuhumiwa wa kashfa za ununuzi wa rada, richmond na kagoda agriculture limited wanafikishwa mahakamani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana sinza, jijini dar es salaam kwa niaba ya vijana hao, mjumbe wa mkutano mkuu wa uvccm mkoa wa dar es salaam, agustino matefu, alisema kuwa wameamua kumuandikia dk. Hoseah barua kwa kuwa wameona watuhumiwa hao hawajafikishwa mahakamani mpaka sasa.
Matefu alisema, katika barua waliyomwandikia mkurugenzi juni 21, juni mwaka huu, walimtaka amchukulie hatua waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya richmond, edward lowassa, na mbunge wa igunga, rostam aziz ambaye anahusishwa na dowans na kagoda.
Alisema kuwa yeye na vijana wenzake wazalendo wa uvccm, wanataka ufafanuzi pia kuhusu mbunge wa bariadi magharibi, andrew chenge, anayehusishwa na tuhuma za ununuzi wa rada ya kijeshi kwa bei kubwa kuliko thamani halisi na kuhoji kwa nini hajafikishwa mahakamani wakati takukuru ina taarifa zote.
"kwa nini hawa watuhumiwa hawafikishwi mahakamani, au takukuru inawaogopa?" sisi, kama vijana wazalendo wa uvccm tunampa mkurugenzi wa takukuru siku 14 za kushughulikia suala hilo na kuhakikisha kuwa watuhumiwa hao wanafikishwa mahakamani," alisema matefu akiwa ameongozana na mmoja wa wajumbe wa umoja wa wazalendo wa uvccm aliyetambulishwa kwa jina moja la lawrence.
Aliendelea kusema kuwa kama hatua hiyo haitakuwa imechukuliwa baada ya siku hizo, watafanya maandamano nchi nzima wao kama umoja wa vijana wazalendo wa uvccm kuwaambia watanzania kwamba naye (dk. Hoseah) anashirikiana na mafisadi kuwakandamiza watanzania.
"kama ofisi yako itashindwa kutekeleza jambo hili, tunafanya maandamano nchi nzima lengo kuu ni kuwaambia watanzania kuwa na wewe si mtu safi na unashirikiana na mafisadi na tutaishinikiza serikali iifute takukuru, " alisema matefu.
Aidha, matefu alisema kama takukuru itashindwa kutekeleza hayo baada ya siku 14 walizopewa maandamano yataazia chuo kikuu cha dar es salaam hadi ofisi za takukuru.
Nipashe ilipomtafuta dk. Hoseah kuthibitisha kama ameipata barua ya vijana hao, hakupatikana na katibu muhtasi wake alisema kuwa alikuwa nje ya ofisi. Hata alipotafutwa kwa simu yake ya kiganjani, ilikuwa imefungwa.
Kwa upande wake msemaji wa takukuru, doreen kapwaya, alikataa kuzungumzia suala hilo kwa maelezo kuwa hakuwa na taarifa kama dk. Hoseah amepata barua hiyo.
Kumekuwa na tuhuma dhidi ya viongozi hao watatu wakihusishwa na kupotea kwa umaarufu wa ccm, wakielezwa kuwa katika mabadiliko yaliyopewa jina la kujivua gamba wanatakiwa waache nafasi zao ndani ya chama. Wote ni wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa (nec) ya ccm.
Sababu kuu wanazotuhumiwa nazo ni kwamba wamekuwa na tuhuma za ufisadi, juu ya richmond, wizi wa fedha za akaunti ya madeni ya nje (epa) ndani ya benki kuu ya tanzania kupitia kampuni ya kagoda na rada ya bei mbaya.
Lowassa na chenge walijiuzulu nafasi zao serikalini kutokana na tuhuma hizo. Chenge alijiuzulu aprili mwaka 2008 kutokana na kashfa hiyo wakati huo akiwa waziri wa miundombinu (sasa ujenzi) baada ya kubainika kuwa na akaunti nene ughaibuni visiwa vya jersey. Alikuwa na akiba ya dola milioni moja, fedha zilizodaiwa kuwa huenda ni mgawo wa rushwa ya rada.
Alikana tuhuma hizo. Rostam amekuwa akihusishwa na kagoda ambayo ilichota sh. Bilioni 40 za epa lakini hadi leo wahusika wake hawajafikishwa mahakamani. Rostam naye amekana kuijua kagoda licha ya kutumia anuani ya kampuni yake.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa arusha, james ole millya, amesema hajamwomba radhi katibu wa ccm wa mkoa, mary chatanda, kwa kuwa hajapata taarifa rasmi ya kufanya hivyo.
Alisema taarifa za kutakiwa kumwomba radhi katibu huyo kwa madai ya kumtolea kauli za matusi, kashfa na lugha za udhalilishaji amezisoma kwenye vyombo vya habari.
"hayo nimeyasoma kwenye vyombo vya habari, lakini mpaka sasa sijapata barua rasmi inayonielekeza nifanye hivyo," alisema.
" lakini hata kama ningepata maelekezo ya kumuomba msamaha, hayupo hapa mkoani, yupo dodoma kwenye vikao vya bunge," alisema.
Chatanda ambaye ni mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa tanga, alithibitisha kuwa hajaombwa radhi na millya.
Alisema kuna njia mbili ambazo mtu anaweza kufanya ili kuomba radhi, moja ikiwa ni kuandika barua na nyingine kwenda kuonana naye uso kwa uso.
Katika kikao cha dharura cha halmashauri kuu ya ccm mkoa wa arusha, kilichofanyika juni 6, mwaka huu, kuzungumzia mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya siasa ya mkoa ya kuwavua uanachama wa ccm wanachama wanane akiwemo millya na mjumbe wa baraza kuu la uvccm, mrisho gambo, kwa madai ya kufanya maandamano haramu yaliyokuwa yakishinikiza kung'olewa kwa chatanda, kilimtaka millya kumwomba radhi chatanda.
" mimi niliondoka siku ya pili baada ya kikao kile, nipo dodoma…bado hajaomba radhi," alisema.
Aidha maamuzi ya kikao hicho, pia yalimtaka gambo kumwomba radhi aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la arusha mjini, dk batilda burian, kwa madai ya kumtolea matusi, kashfa na udhalilishaji wa kijinsia.
Akizungumza na nipashe kwa njia ya simu, gambo alisema kuwa yupo mjini dodoma kwa mambo ya kifamilia.
Alisema kuwa : "binafsi bado sijapata barua yoyote kuhusu maamuzi ya halmashauri kuu ya ccm mkoa, yanayomtaka kufanya hivyo…hayo maneno nayasoma tu kwenye magazeti, nikipata barua labda nitakuwa na cha kusema."
chanzo: Nipashe
Sasa hivi ndiyo serikali inajifanya inataka chenji ya rada wakati wa kesi walikuwa hawaonekani. Hivi kwa nini wabunge wa ccm + Cheyo nao wamejiingiza kwenye huu mkenge. Hivi ni hela za nani zimewapeleka huko uingereza wakati BAE ilishatoa tamko kuwa hizo hela tutazipata thru NGO. Nashindwa kuelewa kwa nini watanzania ni mbumbum hivi. Wanatafuta hizi hela wazichakachue tena. I am tired of illusions!LOwassa alishasema ikifika wakati akachoka na kelele zinazopigwa juu yake juu ya yeye kuitwa Fisadi, sasa atalazimika kusema hata yale ambayo alikuwa hataki kuyasema, mnataka kumuumbua mpaka Raisi wenu wa nchi sasa,
Sasa hivi ndiyo serikali inajifanya inataka chenji ya rada wakati wa kesi walikuwa hawaonekani. Hivi kwa nini wabunge wa ccm + Cheyo nao wamejiingiza kwenye huu mkenge. Hivi ni hela za nani zimewapeleka huko uingereza wakati BAE ilishatoa tamko kuwa hizo hela tutazipata thru NGO. Nashindwa kuelewa kwa nini watanzania ni mbumbum hivi. Wanatafuta hizi hela wazichakachue tena. I am tired of illusions!
Hao wamekosa cha kufanya, tokea lini mwizi akampeleka mwizi mwenzake Mahakamani huku wote ni wahusika na ushahidi upo, fanyeji mambo mengine tu UVCCM
LOwassa alishasema ikifika wakati akachoka na kelele zinazopigwa juu yake juu ya yeye kuitwa Fisadi, sasa atalazimika kusema hata yale ambayo alikuwa hataki kuyasema, mnataka kumuumbua mpaka Raisi wenu wa nchi sasa,
I hate to pat myself on the back. Hawa jamaa wamefuata ushauri vizuri. Na Rostam akafuata ushauri wangu vizuri. So... operation chaos is still on. The best thing fo EL na AC to do is to go back kwenye majimbo yao kufanya mikutano ya hadhara kuzungumzia mafanikio ya CCM as if nothing is going on..
I was looking for this one maana baada ya kusoma ile thread ya yaliyotokana na CC nikajikuta naikumbuka sana hii thread! Thanks.
yeah nilikusoma ikabidi niende kuitafuta. Ila CCM imejionesha kuwa iko dhaifu sana. Yaani, kama RA asingejiuzulu kwa ajili ya biashara zake wote wangekuwa bado wamo...
So.. stay put, enjoy your position, work like ever before and don't mind the new CCM leadership. They can't do a damn thing.
this is great!! maana vinginevyo wataonekana wanawaonea tu. Unless walete specific charges against them, la kusema kuwa waachie ngazi kwa maslahi ya chama haingii akilini.
Nona umeanza utani na wanyamwezi!!mimi simo!Wengine kizungu kimetupita, jee ndiyo unawatetea kwa kuwa hakuna ushahidi wa 'kinyamwezi'? - yaani kukamatwa na ngozi?