Nimesikiliza redio muda fulani asubuhi na kujikuta nagadhibika ila sikufahamu ghadhabu yangu ii juu ya nini hasa! maana watangazaji walikua wanazungumza kwamba askari hao waliuawa kizembe...kweli nimeumia kidogo hasa ukizingatia trick waliyomwekea hawa mabwana! Well,Salimu alikua mtu makini na mtafiti kwa kile alichoamini...hakubweteka wakati akiwa dereva wa mkurugenzi wa makosa ya jinai na kuonesha uhakiki wa hilo aliamua kuchukua mafunzo ya awali idara ya upelelezi kwenye kitengo cha madawa ya kulevya!
Hakuishia hapo kwani alionesha ukomavu kabla hajahamishiwa kitengo maalumu cha kupambana na ujambazi kazi aliyoifanya hadi mauti yanamkuta saa 12 jioni tarehe 15/03/2011 katika kituo cha polisi Kabongwa! R.I.P bro! Safari yako imeisha kiume!