Open space Kibada,kigamboni imeuzwa kwa mtu binafsi??

mkazi

Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
24
Reaction score
10
habari zenu wakuu.

kwa wadau wa kigamboni,hasa wakazi wa maeneo ya Kibada karibu na FULL SHANGWE watakuwa wanafahamu kuhusu uwepo wa eneo kubwa la wazi pembeni ya FULL SHANGWE..eneo hili limekuwa likkitumika kama kiwanja cha michezo kwa muda mrefu sasa,siku za hivi karibuni kuna "fence" imewekwa maeneo ya kuzunguka eneo hilo na magoli yaliyokuwa yanatumia yameng'olewa.

  1. Je?kuna mtu amenunua eneo hili?
  2. Kama ni manispaa imeamua kuliendeleza kwa nini hakuna kibao cha kuonesha aina ya mradi unaoendelea?
  3. Kwa waliofuatilia video,na ramani za mjo mpya wa kigamboni,eneo hili limekuwa "earmarked" kama open space.kwa nini linawekwa fence?
nakiri kuwa sina taarifa za uhakika kuhusu eneo hili ,na kama ni manispaa imeamua kuliendeleza kwa kutengeneza bustani au kiwanja cha kisasa cha michezo ni jambo la kushukuru.lakini kwa nini hakuna kibao chochote kuonesha mradi unaoendelea eneo hili?kwa wale wenye taarifa zaidi si vibaya mkaweka wazi.

Watanzania tumekuwa wepesi kulalamika maeneo ya wazi yakiporwa lakini huwa hatutoi taarifa mapema uvamizi unapoanza,wakazi wa kibada naomba ufafanuzi wa hili.

nimeambatanisha na picha za eneo husika.kwa wenyeji wataweza kulitambua,hapa nimelipiga eneo kwa nyuma.
 
Attachments

  • IMG_20130824_141014.jpg
    IMG_20130824_141014.jpg
    85.5 KB · Views: 182
  • IMG_20130824_141017.jpg
    IMG_20130824_141017.jpg
    80.2 KB · Views: 157
Piga na kwa mbele babaangu mi sioni vizuri hapo...halafu usiogope sogeasogea karibu na kiwanja...
 
nilikuwa kwenye gari,na ndani ya eneo la uwanja kulikuwa na vijana wenye mashoka na vifaa vingine wakichimbua magoli ya mpira uwanjani hapo,sikutaka kuwaingilia,maana sikujua mood yao.leo nitajitahidi nipate picha za karibu.
 
Yuko majisifu mmoja ni memba humu labda atakuja kukujibu. Nikiikumbuka Dar ya miaka ya 80s na hii ya miaka 2000s ni kichefuchefu. Kwetu wapi pa kucheza haikuwa ishu hata kidogo. Leo hii watu wamevamia wamejenga, guest, makanisa, misikiti na magereji kendakenda. Ila ipo siku atakuja chizi wa ukweli atavunja kila kitu na aliyejenga kushtakiwa yeye mwanzo kabla hajaanza kushtaki
 
habari zenu wakuu.

kwa wadau wa kigamboni,hasa wakazi wa maeneo ya Kibada karibu na FULL SHANGWE watakuwa wanafahamu kuhusu uwepo wa eneo kubwa la wazi pembeni ya FULL SHANGWE..eneo hili limekuwa likkitumika kama kiwanja cha michezo kwa muda mrefu sasa,siku za hivi karibuni kuna "fence" imewekwa maeneo ya kuzunguka eneo hilo na magoli yaliyokuwa yanatumia yameng'olewa.

  1. Je?kuna mtu amenunua eneo hili?
  2. Kama ni manispaa imeamua kuliendeleza kwa nini hakuna kibao cha kuonesha aina ya mradi unaoendelea?
  3. Kwa waliofuatilia video,na ramani za mjo mpya wa kigamboni,eneo hili limekuwa "earmarked" kama open space.kwa nini linawekwa fence?
nakiri kuwa sina taarifa za uhakika kuhusu eneo hili ,na kama ni manispaa imeamua kuliendeleza kwa kutengeneza bustani au kiwanja cha kisasa cha michezo ni jambo la kushukuru.lakini kwa nini hakuna kibao chochote kuonesha mradi unaoendelea eneo hili?kwa wale wenye taarifa zaidi si vibaya mkaweka wazi.

Watanzania tumekuwa wepesi kulalamika maeneo ya wazi yakiporwa lakini huwa hatutoi taarifa mapema uvamizi unapoanza,wakazi wa kibada naomba ufafanuzi wa hili.

nimeambatanisha na picha za eneo husika.kwa wenyeji wataweza kulitambua,hapa nimelipiga eneo kwa nyuma.

peleka taarifa sehemu husika tuache tabia ya uwoga. Nenda serikali ya mitaa au halmashauri kahoji.
 
Ndugu si uoga,narudi nyumbani usiku kila siku.(wakazi wa KIGAMBONI wanaijua adha ya pantooni)weekend nikiwa nyumbani hizo ofisi huwa zimefungwa,pia natumia weekend kusalimia ndugu na jamaa.

nimeuliza humu ndani nikiwa na imani kuna wenye ufahamu juu ya kinachoendelea kwenye eneo husika
 
Back
Top Bottom