"ONLY ONE KING" the movie.

JOTO LA MOTO

JF-Expert Member
Apr 11, 2018
758
555
TITLE:ONLY ONE KING

MTUNZI:JOTO LA MOTO

SEHEMU YA KWANZA

NJE.IKULU YA MFALME MKUU-MCHANA
Jengo kubwa jeupe, ndani ya uzio wa ukuta na nyaya za senyenge nzito juu.
Kwenye eneo la kilomita za mraba kama elfu kumi hivi.
Nje kuzunguka jengo wanaonekana Askari kadhaa wakiwa wamevalia maalum huku wamesheheni silaha kubwa na ndogo.
NDANI.IKULU-MCHANA
Mondi, kijana mtanashati, 30, ameketi kwenye moja ya viti mbele ya meza kubwa iliyonakshiwa kwa vito vya dhahabu.
Mlango unafunguliwa, wanaingia Mfalme, bwana wa makamo, 65, na Ali, kijana, 32.”Unaweza kuketi” anasema Mfalme
Mfalme anamuelekeza Ali kwa mkono akionesha kwenye moja ya viti jirani na alipoketi Mondi.Ali anaketi.
Mfalme naye anaenda na kuketi kwenye kiti chake kikubwa kilichopo mbele ya meza ile akiwaangalia Mondi na Kiba.”Ahsanteni kwa kuja”.
Ali na Mondi wanaitikia kwa sauti ya chini huku wakisindikiza kwa kuitikia kwa vichwa.
MFALME
Nimekuwa nikisubiri sana wakati kama huu..
nyie ni Vijana wangu pendwa.
nawakubali sana na mnajua hilo.
Najua ni vigumu kwa Mafahali wawili kukaa zizi
moja..ndio maana nimewaandalia jambo.
Nataka nyie wote muwe Wafalme kwenye Himaya
hii..Mondi utakuwa Mfalme wa kanda ya
Kaskazini..Ali utakuwa Mfalme wa kanda ya
kusini.
Ali na Mondi wanabaki wanamuangalia Mfalme.
MFALME
Naona mmeshikwa na butwaa.
ALI
Umetushtukiza..
MONDI
Ni surprise..lakini umetupa heshima kubwa
sana Mkuu.
MFALME
Ndio..ni surprise..na kama hamtojali twendeni
kwenye hatua inayofuata.
Mfalme anainuka.
MFALME
Dakika moja.
Mfalme anaelekea upande wa nyuma wa ofisi, anafungua mlango na kutoka.
Ali na Mondi wamebaki, Ali anashusha pumzi.
ALI
Naona sasa umefurahi..
Mondi anageuka kumuangalia Ally.
ALI
Ila kukwambia ukweli..
there is only one King Bongo.
Mondi anabaki kimya anamuangalia Ali, kisha.
MONDI
Hebu nisaidie kitu..
ALI
Gani?
MONDI
Achana na Zary.
Ali anaguna kwa kushusha pumzi nyepesi.
ALI
Labda nife kwanza.
Mondi anabaki anamuangalia Ali, anashusha pumzi.
MONDI
Fanya uamuzi sahihi sasa..maana nikitumia nguvu
utaumia.
ALI
Nikimuacha ndio nitakuwa nimeshaumia.
Mondi anaachia kicheko chepesi.
MONDI
Sijawahi kupoteza vita Ali
ALI
Kwa hii umeshapoteza Bw Mondi.
MONDI
Una uhakika?.
ALI
Asilimia laki moja.
MONDI
Unataka tupinge?.
ALI
Ikibidi iwe hivyo?.
Ali anaweka mkono, Mondi anatoa mkono na kisha wanafanya ishara ya kupinga huku Mondi akikata.
Mlango unafunguka anakuja Mfalme akiwa amevalia mavazi maalumu ya kazi.
MFALME
Natumai mpo tayari.
ALI na MONDI
Tupo tayari Mkuu.
Mfalme anaenda hadi ulipo mlango mkuu na kuufungua.
MFALME
Tafadhali.
Huku akiwaashiria Ali na Mondi waongozane kutoka.
xxxxxx
NDANI.UKUMBINI-MCHANA
Ukumbi mdogo kukiwa na Watu kadhaa walioketi.
Mpiga ngoma kuu anapiga ngoma kwa mdundo mmoja na Watu wote waliopo ukumbuni wanasimama.
Wapiga tarumbeta wanaanza kupiga.
Mlango Mkuu unafunguka, wanakuja Mfalme, Ali na Mondi, wanaenda na kufika lilipo jukwaa dogo, wanapanda na kutulia.
MUONGOZAJI
Mheshimiwa Mfalme wa himaya hii ya Bongo..kwa
heshima na taadhima..tupo tayari kushuhudia
uapishwaji wa wasaidizi wako waliopo hapa
mbele yetu.
Kina Dada wawili waliovalia mavazi ya kiasili wanasogea wakiwa na nyungo zenye vitu kadhaa.
MFALME
kuanzia leo..kwa mamlaka niliyo
nayo..nakuapisha Bwana Mondi..kuwa Mfalme wa
kanda ya Kaskazini.
Mpiga ngoma anapiga midundo miwili ya nguvu, tarumbeta zinatumbuiza kwa muziki maalumu, Mfalme anapokea kofia yenye muundo wa kichwa cha Simba na kumvisha Mondi, anapokea kipande kikubwa cha ngozi ya Simba na kumvisha Mondi kutoka begani kwenda kiunoni akisaidiana na Msaidizi, anapokea Fimbo yenye kishikio cha dhahabu na kumkabidhi Mondi.
MFALME
Wewe sasa ni Mfalme wa Jimbo la Kaskazini.
Sauti ya Makofi kutoka kwa Waliohudhuria.
Mfalme anasogea upande wa Ali.
MFALME
kuanzia leo..kwa mamlaka niliyo
nayo..nakuapisha Bwana Ali..kuwa Mfalme wa
Jimbo la Kusini.
Mpigangoma anapiga midundo miwili ya nguvu, tarumbeta zinaanza kutumbuiza kwa muziki maalumu.
Mfalme anapokea kofia yenye muundo wa kichwa cha Simba na kumvisha Ali, anapokea kipande cha ngozi ya Simba na kumvisha Ali kuanzia begani kwenda kiunoni akisaidiana na Msaidizi, anapokea fimbo yenye kishikio cha dhahabu na kumkabidhi Ali.
Mfalme kwa bashasha anaenda na kusimama katikati ya Ali na Mondi.
Wimbo maalum unachezwa kwa tarumbeta na ngoma.
Wimbo unaisha, Mfalme anaachia tabasmu na kuinua mikono yake na kuiweka mabegabi mwa Ali na Mondi.
MFALME
Vijana wangu..najivunia kuwa na nyie kwenye
himaya hii..natumai sasa kila mmoja
ataangalia shughuli za jimbo lake bila
kuingilia shughuli za mwingine.
Wote wanapiga makofi.
MFALME
Kama hamtojali nikamilishe protokali ili
nikaendelee na majukumu mengine.
Mfalme, Ali na Mondi wanashuka kutoka jukwaani, wanaelekea mlango mkuu.
NJE.UWANJA WA IKULU-MCHANA
Mlango mkuu unafunguka, Mfalme , Ali na Mondi wanatoka.
inakuja Cadilac nyeusi na kusimama mbele, msaidizi anafungua mlango, Mfalme anashikana mkono na Mondi, Mondi anaingia Garini na Gari linaondoka.
Cadilac nyingine inakuja, Mfalme anashikana mkono na Ali, Ali anaingia Garini na Gari linaondoka.
Mfalme anaelekea mlango mkuu na kuingia.
NJE.BARABARANI-MCHANA
Cadilac inaenda.
NDANI.CADILAC
Mondi amekaa ametulia, Dereva anaangalia kioo cha kuangalia nyuma.
DEREVA
Naona hauko sawa boss.
MONDI
Hebu nipeleke ofisini.
DEREVA
Sawa boss
NJE.MAKAZI YA MONDI-MCHANA
Cadilac inafika, Mondi anateremka na kwa haraka anaelekea lango kuu na kuingia.
NDANI.MAKAZI YA MONDI-MCHANA
Zichu ameketi kwenye meza akitumia kompyuta ya mezani, Mondi anaingia akiwa mwenye haraka.
MONDI
Niitie Mr Poli.
ZICHU
Ok boss
NDANI.OFISINI KWA MONDI-MCHANA
Mlango unafunguka, anaingia Mondi, anaketi kwenye kiti, anafungua mkebe uliopo mezani, anatoa Cigar, anaweka mdomoni.
Anaingia Mzee Pol.
MONDI
Niandalie mpango kazi..nataka kumrudisha
Zari..subra yangu imeshafikia kikomo.
MEE POLI
Nahitaji milioni mia moja hamsini.
MONDI
Uwe na uhakika.
MZEE POL
Najua ninachokifanya Mr Mondi.
Mondi anabofya Simu ya mezani na kumpa Mzee Pol, Mzee pol anapokea.
MZEE POL
Milioni mia moja na nusu.
SAUTI YA ZICHU KWENYE SIMU
Ok Mzee Pol.
Mzee Pol anarudisha simu mezani.
MONDI
Nikupe muda gani
MZEE POL
Siku ishirini.
MONDI
Ok
Mzee Pol anaondoka, Mondi anaiwasha cigar, anainua miguu na kuweka juu ya meza akijizungusha kwenye kile kiti kikubwa.
MONDI
(mwenyewe)
Naingia namchukua Mtu wangu naondoka..no
fight no blood..kila Mtu anajua nani ni king.
Mondi anaachia tabasamu nyepesi na kupiga pafu ya cigar.
NJE.MAKAZI YA ALI-MCHANA
Nyumba ya ghorofa moja, ndani ya uzio wa ukuta na uzio wa umeme na ulinzi mkali getini.
NDANI.SEBULENI-MCHANA
Zary anamimina kinywaji kwenye glasi, mlangoni anakuja Ali akiwa kifua wazi na kaptula, anafika nyuma ya Zary.
ZARY
Mliongea nini?
ALI
Ya kiumeni.
ZARY
Hamkuongea kuhusu mimi?
ALI
Noo.
Kinapita kimya kifupi.
ALI
Bado hujamsahau.
ZARY
Unataka niseme ukweli?
ALI
Kama huo ukweli utaniudhi baki nao.
Zary akiwa na glasi yenye kinywaji anageuka na kumuangalia Ali.
ZARY
Sitaki kukuudhi Mume wangu.
Ali anaachia tabasamu.
ALI
Ana nini cha mno?
Zary anabonyeza kifuani kwa Ali.
ZARY
Six pack
Ali anabadili muonekano usoni na kumuangalia Zary kwa ukali.
ZARY
Umeniuliza.
ALI
Nimekwambia sitaki jibu la maudhi.
ZARY
Am sorry baby.
Wanabaki kimya kwa sekunde chache.
ALI
Hata useme nini lakini nitabaki kuwa King
of the jungle.
Ali anamsogelea na wanaanza kukiss mdomoni.
NJE.MAKAZI YA MONDI-MCHANA
Mondi na Mzee Pol wanatoka mlangoni, Mondi akiwa amevalia trak sutit nyeusi na Kikombe chekundu mkononi chenye kinywaji.
MZEE POL
Hatoki mara kwa mara..na akitoka anaongozana
na Jamaa..mara ya mwisho kuwa nje ya Kasri ni
alitokea Dubai…ana Wasaidizi tisa na Walinzi
binafsi Watano..ile Limo ni bullet proof.
Wanafika yalipo maboksi kadhaa jirani na geti, Ben anafungua moja ya boksi.
MONDI
Hizi ni nini?
Vinaonekana Vifaa mithili ya Drones.
MZEE POL
Zinatoka Israel..zinaruka hadi futi 800 juu
ya usawa wa bahari..zina uwezo wa kuendelea
kuleta taaarifa kwa saa 48 baadae hata kama
zitashambuliwa na kuteketezwa kabisa.
Huku Mondi akitikisa kichwa kuitikia maneno ya Mzee Pol.
Mzee Pol anainama na kuchukua boksi moja dogo, anatoa kitu mithili yam shale wa kuchezea darts.
MZEE POL
Hizi ni digital stings..zinakaa kwenye
drones..zikikosa target iliyokusudiwa
zinarudi zilipotoka.
MONDI
Yeye ana nini?
MZEE POL
Ana Russian Drones..zimeachwa sana na muda.
Mondi anatabasamu na kupiga funda kadhaa.
MZEE POL
Nadhani ulisema hukusudii kutumia nguvu
Mondi anamuangalia Mzee Pol.
MONDI
Relax Mzee.
Mondi anaendelea kupiga funda akiwa na tabasamu usoni.
NJE.KWA ALI GETINI-MCHANA.
Gari aina ya Subaru inakuja kwa kasi na kufunga breki mbele ya geti, kioo kinafunguka anaonekana Mocha, kijana, 24.
MOCHA
Fungua geti.
MLINZI
Shuka kwenye gari
MOCHA
Fungua geti acha use.. nina ishu ya muhimu.
MLINZI
Geti haifunguliwi Mzee wewe shuka.
Mocha anateremka.
MOCHA
Unajua nataka kumwambia nini Jamaa.
MLINZI
Ongea naye kwenye booth.
Huku Mlinzi akionesha kwa kidole chumba pembeni ya geti,Mocha anashusha pumzi.
MOCHA
K..m..ko
MLINZI
Shukran.
Mocha anaenda kwenye chumba kile.
NDANI YA BOOTH
Hoya Mzee nina ishu muhimu.
SAUTI YA ALI
Nakusikiliza
MOCHA
Siwezi kuongealea hapa Ali.
SAUTI YA ALI
Andika kama hautojali Mocha.
Mocha anashusha pumzi kisha anaanza kubofya vitufe vilivyo chini ya kompyuta ya ukutani.
NDANI.BAFUNI-MCHANA
Ali ameketi ndani ya jakuzi akiwa na I Pad na headphones masikioni.
MAANDISHI KWENYE KIOO CHA I PAD
Jamaa yako anaandaa jambo kule..hivyo kwa
ushauri wangu..
Ali anatabasamu.
ALI
(anamkatisha)
Sikia Mocha..saa kumi nitakuwa kwa Boza.
Ali anachukua Simu iliyo ukingoni mwa jacuzi na kuibofya, anaiweka sikioni, zinapita sekunde kadhaa.
SAUTI YA MONDI
Yes
ALI
Lini unakuja niandae mapokezi.
SAUTI YA MONDI KWENYE SIMU
Kiss my..a..s Ali
Simu inakatika, Ali anaachia kicheko kikubwa.
ALI
Kiss my a..s...nimeipenda hiyo
Anaingia Zary.
ZARY
Kuna nini?.
ALI
Hamna.
ZARY
Ulikuwa unaongea na nani?
ALI
Kuna mshamba mmoja hivi.
Zary anaketi kwenye ukingo wa jacuzi.
ZARY
Baby ulini promise hakutakuwa na shida
kati yenu.
ALI
Ya kiumeni acha yabaki kiumeni Zary.
Huku Ali akimvutia Zary ndani ya jacuzi.
Wanaanza kukiss.

..Itaendelea..
 
Back
Top Bottom