PutinV
JF-Expert Member
- Apr 17, 2017
- 1,046
- 1,651
Alijua kuwa ni kosa litakalo mgharimu maisha yake. Haijalishi kama kifo chake kitachelewa au kitawahi lakini kwa vyovyote vile Waisraeli wasingeweza kumuacha hai kwa kosa la kumwaga damu ya Kiyahudi.
Salam wakuu.
Sina uhakika kama kuna uzi kama huu au la lakini naomba ku-share na nyie moja kati ya operesheni za Mosad huko Dubai mwaka 2010
Mahmoud Abdel Rauf al-Mabhouh akiwa kama operative na chief logistic wa Hamas na operation zao huku akidili na mambo yahusianayo na silaha kutoka katika nchi mbali na kusaidia Iran na vikosi vyao vya Kikurd katika vita dhidi ya Israel.
Mwaka 1989 Mahmoud al-Mabhouh operative aliwaua askari wawili wa Israel ambao ni Avi Sasportas na Ilan Sa'adon wakati wa antifada ya kwanza.
Tangu siku hiyo Mahbouh amekuwa akiishi kwa tahadhari sana kwani alijua tangu siku hiyo yuko kwenye kill list ya moja ya mashirika hatari zaidi ya kijasusi ya dunia yaani Mosad.
Iliwachukua miaka takribani 20 kwa Israel kutekeleza lengo lao la kulipiza kisasi kwa mauaji ya askari wake wawili wa IDF.
JANUARI 18 2010 Jumatatu
Dubai inapokea zaidi ya wageni 100 000 kila siku wengi wakiwa ni watalii kutoka maeneo mbalimbali ya kaskazini mwa dunia. Watalii huwa wengi zaidi katika kipindi cha majira ya baridi ambapo watu wa maeneo hayo hukwepa baridi na kwenda Dubai kula bata kutokana na hali yake nzuri ya hewa, hoteli za kifahari na mals kubwa na za kisasa.
Lakini asubuhi ya tarehe 18 siku ya Jumatatu wanawasili watu 27 wakiwa wametoka katika nchi mbalimbali za Ulaya, Lakini watu hawa watatu hawajaja Dubai kula bata kama ilivyo ya wengi wanao wasili kutoka Ulaya bali wako Dubai kwa ajili ya operesheni maalumu ambayo baadaye ingeushtua ulimwengu.
12 kati ya hao walikuwa na paspoti za Uingereza, 6 zilikuwa paspoti za Ireland, nne za Ufaransa, nne za Australia na moja ya Ujerumani iliyokuwa na jina la Michael Bodenheimer kutoka mji wa Cologne.
Watu hawa 27 (Wakiwemo wanawake) walikua memba wa kikosi cha Mosad kilicho itwa Caesarea na baadhi yao haikuwa mara ya kwanza kufika Dubai.
Baadhi yao walienda Dubai March na Juni mwaka 2009 kwa ajili ya kuchunguza 'plasma screen', code au jina la siri walilo mpachika Mahbouh. Ilikuwa ni lazima kumchunguza Mahbouh kabla ya kufanya operesheni rasmi ili kuepusha kile kilicho tokea mwaka 1973 ambapo agent wa Mosad alimuua kimakosa raia wa Moroko huko Norway wakidhani ni memba wa kundi la kipalestina la PLO.
Pia Katika muda wote huo walio kuwa wametembelea Dubai walifanikiwa kuchunguza mifumo ya vitasa na milango katika hoteli mbalimbali za Dubai.
Hao hapo ni baadhi ya picha kutoka kwenye paspoti zao
Kwa mujibu wa taarifa za kijasusi, target yao ambayo ni Mahbouh angewasili siku inayo fuata baada ya tarehe 19 Januari yaani tarehe 20 kwa ajili ya deal fulani fulani zinazohusiana na masuala ya silaha.
Naendelea....
Sf
Sent from my iPhone using JamiiForums