Onyo: UKAWA wajipime

Onyo: UKAWA wajipime

Hakuna safari isiyo na milima na mabonde, kusonga mbele ni lazima aiseee, kamanda mmoja akirudi nyuma haimaanishi wapambanaji wote warudi nyuma.

Hivi kwa nini watanzania tunakuwa na uoga wa tusichokijua? Acheni mambo haya tusonge mbele, lazima tuuonyeshe ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa imara bila CCM wala CHADEMA. Kapige kura kwa mgombea unayeona ni sahihi kwako.

Cc Kifyatu
 
Last edited by a moderator:

Nimependa sana your sense of optimism. Natumai uko sahihi.

Wasiwasi niliokuwa nao ni kuwa this time the stakes are too high. Kama UKAWA wakishinda basi chereko. Lakini UKAWA wakishindwa basi tutakuwa tumeua upinzani madhubuti kwa kipindi kirefu sana - I hope I am wrong.

Ninachozungumzia hapa ni opportunity cost ya kushindwa. Kama watu wanataka kucheza hii kamari, mimi ni nani kuwazuia.
 
Unakistahili ila umejisahau ukatuletea hadithi za shuleni hapa

Asante. Lakini kwa maoni yangu naona kama hukuzipenda hizi hadithi zangu. Nitajaribu vizuri siku nyingine.
 
we gamba hakuna kitu kama acheni kuweweseka .......mgogoro huo labda upo kichwani kwako

kichaaa wewe kwani mgogoro mbona hupo toka walipoungana kwani wewe haujui kwamba kuna mgogoro ukawa!??acha wamalize mgogoro then tu waje kwenye kampeni za 2020 mwaka huu wamefail...
 
Najua wanajamvi wengi ninaowapenda watanila nyama kwa nitakachokisema hapa lakini kinatoka moyoni.

Kuna mpasuko mkubwa katika UKAWA, tupende au tusipende. CCM haina nguvu kubwa dhidi ya UKAWA bali UKAWA ina udhaifu mkubwa sana ndani yake. Natumai ninakosea katika dhana yangu hii lakini naomba unisikilize.

Kwa maoni yangu, udhaifu wa UKAWA ni:
  1. Mgawanyiko wa vyama vya upinzani ndani ya UKAWA (sina ushahidi) kuhusu wagombea wa uchaguzi huu.
  2. Udhaifu wa mvuto (kutokuwa na labwa jukwaani) wa mgombea uraisi wa UKAWA.
  3. Makundi ndani ya chama kikuu (CDM asilia, CDM maslahi) yaliojitokeza katika hii kampeni.

Pengine ni mawazo yangu tu na kuwa kila kitu ni shwari na mwisho wa siku UKAWA watapeta, lakini natoa tahadhari hii:

  • Kama kuna uhakika wa ninacho kisema hapa - kuwa CCM watashinda - basi kuna hatari kubwa ya upinzani (vyama vinavyounda UKAWA) kufifia nuru yake na kutoweza kuikabili serikali inayofuatia kikamilifu. Mungu apishilie mbali. Vyama mahiri kama CDM vinaweza kuwa dhaifu hata kuliko vyama makinda kama ACT.

  • Kama nadharia yangu ni potofu basi tuendelee. Natumai baada ya uchaguzi vyama vya UKAWA vitakabiliana na mgawanyo wa madaraka bila matatizo.

WAZO GUMU NA LISILOFIKIRIKA
Kama inaashiria kuwa kampeni ya UKAWA inayumba kufikia uwezekano wa kushindwa uchaguzi, basi nashauri (mola wangu - nitatukanwa hapa) UKAWA wajitoe kwenye kinyang'anyiro hiki kwa sasa na ijipange vizuri kwa mwaka 2020. (sijui kama hii inaruhusiwa na NEC). Kitendo hiki ni kigumu bali ni cha kijasiri (na pengine ni cha kwanza katika tasnia ya siasa - sijui). Kitendo hiki kitaviletea vyama vya upinzani heshima kubwa sana na kuwapa jukwaa la kujinadi kuwa wana maono ya uongozi. Kusubiri ili kupania uongozi miaka mitano ijayo katika umri wa mama Tanzania si kitu kikubwa sana.

Najua wanachama wengi wa UKAWA wanataka CCM itoke tupate nguvu, uongozi, sera, muelekeo mpya. Watu wamechoka na CCM. Miaka zaidi ya 50 na bado watu wanasota. Lakini fikiria hivi: Kama UKAWA wakishindwa kipindi hiki basi inaweza kuchukua miaka mingi sana kabla upinzani hawajaweza kujipanga tena na mikakati mipya ya kuikabili CCM.

Hii inaitwa "food for thought" kwa viongozi wa UKAWA kutafakari. Wasaga lami watafuata tu maamuzi ya viongozi wa UKAWA. Kwa hiyo nyie wasaga lami wenzangu mnaweza kunitupia mawe tu nimekwisha jifunika zulia - sitadhurika.

Natumaini viongozi (UKAWA elites) watatafakari huu ushauri wangu. Sitegemei jibu lao.

Kuna kitu kimoja watu mnajisahaulisha kwa makusudi mnapochambua upinzani na uchaguzi. Kuwa zaidi ya nusu ya watakaopigia kura wapinzani watawapigia sio kwa sababu ya uimara au ubora wa wapinzani, bali kwa sababu ya chuki dhidi ya chama tawala. Kwamba hii ni sawa au sio sawa, nadhani sio dhima ya huu uzi. Lakini ukweli ndio huo.
Mfano dhahiri ni katika baadhi ya majimbo na kata ambazo wapinzani walishinda uchaguzi uliopita ambako hata mtoto mdogo alikuwa anaona kabisa mgombea wa CCM ni imara na madhubuti kuliko wa upinzani, lakini watu kwa sababu ya hasira dhidi ya chama tawala wakapigia upinzani.

Jambo la pili ni kuwa sitarajii hata miaka 100 ijayo kukaja kukatokea chama cha upinzani imara kuliko chama tawala hapa Tanzania, chini ya katiba na sheria ambazo zinatengeza mfumo tulio nao sasa. Mfumo unaokipa chama tawala madaraka juu ya dola, dola ambayo ina"regulate" mienendo ya siasa nchini.

Ndio watu wanasema (na sio utani) kuwa hata ukiweka mtu wa CCM na jiwe nitapigia jiwe. Na ni kuhakikishie watu wenye hasira dhidi ya CCM wameongezeka sana this time, na usishangae ni wengi kuliko wenye mahaba kwa CCM ukichanganya na walio neutral...

Tafakari tena...
 
Mzee wa mtazamo, itazame ni CCM au migogoro NI UKAWA tu. huna hoja kabisa. UKAWA NI watanzania wote, hata wewe NI UKAWA na tunaunganishwa na concept moja kubwa, ondoa CCM tuanze upya.
 
Yani wewe mkuu uko sahihi kabisa na hayo ndio matumaini ya waTanzania wengi kuwa CCM lazima itoke. Lazima CCM ifundishwe kuwa uongozi wa Tanzania sio amana yao tu. Mkuu wazungu wanasema "you are preaching to the choir" - huhitaji kunihubiria hicho kitu, nakijua fika.

Sababu ya kuleta huu uzi ni baada ya kuona kuyumba kwa kampeni ya UKAWA katika nafasi ya uraisi. Inawezekana ni hisia zangu tu na kwa hilo natoa samahani. Lakini swala linakuja kuwa kama kuna uwezekano wa UKAWA kushindwa basi tufanyeje? Hapo ndipo nilipopata kigugumizi na kutoa ushauri huu. Sio Shurti, viongozi wa UKAWA wanajua wanachofanya - mimi ni nani kwani?
 
Mkuu usitegemee kusikilizwa ukweli ni kuwa hao watanzania wengi waliochoka wanahitaji tu kupewa matumaini na Ukawa ku-destablize watampigia Magufuli. Usisahau Magufuli anaongea lugha aliyotumia Dr Slaa mwaka 2010 na basi Ukawa hawajashtuka. Safari hii CCM wanajua fika kuwa wako vulnerable hivyo wamejipanga sana kimkakati.
Ukawa hii ya sasa wanajilisha upepo tu!
 
Mzee wa mtazamo, itazame ni CCM au migogoro NI UKAWA tu. huna hoja kabisa. UKAWA NI watanzania wote, hata wewe NI UKAWA na tunaunganishwa na concept moja kubwa, ondoa CCM tuanze upya.

Matumaini yangu ni kuwa uko sahihi.
 
Tunaweza tukawa na upinzani hata kama ccm itashinda.tunaloaminishwa ni ukawa kwenda ikulu hii ndio hoja.lakini basi tutafakari huna madiwani huna wabunge serikali gani hiyo?suala ni ikulu kunani?tutafakari watanzania!!!!
 
Nimekupata mkuu.

Lakini IKULU - eeh. Labda kama bunge limesheheni wabunge wa UKAWA, bila ya hivyo turufu ya IKULU ni kubwa sana. Fikiria.
 
nijibu au nifafanue. huyu mchambuz anaufinyu wa uwono wake. asili ipi, mnyika,llisu, achana na slaa amejitoa. njoo kweny hiyo fikra dhaifu, cdm maslahi, je unamaanusha mboye,Lowasa.!! Mkuu usifanye analysis butu hivyo. Lowasa na wageni ni wanamanadiliko. ccm yangu awamu zake zoote. pangetosha. dira anatakiwa ionyeshe kufikiwa. ahadi zimetosha,

kilichopo Sasa ni haraka, mchaka mchaka. na ndio maana Unaonaje watanzania hawataki porojo, uadilifu, matusi, wizi, kuaminishwa binafs natak maisha mengine
 
Kama serikali za mitaa tu nyingi ni ccm hii ni ishara tosha madiwani watakuwa wengi hali kadhalika wabunge.sioni ni vipi waliyo wengi wakapigia ukawa kwa uraisi.linalokera hata ktk kampeni za ukawa hatusikii mkiwanadi madiwani na wabunge kikubwa ni ikulu ikulu msitufanye kuota ndoto za kufikirika
 
nijibu au nifafanue. huyu mchambuz anaufinyu wa uwono wake. asili ipi, mnyika,llisu, achana na slaa amejitoa. njoo kweny hiyo fikra dhaifu, cdm maslahi, je unamaanusha mboye,Lowasa.!! Mkuu usifanye analysis butu hivyo. Lowasa na wageni ni wanamanadiliko. ccm yangu awamu zake zoote. pangetosha. dira anatakiwa ionyeshe kufikiwa. ahadi zimetosha,

kilichopo Sasa ni haraka, mchaka mchaka. na ndio maana Unaonaje watanzania hawataki porojo, uadilifu, matusi, wizi, kuaminishwa binafs natak maisha mengine

Nimependa sana ujasiri wako wa kupinga fikra zangu finyu.

Napenda sana midahalo ya mada kama hizi bali nashindwa kulielewa swali lako. Mkuu, kwanza punguza jazba ili tuelewane. Pengine sote tuko kwenye timu moja.

Nikisema CDM asilia au CDM maslahi unayafahamu haya maneno au unajua maana yake? Labda tuanzie hapa. Sitaki kukukwaza kwa hiyo nitajieleza:

CDM asilia = wana CDM kabla ya UKAWA - Mbowe, Slaa, Lisu, Mnyika, Safari, Baregu, Sugu, Mdee, etc. (not in order of fame)

CDM maslahi = Lowasa (+CUF running-mate kutoka Zanzibar), Sumaye, Masha, Lembeli, + all other CCM implants.

Watu wanaona kuwa wana CDM-asilia waliowakoga watu wengi siku zote hizi hawahusishwi sana kwenye kampeni ya raisi kuliko wana CDM-maslahi - na swali ni kwa nini?

Kitu hiki kinaleta mpasuko ndani ya chama - au pengine sio kweli.

Kama hiki kitu hakikubugudhi basi yaishe, la sivyo soma bandiko langu la awali.
 
Yani wewe mkuu uko sahihi kabisa na hayo ndio matumaini ya waTanzania wengi kuwa CCM lazima itoke. Lazima CCM ifundishwe kuwa uongozi wa Tanzania sio amana yao tu. Mkuu wazungu wanasema "you are preaching to the choir" - huhitaji kunihubiria hicho kitu, nakijua fika.

Sababu ya kuleta huu uzi ni baada ya kuona kuyumba kwa kampeni ya UKAWA katika nafasi ya uraisi. Inawezekana ni hisia zangu tu na kwa hilo natoa samahani. Lakini swala linakuja kuwa kama kuna uwezekano wa UKAWA kushindwa basi tufanyeje? Hapo ndipo nilipopata kigugumizi na kutoa ushauri huu. Sio Shurti, viongozi wa UKAWA wanajua wanachofanya - mimi ni nani kwani?

Labda ni kitu gani kinachokufanya uone kuwa kampeni za uraisi za UKAWA zimeyumba?
 
Back
Top Bottom