DOGO: Baba kwani mimi
nimetoka wapi?
BABA: Dah mwanangu
mbona unaniuliza swali
gumu hivyo? Nwei
hebu kaa hapo
nikuhadithie.
Mimi nilikutana na mama
yako siku moja wakati
anatoka kazini, tulikutana
kituo cha basi, mvua
kubwa ikaanza ikalazimika
tuchelewe sana
kupanda basi, hivyo
tukazoeana sana. Baada ya
kama miezi mitatu
tukaona ni vema tuoane,
tukawaeleza wazazi wetu
wakatukubali, harusi
ikafanyika, tena kubwa
sana, tukaanza kuishi
pamoja na kwa kifupi ndio
wewe ukapatikana.
Ukikua kidogo utanielewa
nina maana gani
DOGO: Haya, ila mwalimu
atanipiga
nisipomwambia kesho,
katuambia wote tuwaulize
wazazi wetu tumetoka
wapi. Mwalimu wetu
kasema
yeye ametoka Arusha