Onja video ya 3d kwenye screen ya computer yako

Onja video ya 3d kwenye screen ya computer yako

castongo

Member
Joined
Mar 16, 2008
Posts
57
Reaction score
74
KUHUSU 3D
Picha kwenye screen ya kawaida inaonekana flat, kwa vipimo viwili "2 dimensions", "2d". Picha ya 3d, mbali ya kuonekana kuwa na upana na urefu, inaonekana pia kuwa na kina, na ndio "dimension" au kipimo cha tatu. Mwonekano huo wa kina unaifanya picha ya 3d kuonekana kama inaendelea kuelekea ndani ya screen, na hivyo kukufanya uhisi unaangalia vitu halisi kama kwa kupitia dirisha. Wakati mwingine vitu vingine vinaonekana kama vipo nje ya screen.

PICHA YA 3D INA NINI
Kwa maelezo mafupi kabisa, picha hizo zina taswira mbili zinazo tofautiana kidogo, moja kwa kila jicho. Wazungu wamesema "stereoscopic". Unapotazama picha ya 3d unaona kama vile unatazama taswira moja, lakini kimsingi unatazama taswira mbili tofauti. Taswira inayoonekana na jicho la kushoto haionekani na jicho la kulia, na taswira inayoonekana na jicho la kulia haionekani na jicho la kushoto. Taswira hizo mbili zinachambuliwa kwenye ubongo na kukufanya uone taswira moja yenye kina.

MBINU MBALIMBALI
Ni vigumu kutofautisha taswira kwenye screen moja kwa kila jicho. Leo unapozungumzia 3d unaskia habari za video ya pekee, tv channel ya pekee, screen ya pekee, miwani ya pekee nk. Hata hivyo mbinu mbalimbali zimetumika nyakati tofautitofauti kulingana na maendeleo ya teknolojia ya wakati husika.
Mbinu ya kwanza wazungu waliita "Anaglyph". Hapo walicheza na tofauti ya rangi. Mara nyingi picha pamoja na kuwa na rangi nyingine, ilikua na rangi nyekundu na buluu kama picha hii.http://data:image/jpeg;base64,
maxresdefault.jpg

Na miwani iliyotumika ilikua na vioo vyenye rangi hizo mbili kama hii.
3d-stereo-anaglyph-glasses-18882358.jpg
Jicho lenye kioo rangi nyekundu lilishindwa sehemu za bluu, na lenye kioo cha bluu likawa kinyume chake na hivo taswira mbili zikawa zimetenganishwa. Tatizo ni kwamba rangi hizo zisingeweza kuonekana tena kwenye picha na kuifanya picha hiyo kuwa na mapungufu kidogo, lakini lengo la 3d lilifikiwa.
20-pcs-lot-Paper-3D-Glasses-font-b-Anaglyph-b-font-font-b-Red-b-font.jpg

Mbinu ya pili ilijulikana kama "Polarized". Hapa wazungu waligundua kuwa mionzi ya mwanga inaweza kuchujwa na kupewa mwelekeo mmoja. Wa wima, au wa mlalo, wa mzunguko wa saa au kinyume cha saa kwa kutumia vioo vya pekee vilivyo julikana kama "polarized glasses". Hapo projector mbili zenye vichujio tofauti vya mwanga zilirusha taswira mbili kwenye ubao mmoja. Mwanga huo ulichujwa baadae na miwani ya pekee aliyovaa mtazamaji yenye vichujio vya mwanga vilivyo wezesha kutofautisha taswira ya kila projector kwa kila jicho. Kwa mfano hapa jicho la kushoto liliona taswira ya projector ya kushoto na jicho la kulia liliona taswira ya projector ya kulia.
linear-polarized-3d-work.jpg

Video za namna hii zinatazamwa hadi leo kwenye kumbi za filamu za pekee, zilizo tengenezwa kwa njia hiyo. Hapa rangi zote zinaonekana na picha ni za kiwango kizuri sana.
Mbinu ya tatu inaitwa active shutter. Hii ni ya kisasa. Miwani yake inauzwa ghali, pengine inaanzia laki na kuendlea wakati miwani ya "polarizing" inaweza kuuzwa hadi elf tano. Miwani hiyo ya active shutter inakua na betri, na inafanya kazi kwa kufungua jicho moja na kufunga jingine kwa kupokezana kwa haraka sana kiasi kwamba aliyevaa hawezi kutambua. Hufanya hivyo kwa kupokea maelekezo kwa njia ya infrared kutoka kwenye screen ambayo nayo hubadilisha picha kwa kila jicho kwa haraka hiyo hiyo. Na hivyo hifikia lengo la taswira mbili, kila taswira kwa kila jicho.
activeshutte.png
Screen zinazotumika hapa ni za kisasa, zile zenye majina kama akina Samsung 3d na wazee wengine wenye majina. Hivo usinunue miwani ya plarized ukitaka unataka kuangali 3d kwenye madude hayo.
201504211844171302.jpg

Rangi zinakua nzuri sana, ila ukiangalia muda mrefu utahisi kichwa kinauma kidogo.
Leo utaskia pia watu wanaangalia picha za 3d kwa kutumia maboksi ya Virtual Reality, "VR"
models-vr-930x614.jpg

na Google cardboard vr.
fold1.jpg

Lakini kimsingi ndani pale picha inakua imegawanywa kwa kila jicho, na kuleta hisia ya kina, pamoja na upana na urefu na hivyo 3d.
Nimalizie hapa kwanza. Elewa kwanza hii nitakuletea maelezo jinsi ya kuchakachua 3d kwenye screen ya computer yako.
 
dah haya mambo siyaelewagi kabisa kuna app ya 3D kwenye pc ninayotumia hapa sema ndo sijui kuitumia inaitwa 3d builder
 
Article imeeleweka sana ebu tuletee ayo maufundi ya kuchakachua 3d kwenye pc
 
3D na VR ni vitu sawa in theory lakini tofauti sana, naongea hivi kwa sababu nimesha experience vyote viwili.. 3D kwenye Nintendo 3DS, kwenye simu moja ya LG, li TV likubwa la 3d la Samsung na kwenye Cinema Mlimani city as well VR kwa Gear Vr ya Samsung (bado sijagusa htc vive au oculus) .

Kwa kifupi in 3D unaona vitu vinakufuata nje mfano movie ya transformers utaona screw inakurukia au the hobbit utaona mshale unakufuata lakini wala sio unavyosema "unaona ndani" while in VR sasa ndio ina mimic reality/uhalisia (depth perception) mpaka inafika wakati ubongo unashindwa tofautisha cha kweli au uongo maana unaona digri zote 360 au 180 inategemea na kifaaa. Vr umeirahisisha sana kuna mambo mengi sana zaidi ya kushow two images per eye.

Vifaa vinauzwa Kwanzia 40,000(Bobo vr, vrbox) tafuta kimoja uone tofauti na pia uwe na pia device yako iwe ina ppi kubwa as well resolution kubwa uta
 
3D na VR ni vitu sawa in theory lakini tofauti sana, naongea hivi kwa sababu nimesha experience vyote viwili.. 3D kwenye Nintendo 3DS, kwenye simu moja ya LG, li TV likubwa la 3d la Samsung na kwenye Cinema Mlimani city as well VR kwa Gear Vr ya Samsung (bado sijagusa htc vive au oculus) .

Kwa kifupi in 3D unaona vitu vinakufuata nje mfano movie ya transformers utaona screw inakurukia au the hobbit utaona mshale unakufuata lakini wala sio unavyosema "unaona ndani" while in VR sasa ndio ina mimic reality/uhalisia (depth perception) mpaka inafika wakati ubongo unashindwa tofautisha cha kweli au uongo maana unaona digri zote 360 au 180 inategemea na kifaaa. Vr umeirahisisha sana kuna mambo mengi sana zaidi ya kushow two images per eye.

Vifaa vinauzwa Kwanzia 40,000(Bobo vr, vrbox) tafuta kimoja uone tofauti na pia uwe na pia device yako iwe ina ppi kubwa as well resolution kubwa uta

Ndio ni kweli kabisa unavyo sema. Nimegundua uwanja wa VR ni mkubwa zaidi. Pale wanakua wamechanganya vitu viwili. Cha kwanza kuna 3d ambayo ni makini zaidi maana taswira unazo tazama zinakua zimetenganishwa vizuri sana maana ni screen mbili kabisa. Na cha pili ni kwamba ni dynamic na iteractive, kwamba unapogeuza shingo na tswira inabadilika kulingana na uliko elekea. Hivyo inakupa ruhusa ya kutazama vitu vilivyo mbele yako na unaweza kugeuka mpaka kutazama nyuma, juu chini. Hiyo inakufanya upate hisia kuwa upo mahali pale unapo angalia. Unaweza kuvaa na kujiona upo juu ya mnara mrefu sana, ndani ya bahari, kwenye mji nk. Kwa mabox ya kawaida ya VR unatumia simu yako. Kwa mfano nilibahatika kupata google cardboard hilo ni rahisi sana kulinganisha na maboksi ya gharama kama hilo ulilosema la 40,000, kisha nikadownolad app ya cardboard ambayo inapatikana kwa android na Ios Cardboard - Android Apps on Google Play android.Hapo sasa unaweza hata kuangalia video za 360 kwenye youtube 360° Videos. Tatizo ni kwamba simu nyingine hasa hizi za akina tecno zinakosa "Gyro" au "Gyrometer au inclinometer" kwahiyo picha inakua haigeuki kulingana na unavyo geuza simu. Ukitaka kuchunguza kama smart simu yako ina gyro, fungua mojawapo ya video za 360 kwenye youtube kisha geuka na simu yako uone kama picha inasogea kama haigeuki ujue simu yako haina. Kabla ya kuiweka kwenye box iweke iwe full screen kisha gusa kialama cha cardboard
google-cardboard-icon-youtube.jpg

(kilichozungushiwa alama nyekundu) hapo video yako itagawanyika kwenye screen mbili weka kwenye box na vaa kitu. Agalia video kwa kugeuka geuka kutazama pande zote za video. Utahisi upo ndani yake.
Kwa mabox yale ya akina Oculus, Playstation Vr nk. ni kama ulivyo sema story ni tofauti. dpi ni kubwa na hivyo resolution tofauti na haya ya kuweka simu unaweza almost kuona pixels. Hayo madude yametengenezwa rasmi kwa ajili ya hiyo shughuli, yanarespond haraka kiasi kwamba unaona kama upo pale pale bila chenga.Watu wanatazama 360 still pictures, videos, games za hatari nk. Kwa mfano ukitazama experience ya oculus rift utagundua walio tengeneza hawana utani.
Kesho nitaandika ile mbinu ya kutazama straight kwenye screen ya computer.
 
Njia rahisi ya kuangalia na kupata kidogo vionjo vya 3d kwenye computer yakoni kwa kutumia Anaglyph, ile niliyo eleza hapo mwanzoni. Kama nilivyosema ni picha zinazo kuwa na rangi mbili. Inaweza kuwa nyekundu na buluu, au nyekundu na rangi nyingine inayoitwa cyan (ambayo ni katikati ya kijani na buluu). Katika kutazama video hizo (kuna still picture pia) lazima utumie miwani ya red blue, au red cyan kama katika maelezo ya awali. Nilishindwa kupata miwani ya namna hiyo hapa bongo, nikaona maelekezo mengi ya kutengeneza miwani ya namna hiyo online.

Nikajaribu kutumia marker pen, na miwani clear ya plastic niliyonunua kwa machinga. Matokeo yakawa kidogo sana maana sikupata marker nzuri, lakini kwa kiasi nikawa naona dimension ya tatu. Nikasoma pia maelekezo mengine ni kutafuta celopaper zenye rangi hizo, nikakosa, na muda haukuwepo sana lakini nilitamani sana kujaribu. Baadae katika kununua kitu online nikaona na miwani hii ikiwa inauzwa dolar moja point nikaijumlishia kwenye order.
http:// Amazon product ASIN B004HN2U7Wvideo za anaglyp 3d zipo nyingi tu youtube na still picture kibao kwenye net, ni wewe kusearch tu. Kwa mfano ya kujaribia miwani yako hii hapa.

Lakin video za "side by side 3d" ndio nyingi zaidi.

Sasa hizi zinatazamajwe kwa anaglyph glasses.
Unatumia player inayoitwa "VLC media" inafahamika sana, ni ya bure. Download toleo la kisasa zaidi. Hii ni kwa waheshimiwa wa windows, Mac na wengine sijajaribu. Ukishafungua VLC nenda kwenye "tools" kisha"effects and filters" kisha "Video effects" kisha "Advanced" utaona radio selecton ya "Anaglyph 3D" chagua hiyo.

Baada ya hapo fungua video ya youtube yenye side by side ndani ya VLC.
Ni kwa namna gani.
Kwanza unaweza kuidownload video hiyo na kuicheza moja kwa moja ndani ya VLC.
Lakini unaweza pia kucheza video bila kudownload.
Fanya hivi. Tafuta video kwenye youtube au pengine popote yenye side by side 3d. Rightclick juu ya video kisha click "copy video url". Sasa nenda kwenye vlc player yako click "Media" kisha "Open location from clipboard" kama una internet nzuri video itacheza moja kwa moja kwenye vlc yako toka youtube.
Vaa miwani yako ya red blue au red cyan. Enjoy.
 
Back
Top Bottom