Onyo kwa mnaoendesha magari kupitia kitonga iringa

Onyo kwa mnaoendesha magari kupitia kitonga iringa

..mkuu JayK 2H inakazi gani..?
 
Last edited by a moderator:
Ahsanteni sana kwa darasa. Hapa nimejifunza mamb
o mengi
 
Kwa umbumbumbu wako na misifa uliyonayo unafikiri elimu inapatikana shule tu ... wewe ndo unatakiwa urudi shule! If u r coming from legally 'prevelage' family na si kile kizazi cha nyoka nenda katoe sadaka na umshukuru MUNGU coz gari si 'makalio' kwamba kila mtu analo na akaweza kujifunza na kujua kila kitu!!!!

......Hewala Mkuu...mimi mbumbumbu......

.....ni mbaya sana kuwa maskini na wakati huo huo ni mjinga......
 
Pole mkuu,mshukuru Mungu kwa kwenda upande wa pili wa hilo gems!!!!iyo ni mitaa yangu, na kula kidudio hspo Mwaisela taartibu.
 
Wiki iliyopita nilisafiri kwenda Songea na gari yangu aina ya noah kutokea DSM, nilivyokuwa narudi nikaona nisanye abiria wanichangie mafuta. Sasa nimetoka Songea mpaka Iringa bila matatizo yoyote na sikuona kama gari ina tatizo lolote. Nilipofika kwenye milima ya kitonga nikaanza kuteremka ghafla mbele yangu kukawa na roli linateremka taratibu, si nikaamua kuliovateki, katika kuliovateki lile roli nikawa nimeliacha gari langu limechanganya speed ili niliovateki roli. Hamadi namaliza kiliovateki kuna kona kali upande wangu mimi dereva, narudisha mguu kati kwenye breki hamna kitu yaani naipata kwa mbali sana, nikajaribi kulala nayo ikanishinda nikaenda kubamiza kwenye lile gema la mbele yangu “head-on”. Kioo cha mbele kikatuchanachana mimi na abiria aliekuwa aliekuwa mbele. Gari kwa mbele ikaharibika nyakanyaka mchuzi tu ukawa unamwagika chini umechanganyika maji ya rejeta, hydraulic na oil vikawa vinamwagika, Nilichofanya ni kuwarudishia abiria nauli zao na mimi kutafuta gari ya kuivuta kuja dar. Hapa nilipo nipo mwaisela nyuma ya key board.

USHAURI: Wengi hatuna kawaida ya kuangalia “break pads” za magari yetu kama hazijaisha. Ukiendesha gari hapa mjini inaweza isiwe ishu ila ukiamua kutoka nalo kwenda mikoani hebu jaribu kutazamabreak pads kama ni nzima. Gari ikiwa na break pads zilizolika sana inaweza ikawa inashika break ikiwa haina mzigo, ila ukiwa na mzigo au abiria halafu unateremka kwenye kilima kikali kama kitonga, hiyo ni time bomb.


Pole sana Mkuu, ajali ni ajali na sometimes haina kinga.
Lakini hapo kwenye bluu : Gari yako iko licenced kubeba abiria na ww mwenyewe unayo leseni ya kuendesha gari ya abiria?
 
Sijawahi kupita hapo kitonga napasikia tu,hamna sign ya kona kali kwani,maana kutokana na maelezo yako ni kama vile hukutarajia kukutana na kona kali!!
 
Pole mkuu kwa matatizo yaliyokujuta!!. Nakubaliana na ushauri wa wadau wote juu ya safe drivin na kukagua gari kabla ya safari ndefu au hata fupi.
Lakini Kilichotokea kwenye Gari lako mpaka kupelekea wewe upate ajali ni "brake system over heating" , ni moja ya sababu kubwa sana kwa ajali nyingi za malori ya mizigo. lakini hutokea mara chache kwa magari madogo.Efficiency ya brake hupungua kadiri joto linavyopanda na ikifika maximum heat tolerance brake hupotea ,Ugumu ni kwamba tatizo hili halijionyeshi mijini au kila mahali kwa kuwa pads hazijiexpose kwenye continous heat kwa muda mrefu .yaani zinatumika na kupata muda wa kupoa.
Brake system ku overheat husababishwa na 1: kuchoka kwa pads and brake liners au 2: exessive use of brake 3: kubeba mizigo mizito na 4: low quality spare parts hasa pads. EXCESSIVE USE OF BRAKE ndio tatizo kubwa sana kwa madereva wengi, ila Kwa bahati nzuri wengi huwa hawapiti sehemu ambazo brake tolerance inakuwa tested to the maximum. Kwa kuwa scenario hii ya brake system ku over heat, hujitokeza mara chache sana katika baadhi ya maeneo , madereva wengi wa mjini hawafahamu. Maeneo kama Kitonga ,wami ,mbalizi, likumbulu ,ihemi ,'uwanja wa ndege' kule kyela ni baadhi ya milima mirefu ambayo inafanana sana ajali zake . Chunguza ajali za maeneo hayo ni kwenye kona za mwisho au katikati ya mlima ,(mazingira ambayo brake inakuwa imetumika kwa muda mrefu)


Next time ukisafiri pamoja na kufanya service ya kutosha jaribu sana kuwa makini usiruhusu hali hiyo kujitokeza ,kama umebeba mizigo mizito jaribu kutumia gia kubwa unaposhuka na ukihisi brake pedal inakuwa' spongy' ni dalili kuwa pads zimeheat. Simama uruhusu zipoe brake itarudi kama kawaida.
N.B tatizo hili linaweza kutokea hata kama gari ni mpya!!
 
Pole sana ila pamoja na matatizo ya break Sio busara kupiga overtake Kama mbele huoni, Leo umepata majeraha Kesho tutakupoteza, utaiachia familia simanzi na mateso.
 
Ni kweli unapokuwa na mzigo na unapanda na kushuka ni vyema kutumia Gia kubwa Lakini alikuwa Ana overtake wakati anateremka! Ina maana aliongeza mwendo huwezi Tumia Gia kubwa kuongeza mwendo, kwa kifupi Sio busara kupiga overtake mlimani iwe kupanda au kushuka, maamuzi yoyote utakayofanya yanaweza kupelekea ajali.
 
...huwa nachapa lapa sana njia hizi lakini hii shule imeongeza kitu kwangu,pamoja kiongozi...

Sio siri nami shule imekolea maana nipo milimani na huwa situmii hizo gia dhidi ya kwenye tope tu.
 
Automatic Car Gear Selector
P=PARK - the gear selector should be in this position when the car is parked as it typically locks the transmission so that the car cannot move. In conjunction with this, the parking brake (hand brake) may also be applied. On most cars, the engine cannot be started unless the lever is in this (or 'N') position.

R=REVERSE - selecting this position allows the vehicle to be driven in the reverse (backwards) direction.

N=NEUTRAL - in this position, the engine is disconnected from the drive train (gears) and the vehicle will not be propelled in either direction when the gas (accelerator) pedal is pressed. The wheels are not locked and the vehicle will be able to roll downhill if the brake pedal is not pressed.

D=DRIVE - this is the position that is typically used when the vehicle is being driven. As the vehicle increases (or decreases) in speed, the automatic gear box will select the correct gear for both speed and road conditions.

2=GEAR 2 - typically, automatic gear boxes have 3 of 4 forward gears, so some vehicles may have both 2 and 3 marked on the hear selector. By using this position, the driver 'locks' the transmission in a lower gear so that the engine will run with increased revolutions. This is useful when rapid acceleration is desired. It should be noted that maintaining high revolutions in lower gears will increase the fuel consumption of the vehicle and also the stresses on the vehicle and passengers. It should therefore be used for short periods only.

L=LOW - (may be indicated by '1') this is the lowest gear (or 1st gear) available. This position is useful when the vehicle needs to negotiate difficult terrain (such as a steep incline with a poor surface). For downward slopes, the LOW gear provides additional braking through the engine.

OD=OVERDRIVE - for vehicles fitted with this option, an extra gear is provided that has a lower ratio than the normal top gear. The power output delivered by this gear is low in comparison to the normal gears and is used for high speed cruising (on interstates / motorways etc). Engine revolutions are reduced, as are noise levels. Fuel consumption is improved.

labda niongeze kidogo,usije ukakutana na BMW,AUDI,VOLVO,M. BENZ macho yakakutoka.....
baadhi ya gari hizi zina two options at the same time
1.automatic transmission ambayo inaweza kuwa
a.basic P R N D L(1,2)
b.more advanced P R N D 4 3 L(1,2)
-hizi gari zina 6-7 speed gearbox ambazo ukiweka D unapata zote....ukiweka 4 unapata gear 1,2,3,4 tu.......ukiweka 3 unapata 1,2,3.....na ukiweka L ambayo unaitumia kwenye milima/miteremko mikali au kuvuta gari ingine unapata gear kubwa 1,2.

2.automatic+semi-automatic(mistakenly called manual)-kama umeendesha hizi gari au kupata utaona pale pembeni ya maandishi P R N D 4 3 L kuna alama +/- juu kuna +(shift up),chini +(down shift)....ukisukuma gear lever upande wa +/- utaweza kuingiza gear na kutoa wewe mwenyewe kwa kusukuma gear lever up or down....i.e + or -(hamna clutch ndio maana inaitwa semi-auto)....nyingi zina protective sensor ukichelewa kuingiza gear itaingiza yenyewe kama auto

hizi gari hazina OD option, gearbox zake ni smart zinasense when u want to accelerate hardly just by the way u press the accelerator wanaita kick back effect....gear inajibadili automatically eg from 4 to 3



bmw_5_series_550i_sedan_2008_interior_gearshift.jpg
 
thanks for a life-saving reminder, especially for watu wa mjini.
 
Duuhh......Mkuu inabidi urudi
shule ya kuendesha gari......moja ya sababu kubwa ya ajali nyingi
barabarani ni watu kama aliyeleta mada na wewe ndugu yangu.......

Ni muhimu kuifahamu gari yako vyema....hilo ni jambo a msingi kabisa
tulilofundishwa hata kabla ya kuanza mafunzo ya kuendesha
gari.........naona siku hizi watu wakishajua kunyoosha usukani....na
kufahamu breki ziko wapi basi.......safari inaanza Dar-Songea.......hii
ni hatari sana....

Mleta mada pole aisee....

Mkuu unamkashifu Mwalimu wangu.....mliberali wewe....
 
Mleta mada, kuna uhusiano gani sasa kati ya kupitia kitonga na hiyo mechanical error ya break iliyotokea. Hapo tatizo ni kwako kutofanya service kwa kuangalia gari yote kabla ya safari ndefu. Badilisha heading hiyo.
Msamehe, ajali imemfanya ashindwe kupatta heading
 
Labda nitumie nafasi hii hii pia kumpa pole mleta mada!
MOSI-@[URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=144417"]Heinrich Himmler[/URL], nakubaliana na maoni ya huyu Mzalendowetu niliyemnukuu. Service ni kitu cha msingi sana kabla hujaanza safari ndefu kama hiyo ya Songea-Dar. Hata kama gari ni jipya, usijipe uhakika wa 100% kwamba liko fit, lijaribu kabla hujalisafiria. Kulikagua usalama kwa fundi wa mtaani haigharimu hata 20,000/.
PILI-Kwa gari za automatic transmission kama ilivyo Noah, unapokuwa umepakia mzigo mzito ama abiria wengi na unashuka mlima kama Kitonga inatakiwa utumie gia L pale kwenye gear lever ikisaidiana na breki. L imewekwa kwa ajili ya kushukia milima mikali (wame lock L kwenye gia namba 1) pale gari inapokuwa na mzigo. Kwa mantiki hiyo, hata kama breki zitafeli, gari haiwezi kwenda kwendo mkubwa kwa sababu imekuwa locked kwenye gia namba 1 ambayo ni nzito, itakusaidia hata 'kujibamiza' salama kwenye kingo. Unapopanda mlima ukiwa na mzigo unatumia gia na 2 iliyo kwenye hiyo lever.
Kama kuna maswali zaidi niulize, kwa kuwa nina Noah pia na hiyo njia uliyopita ndio njia yangu almost kila mwezi.

Mkuu tuko wengi tusiojua matumizi ya automatic transmitted gear system, mimi ni mmojawao. Utakuwa wa msaada sana ukitoa somo kamili kama vile L ni ya nini D2 inatumika lini nk
 
Last edited by a moderator:
Kwa maelezo yako, hamna dereva hapo, kuna muendesha gari anayeendesha tu kwa kuwa analo.
 
pole sana mkuu kwa kujiokoa wewe na abiria wako.

hongera kwa kutumia ujanja wa kubamiza gari ukutani, maana ungejichanganya kidogo oporomokee kule mtoni. tungeokoa matairi tu.

nimeshudia ajali nyingi kwenye ule mlima, muda mwingi kunakua na magari yaliyoharika au kupata ajali.!!!
 
Back
Top Bottom