Bora kuwa Mshamba kwa mambo mabaya

Bora kuwa Mshamba kwa mambo mabaya

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
1,733
“Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. ”
Rum 16:19 SUV

Tunaweza kufikiri ni sifa kujua kila kitu, wakati mwingine tunapenda kujifunza kwa watenda mabaya mbele za Mungu.

Tunaweza kuona ni njia sahihi, bila kujua ni njia inayotupeleka kumtenda Mungu dhambi, maana katika kujifunza kwetu tunaweza kuvutwa kutenda yasiyofaa mbele za Mungu.

Wakati mwingine tunaweza kuona kujua mabaya ni wajanja, na wengine hufika wakati wakathubutu kuyatenda mambo yasiyofaa.

Neno linatutaka kuwa wajinga katika mambo mabaya, bora kuonekana mshamba wa porini kuliko kuwa mjanja wa mjini uliyefarakana na Mungu wako au usiye na uhusiano mzuri na Mungu wako.

Mtu anayeonekana mshamba kwa mambo ya hovyo, hatupaswi kuwa na kejeli kwake na kumcheka au kumdhihaki, na hatupaswi kuwaona ni washamba.

Ushamba kwenye mambo mabaya ni bora sana, kuliko ujanja kwenye mambo machafu na yasiyopendeza Mungu wao.

Acha dunia ikupite pembeni kwa baadhi ya mambo yasiyofaa, yale yanayokufaa yafuatilie kwa uaminifu yakufikishe mahali unaenda.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Kuna watu humu kimsingi wanaonekana ni wanawake wanavyojifanya kushabikia USHOGA hawa unawaambiaje ?

Biblia ipo wazi kwenye hili, imekataza mwanaume kulala kingono na mwanaume mwenzie. Na mwanamke kulala kingono na mwanamke mwenzie.

“ ‘Usikutane kimwili na mwanaume vile mwanaume anavyokutana kimwili na mwanamke; hilo ni chukizo.”
Walawi 18:22 NEN

“ Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, WALA WALAWITI, wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyangʼanyi hawataurithi ufalme wa Mungu. ”
1 Wakorintho 6:9-10 NEN
 
Sawa,na Hawa wanaume wanajisifia kuzama chumvini je?
 
Back
Top Bottom