Hivi karibuni kumekuwapo na ongezeko kubwa la wataalamu wa uchambuzi wa mpira wa miguu, vituo vyote vya luninga na radio stations zina wachambuzi ukiwasikiliza wote ni wanaonyesha weledi wa hali ya juu ktk kuchambua soka la ndani na nje. Kwa maoni yangu hatua hiyo ni jambo zuri tu halina shida, lakini sasa swali ambalo nimekuwa nikijiuliza;
1. Kwa nini sasa hatuzalishi wachezaji bora wenye viwango kama Samatta? Au weledi wetu unaishia mdomoni tu? Nchi nzima tuna football academies zisizozidi 8, je academies hizi zinajikita kufundisha wachambuzi wa soka kuliko wachezaji?
2. Ningetamani sana kuona wataalamu wa vitendo (wachezaji) zaidi kuliko wataalamu wa kuchambua au kuwe na uwiano sawa, yaani wataalamu wa uchambuzi na wachezaji bora.