Onyo: Dr. Magufuli asizomewe tena

Onyo: Dr. Magufuli asizomewe tena

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Tumechoshwa na vitendo vya kuzomewa kwa mgombea wetu. Kuanzia kule Mbeya na hata hapa Dar es Salaam,Dr. Magufuli amekuwa akizomewa na kuoneshwa wazi kuwa hatakiwi. Yeye hujikaza kisabuni tu. Hutetemeka lakini huimarika.

Amewakosea nini hadi mumzomee? Wana-Dar es Salaam hamna tabia hiyo. Mmekuwa watiifu kwa CCM kwa muda wote. Mmekuwa hata wavumilivu kuitwa wala-miguu ya kuku. Kiwewapata nini? Nani kawaondoa utii kwa CCM?

Mkimzomea tena Dr. Magufuli,nasi tutamzomea wenu hata kwa kuigiza kwenye giza. Mnapaswa kumshangilia Dr. Magufuli na kumpa kura zenu. Msimzomee na kumnyima kura tafadhari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mimi huwa nazomea kimoyo moyo hata picha zake ktk mabango mbalimbali jijini dar.
 
CCM siasa zetu za kistaarabu. UKAWA wanaendeshwa kwa viroba! Katika hali kama hiyo ni lazima watafanya hizo tabia za kuzomea.

Aidha, UKAWA waelewe kuwa, CCM ina wanachama na wapenzi wengi pia, hivi na sisi tukiamua kuanza hiyo tabia ya zomea zomea, mgombea wao Lowassa atapona kweli?

Rai yangu ni kwamba vijana waache kukubali kutumiwa na wanasiasa kwa kupewa viroba ili kukidhi matakwa yao ya kudhalilisha wagombea. Hii tabia sio nzuri na haikubaliki.
 
Hata haya ulioandika sio ya kistaarabu. Huwezi kutoa onyo. We nani katika siasa za hapa Tanzania?
 
Na mwanza Nyegezi stand kwenye mkutano wa wenje alizomewa.alikuwa anatoka sengerema
 
Kweli kuzomea na matusi zote sio tabia nzuri, hasira zetu tukazionyeshe kwenye sanduku la kura hapo jumapili
 
Mi natafuta opportunity ya kumzomea ni vile sijagongana nae tu. Lakini jpili ndio nitamzomea vizuri kwenye sanduku la kura.
 
napenda sana kuwashukuru wazazi wangu
kipindi kile wananikazania kuhusu elimu sikuwa ninaaelewa umuhimu wake
leo ndio ninaelewa kuwa shule ni kila kitu

wanaozomea ni mafala na malofa ... huwezi kuwa ukawa na akili nzuri na mwenye elimu yako ukakaa barabarani ukazomea unless hujaelimika ila tu umekaa tu muda mrefu darasani.....
 
Awe anatumia tu chopa ili moja kwa moja anatua katikati ya mkutano wake!

Sasa Bulembo awe anasema amefanya mikutano mikubwa mingapi, midogo mingapi na amezomewa mara ngapi!

Namshauri Lowassa kwa vile anakubalika ardhini na angani amalizie kwa kutumia barabara
 
CCM siasa zetu za kistaarabu. UKAWA wanaendeshwa kwa viroba! Katika hali kama hiyo ni lazima watafanya hizo tabia za kuzomea.

Aidha, UKAWA waelewe kuwa, CCM ina wanachama na wapenzi wengi pia, hivi na sisi tukiamua kuanza hiyo tabia ya zomea zomea, mgombea wao Lowassa atapona kweli?

Rai yangu ni kwamba vijana waache kukubali kutumiwa na wanasiasa kwa kupewa viroba ili kukidhi matakwa yao ya kudhalilisha wagombea. Hii tabia sio nzuri na haikubaliki.

Nguvu mnayo itumia kwenye uchaguzi huu, mnge kuwa mmewekeza kwenye maendeleo ya waTanzania, msinge hangaika kiasi hiki. Jezi za kijani manjano, magari ya washawasha, bendera na mabango, vijarida, radio na telivishen, wana,uziki ma na wasanii, misafara ya magari na watu, maFUSO kusombelea watu, posho za wapiga debe na wapambe, mengine jazia ...............................!!!!!!!!!!!!!!!

na bado mnazomewa mnasema ni VIROBA!!!??
 
Watoto WA shule wanafukuzwa wasipande daladala DSM inasikitisha sana Lisa ccm NA kodi ya dizel naomba lowasa angalia hilo
 
Back
Top Bottom