Oni dogo kwa mitandao ya simu

Oni dogo kwa mitandao ya simu

Wanstechnical

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2014
Posts
266
Reaction score
225
Kwa wale wanaomiliki smart phone...nadhani suala la vifurushi sio geni, na nahisi huwa mnatamani zile sms kibao zinazotolewa kwenu zingebadilishwa na kuwa "data"kwa sababu hazina umuhimu manake kama ni meseji whatsapp ipo na inatosha.

Kwa upande wa pili kuna wale wenzangu na mimi ambao bado tunamiliki Nokia tochi kwetu data za mb ni kama uchawi tu maana hazitunufaishi na tunaomba kucha ili ziweze kuwa dakika za kuongelea.

Kwa msingi huu, hii mitandao kama Vodacom,tigo,airtel na mingine haioni umuhimu wa kuweka namna ambayo itamfanya kila mmiliki simu(aina yoyote) aweze kufurahia huduma zao?

Ni mtazamo tu👆
 
Wazo zuri sana mimi ni bora hata wanyime dk na sms ila wanipatie bundle la kutosha.
 
Back
Top Bottom