Online market kama kupatana.com; wengine ni matapeli

Godio

Member
Feb 12, 2017
51
38
Online markets kama Kupatana.com, zoomtanzania.com, jumia.co.tz, n.k. sio tu mitandao hii imeleta masoko ya bidhaa mbalimbali viganjani mwetu pia imesaidia kuokoa muda ambao ungetumika kufwata bidhaa hiyo. Pia inasaidi katika ulinganifu wa bei za bidhaa ili kujua 'market price' ya bidhaa husika.

Lakini kuna baadhi ya watu wanatumia mitandao hiyo kama njia yao ya utapeli. Hivi karibuni rafiki wa rafiki yangu ametapeliwa fedha na mtu anaejifanya muuzaji kutokea Iringa. Mtu huya anajulikana kwa jina moja la "Naseeb" kama alivyojilisti kwenye Kupatana.com. Alimwambia huyo rafiki wa rafiki yangu alipie 50% ya bei ya bidhaa ambayo ilikuwa ni 'LG SMART CURVED TV INCH 55 & LG HOME THEATER' alidai anaiuza kwa Tshs. 300,000/- na alimuakikishia kuisafirisha siku hiyohiyo. Baada ya malipo tu Jamaa akaiblock namba na akijua kapigiwa kwa namba nyingine anaiblock pia.

Ndio ivo pesa imeishatolewa na jamaa kaingia mitini na bado anaendelea kulisti bidhaa zake za uongo Kupatana tena anazilipia ziwe 'premium ads' (cheki picha).
IPHONE 6PLUS.jpg
LG.jpg
MAC BOOK.jpg
OKOA WENGINE WASITAPELIWE NA HUYU JAMAA - TENA USAWA HUU ULIVYO MGUMU NI SHIDA TUPU.
 
Never pay in advance(kama walivyo tahadharisha) kwa sababu haya masoko yetu bado ni machanga,hayana mfumo wa malipo ulio salama badala yake muuzaji/tapeli anaipokea moja kwa moja pesa yako.Mie huwa nikiona dili inaonekana ni nzuri sana muuzaji yupo mbali na eneo langu ninampa options mbili.Either autume kwa mtu/ndugu/rafiki yake aliye ktk eneo langu ili mimi nikaulipie pale au namuunganisha na mtu ninayemfahamu eneo alilopo na silipi hadi nihakikishe bidhaa ipo mkononi mwangu.
 
Huyu Jamaa yuko Iringa Ludewa... Alitaka kunitapeli, anadai anauza Mac book kwa 300k...

Nilipomwambia na Mimi nipo Iringa nakuja kuchukua mzigo, akaniambia wait ntakupigia...

Akawa kimya, nikamtafuta, akasema eti mzigo umeshauzwa... Hahahahaha...

Tapeli kumbee....
 
Huyo rafiki yako ni mjinga wa kutupwa na hafai kuishi katika sayari hii, yaani curved lg 55" na hometheatre yake kwa 300000? Hata wewe ulieleta huu uzi ni mpuuzi, mod ondoeni huu ujinga
 
Jamani muwage mnatumia akili kidogo kabla hamjanunua, hizo bei tu na brand za hivyo vitu mtu ungejua right away ni tapeli! Haziko hata nusu ya actual bei!
 
Polisi gani ahangaike na ujinga huo? Aah wap, yaani mzigo wa kuuzwa 4m wewe uambiwe utauziwa kwa 300k halafu uhangaishe watu? Nadhani akienda polisi ataekwa yeye ndani

iPhone 6plus kwa laki 3, MacBook laki 3 jamani doh!!! Mtu unashindwa kujiongeza ukajua ni utapeli huo?? Watu wengine sijui huwa wanawaza nini
 
Polisi gani ahangaike na ujinga huo? Aah wap, yaani mzigo wa kuuzwa 4m wewe uambiwe utauziwa kwa 300k halafu uhangaishe watu? Nadhani akienda polisi ataekwa yeye ndani
Hapa nazungumzia uhalifu,huu anaofanya huyu jamaa ni utapeli
 
Huyu jamaa Aliwahi kutaka kuniuzia computer akasema yupo ludewa nilivyomueleza nipo hapo hapo yupo sehemu gani niende nichukue mzigo akaniuliza kwa ukali wewe unaijua LUDEWA nikamjibu nimeishi hapa miaka mitatu sasa niambie ulipo nije au kama hutojali unaweza kunipitia hapa Central police station coz bado sijatoka kazini alichojibu ni tusi na kukata simu. kuanzia sikuhiyo namba yangu anayo hata nipige vipi hapokei. Nadhani kuna haja ya hawa kupatana waweke sehemu ya kuweka comment kwa wauzaji wa vitu kwenye mtandao wao iwe kama ku RE service za hawa watu nadhani kupitia hiyo tapeli utamjua kwenye
 
uyo jamaa nilishaga msanukia vitu kaweka bei chee balaa, nikaona uyu atakuwa tapeli, ukifungua tu app unakutana nae.
 
Huyo rafiki yako ni mjinga wa kutupwa na hafai kuishi katika sayari hii, yaani curved lg 55" na hometheatre yake kwa 300000? Hata wewe ulieleta huu uzi ni mpuuzi, mod ondoeni huu ujinga
Wewe utakuwa unamfahamu...naseeb...ama nawe unafanya dhuluma kama hizi; kwa nini unataka mod waondoe uzi wakati unasaidia kuelimisha uma aina ya utapeli ulipo!?
 
Mna pesa za mchezo acha awachangie wasio nazo.

Hongera kwa huyo tapeli.

Safi sana.
 
Back
Top Bottom