Labda nitumie nafasi hii hii pia kumpa pole mleta mada!
MOSI-@[URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=144417"]
Heinrich Himmler[/URL], nakubaliana na maoni ya huyu
Mzalendowetu niliyemnukuu. Service ni kitu cha msingi sana kabla hujaanza safari ndefu kama hiyo ya Songea-Dar. Hata kama gari ni jipya, usijipe uhakika wa 100% kwamba liko fit, lijaribu kabla hujalisafiria. Kulikagua usalama kwa fundi wa mtaani haigharimu hata 20,000/.
PILI-Kwa gari za automatic transmission kama ilivyo Noah, unapokuwa umepakia mzigo mzito ama abiria wengi na unashuka mlima kama Kitonga inatakiwa utumie gia
L pale kwenye gear lever ikisaidiana na breki.
L imewekwa kwa ajili ya kushukia milima mikali (wame lock
L kwenye gia namba 1) pale gari inapokuwa na mzigo. Kwa mantiki hiyo, hata kama breki zitafeli, gari haiwezi kwenda kwendo mkubwa kwa sababu imekuwa locked kwenye gia namba 1 ambayo ni nzito, itakusaidia hata 'kujibamiza' salama kwenye kingo. Unapopanda mlima ukiwa na mzigo unatumia gia na
2 iliyo kwenye hiyo lever.
Kama kuna maswali zaidi niulize, kwa kuwa nina Noah pia na hiyo njia uliyopita ndio njia yangu almost kila mwezi.