Ex Spy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2007
- 213
- 1,726
Hivi, tuna serikali ambayo ni responsive kwa wananchi kweli? Mbona dharau kwa wananchi zimezidi kiasi hiki? Ni uvunjifu wa Sheria ya Usalama Barabarani (2002), kifungu cha 19 B (1) na (2) na kifungu cha 54 (1), (2), (3), (4) na (5).
1) Nani ameruhusu watu hawa kujiwekea ving’ora au vimulimuli kihololela? Ilifuatwa sheria?
2) Tunajenga Taifa la aina gani kiasi kwa sasa unakutana hadi na IST ina vimulimuli?
Nilishangaa kukutana na DC aliyetemwa akiwa na gari la vimulimuli; nikajiuliza - kwani huyu bwana mdogo ni nani sasa?
Hayati Magufuli pamoja na udhaifu wake alikemea hili (angalau); sasa ‘wahuni’ wamerejea tena kazini na wanafanya hivi bila kukemewa wala Sheria kuchukua mkondo kwao.
Tujikumbushe:
a) Agosti 2019 - Jeshi la Polisi Latoa katazo Kwa Madereva Nchini
b) Julai 2020 - Polisi waagizwa kuwakamata wanaofunga ving’ora na vimulimuli kwenye magari
c) Hatua zikachukuliwa Dodoma: Polisi wanayashikilia magari 25 kukiuka amri ya IGP kwa kuyafunga magari yao ving’ora na taa kali
Sasa kwanini sasa imekuwa rahisi? Wanamwona Rais Samia kuwa dhaifu? IGP ni dhaifu kiasi hicho?