Najua wanajamvi wengi ninaowapenda watanila nyama kwa nitakachokisema hapa lakini kinatoka moyoni.
Kuna mpasuko mkubwa katika UKAWA, tupende au tusipende. CCM haina nguvu kubwa dhidi ya UKAWA bali UKAWA ina udhaifu mkubwa sana ndani yake. Natumai ninakosea katika dhana yangu hii lakini naomba unisikilize.
Kwa maoni yangu, udhaifu wa UKAWA ni:
Pengine ni mawazo yangu tu na kuwa kila kitu ni shwari na mwisho wa siku UKAWA watapeta, lakini natoa tahadhari hii:
WAZO GUMU NA LISILOFIKIRIKA
Kama inaashiria kuwa kampeni ya UKAWA inayumba kufikia uwezekano wa kushindwa uchaguzi, basi nashauri (mola wangu - nitatukanwa hapa) UKAWA wajitoe kwenye kinyang'anyiro hiki kwa sasa na ijipange vizuri kwa mwaka 2020. (sijui kama hii inaruhusiwa na NEC). Kitendo hiki ni kigumu bali ni cha kijasiri (na pengine ni cha kwanza katika tasnia ya siasa - sijui). Kitendo hiki kitaviletea vyama vya upinzani heshima kubwa sana na kuwapa jukwaa la kujinadi kuwa wana maono ya uongozi. Kusubiri ili kupania uongozi miaka mitano ijayo katika umri wa mama Tanzania si kitu kikubwa sana.
Najua wanachama wengi wa UKAWA wanataka CCM itoke tupate nguvu, uongozi, sera, muelekeo mpya. Watu wamechoka na CCM. Miaka zaidi ya 50 na bado watu wanasota. Lakini fikiria hivi: Kama UKAWA wakishindwa kipindi hiki basi inaweza kuchukua miaka mingi sana kabla upinzani hawajaweza kujipanga tena na mikakati mipya ya kuikabili CCM.
Hii inaitwa "food for thought" kwa viongozi wa UKAWA kutafakari. Wasaga lami watafuata tu maamuzi ya viongozi wa UKAWA. Kwa hiyo nyie wasaga lami wenzangu mnaweza kunitupia mawe tu nimekwisha jifunika zulia - sitadhurika.
Natumaini viongozi (UKAWA elites) watatafakari huu ushauri wangu. Sitegemei jibu lao.

- Mgawanyiko wa vyama vya upinzani ndani ya UKAWA (sina ushahidi) kuhusu wagombea wa uchaguzi huu.
- Udhaifu wa mvuto (kutokuwa na labwa jukwaani) wa mgombea uraisi wa UKAWA.
- Makundi ndani ya chama kikuu (CDM asilia, CDM maslahi) yaliojitokeza katika hii kampeni.
Pengine ni mawazo yangu tu na kuwa kila kitu ni shwari na mwisho wa siku UKAWA watapeta, lakini natoa tahadhari hii:
- Kama kuna uhakika wa ninacho kisema hapa - kuwa CCM watashinda - basi kuna hatari kubwa ya upinzani (vyama vinavyounda UKAWA) kufifia nuru yake na kutoweza kuikabili serikali inayofuatia kikamilifu. Mungu apishilie mbali. Vyama mahiri kama CDM vinaweza kuwa dhaifu hata kuliko vyama makinda kama ACT.
- Kama nadharia yangu ni potofu basi tuendelee. Natumai baada ya uchaguzi vyama vya UKAWA vitakabiliana na mgawanyo wa madaraka bila matatizo.