Onyo kwa mnaoendesha magari kupitia kitonga iringa

Onyo kwa mnaoendesha magari kupitia kitonga iringa

Joined
May 20, 2013
Posts
71
Reaction score
151
Wiki iliyopita nilisafiri kwenda Songea na gari yangu aina ya noah kutokea DSM, nilivyokuwa narudi nikaona nisanye abiria wanichangie mafuta. Sasa nimetoka Songea mpaka Iringa bila matatizo yoyote na sikuona kama gari ina tatizo lolote. Nilipofika kwenye milima ya kitonga nikaanza kuteremka ghafla mbele yangu kukawa na roli linateremka taratibu, si nikaamua kuliovateki, katika kuliovateki lile roli nikawa nimeliacha gari langu limechanganya speed ili niliovateki roli. Hamadi namaliza kiliovateki kuna kona kali upande wangu mimi dereva, narudisha mguu kati kwenye breki hamna kitu yaani naipata kwa mbali sana, nikajaribi kulala nayo ikanishinda nikaenda kubamiza kwenye lile gema la mbele yangu “head-on”. Kioo cha mbele kikatuchanachana mimi na abiria aliekuwa aliekuwa mbele. Gari kwa mbele ikaharibika nyakanyaka mchuzi tu ukawa unamwagika chini umechanganyika maji ya rejeta, hydraulic na oil vikawa vinamwagika, Nilichofanya ni kuwarudishia abiria nauli zao na mimi kutafuta gari ya kuivuta kuja dar. Hapa nilipo nipo mwaisela nyuma ya key board.

USHAURI: Wengi hatuna kawaida ya kuangalia “break pads” za magari yetu kama hazijaisha. Ukiendesha gari hapa mjini inaweza isiwe ishu ila ukiamua kutoka nalo kwenda mikoani hebu jaribu kutazamabreak pads kama ni nzima. Gari ikiwa na break pads zilizolika sana inaweza ikawa inashika break ikiwa haina mzigo, ila ukiwa na mzigo au abiria halafu unateremka kwenye kilima kikali kama kitonga, hiyo ni time bomb.
 
Mleta mada, kuna uhusiano gani sasa kati ya kupitia kitonga na hiyo mechanical error ya break iliyotokea. Hapo tatizo ni kwako kutofanya service kwa kuangalia gari yote kabla ya safari ndefu. Badilisha heading hiyo.
 
Wiki iliyopita nilisafiri kwenda Songea na gari yangu aina ya noah kutokea DSM, nilivyokuwa narudi nikaona nisanye abiria wanichangie mafuta. Sasa nimetoka Songea mpaka Iringa bila matatizo yoyote na sikuona kama gari ina tatizo lolote. Nilipofika kwenye milima ya kitonga nikaanza kuteremka ghafla mbele yangu kukawa na roli linateremka taratibu, si nikaamua kuliovateki, katika kuliovateki lile roli nikawa nimeliacha gari langu limechanganya speed ili niliovateki roli. Hamadi namaliza kiliovateki kuna kona kali upande wangu mimi dereva, narudisha mguu kati kwenye breki hamna kitu yaani naipata kwa mbali sana, nikajaribi kulala nayo ikanishinda nikaenda kubamiza kwenye lile gema la mbele yangu "head-on". Kioo cha mbele kikatuchanachana mimi na abiria aliekuwa aliekuwa mbele. Gari kwa mbele ikaharibika nyakanyaka mchuzi tu ukawa unamwagika chini umechanganyika maji ya rejeta, hydraulic na oil vikawa vinamwagika, Nilichofanya ni kuwarudishia abiria nauli zao na mimi kutafuta gari ya kuivuta kuja dar. Hapa nilipo nipo mwaisela nyuma ya key board.

USHAURI: Wengi hatuna kawaida ya kuangalia "break pads" za magari yetu kama hazijaisha. Ukiendesha gari hapa mjini inaweza isiwe ishu ila ukiamua kutoka nalo kwenda mikoani hebu jaribu kutazamabreak pads kama ni nzima. Gari ikiwa na break pads zilizolika sana inaweza ikawa inashika break ikiwa haina mzigo, ila ukiwa na mzigo au abiria halafu unateremka kwenye kilima kikali kama kitonga, hiyo ni time bomb.

Nadhani suala la msingi ni kuwa "dereva makini", kuanzia kwenye kukagua gari lako kabla ya safari yoyote, mpaka kwenye kufuata sheria za barabarani, hapo wewe ulivayoleti vyote viwili!
Pole Mkkuu!
 
Mleta mada, kuna uhusiano gani sasa kati ya kupitia kitonga na hiyo mechanical error ya break iliyotokea. Hapo tatizo ni kwako kutofanya service kwa kuangalia gari yote kabla ya safari ndefu. Badilisha heading hiyo.

Labda nitumie nafasi hii hii pia kumpa pole mleta mada!
MOSI-@[URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=144417"]Heinrich Himmler[/URL], nakubaliana na maoni ya huyu Mzalendowetu niliyemnukuu. Service ni kitu cha msingi sana kabla hujaanza safari ndefu kama hiyo ya Songea-Dar. Hata kama gari ni jipya, usijipe uhakika wa 100% kwamba liko fit, lijaribu kabla hujalisafiria. Kulikagua usalama kwa fundi wa mtaani haigharimu hata 20,000/.
PILI-Kwa gari za automatic transmission kama ilivyo Noah, unapokuwa umepakia mzigo mzito ama abiria wengi na unashuka mlima kama Kitonga inatakiwa utumie gia L pale kwenye gear lever ikisaidiana na breki. L imewekwa kwa ajili ya kushukia milima mikali (wame lock L kwenye gia namba 1) pale gari inapokuwa na mzigo. Kwa mantiki hiyo, hata kama breki zitafeli, gari haiwezi kwenda kwendo mkubwa kwa sababu imekuwa locked kwenye gia namba 1 ambayo ni nzito, itakusaidia hata 'kujibamiza' salama kwenye kingo. Unapopanda mlima ukiwa na mzigo unatumia gia na 2 iliyo kwenye hiyo lever.
Kama kuna maswali zaidi niulize, kwa kuwa nina Noah pia na hiyo njia uliyopita ndio njia yangu almost kila mwezi.
 
Last edited by a moderator:
I think is the problems of the road,very sorry mr.
 
Nadhani ni makosa yako hasa mtoa mada. Kwanza inainekana haukuifanuia service gari, pili utaendeshaje kwa speed kiasi hicho hapo kitonga na konakona zote hizo?
 
Labda nitumie nafasi hii hii pia kumpa pole mleta mada!
MOSI-@[URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=144417"]Heinrich Himmler[/URL], nakubaliana na maoni ya huyu Mzalendowetu niliyemnukuu. Service ni kitu cha msingi sana kabla hujaanza safari ndefu kama hiyo ya Songea-Dar. Hata kama gari ni jipya, usijipe uhakika wa 100% kwamba liko fit, lijaribu kabla hujalisafiria. Kulikagua usalama kwa fundi wa mtaani haigharimu hata 20,000/.
PILI-Kwa gari za automatic transmission kama ilivyo Noah, unapokuwa umepakia mzigo mzito ama abiria wengi na unashuka mlima kama Kitonga inatakiwa utumie gia L pale kwenye gear lever ikisaidiana na breki. L imewekwa kwa ajili ya kushukia milima mikali (wame lock L kwenye gia namba 1) pale gari inapokuwa na mzigo. Kwa mantiki hiyo, hata kama breki zitafeli, gari haiwezi kwenda kwendo mkubwa kwa sababu imekuwa locked kwenye gia namba 1 ambayo ni nzito, itakusaidia hata 'kujibamiza' salama kwenye kingo. Unapopanda mlima ukiwa na mzigo unatumia gia na 2 iliyo kwenye hiyo lever.
Kama kuna maswali zaidi niulize, kwa kuwa nina Noah pia na hiyo njia uliyopita ndio njia yangu almost kila mwezi.

Mkuu umenena, hizo D 1 na 2 (L), madereva wengi wa auto wanaziona mapambo!
 
Idimi asante kwa elimu, hebu nisaidie hapa, binafsi ninapo endesha automatic car huwa natumia D peke yake na mara nyingi nimeona kubadilisha gia mara zote ni lazima usimame kwanza. Now, swali ni kutoka kwenye D kwenda kwenye L ama 2 ... je ni lazima usimame kwanza ndo ubadilishe then uendelee na safari ama unaweza kubadilisha ukiwa katika mwendo?????
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pole sana na tunashukuru kwa ushauri. Ni kweli brake pad ni vitu ambavyo tuna overlook sana haswa kama brake zinakamata bila kujua kama safari ni kwenye slope kali lazima zihakikiwe. Thank for advice
 
Jamani magari haya ni uchawi wa kizungu na walijitengenezea wenyewe, sasa nyie endeleeni kuchezacheza nayo...sisi Wamatumbi zetu nyungo na breki yake makalio
 
Ruti ndefu lazima ufanye service ya uhakika mkuu Pole sana Mungu akusaidie upone mapema
 
duh!!! pole sana kaka, kwa ulivo elezea inaonesha wewe ni mzoefu, hongera kwa hlo
 
Sio vizuri kuchekesha sehemu ya huzuni

Konnie, yani mimi natoa ushauri weye wanishutumu nachekesha...binafsi nimehuzunika sana kwa kuwa huwa naendesha gari na hapo Kitonga nimeshapapita mara nyingi tu!!!
Na kwa namna hiyo sehemu ilivyo, huyu ndugu anaonekana alikuwa makini mno kwa kuweza ku-control gari lake...maana upande wa pili wa barabara kuna korongo moja kubwa sana...
 
Toa namba yako ya tiGO tukutumie pesa ya pole na hongera kwa uzalendo wako!!!
 
Back
Top Bottom