Online dating ya bongo na vituko na vitimbi tele

Online dating ya bongo na vituko na vitimbi tele

mlinzi mlalafofofo

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2008
Posts
762
Reaction score
1,400
1. Mtu ameweka picha kwenye page yake kumbe sio yeye bali ni picha ya rafikiake/mdogoake au nduguake gani sijui.

2. Mnakubaliana for a meeting, mwenzio anaanza kulia njaa mara anataka atumiwe pesa ya kula kwanza mara pesa ya nauli. Na ukituma pesa anazima simu au anakublock mazima!

Mdau karibu tuendelee kuweka masaibu yaliyokukuta kwenye hizi online dating platforms
 
Mwingine badala ya kuweka picha yake anaweka picha ya vitu anavyomiliki kama maua vikombe makabati mbwa au wine aliyokunywa jana.

mwingine anapiga picha miguu yake sijui kucha hlf ndo inakuwa picha yake ya profile😁

Mwingine kaweka profile vizuri na picha yake lakini ukiongea naye anakuambia "mi sipo hapa kwa mambo hayo". Yani ni full vituko.
 
Nitajie dating site zinazotumika Sana siku hiz
 
Nyie si mnajikuta kuendana na wakati. Mnatongozana kwenye hizo platform kujifanya wajanja wa mjini kumbe mnashindia mihogo maghetoni kwenu.
Na bado mtapigwa vizinga hadi mkome.

Fuata utaratibu maalumu uliowekwa wa kutafuta mchumba achana na hizi platform huko mnakutana na wadangaji
 
Back
Top Bottom