alexelias
JF-Expert Member
- Sep 1, 2017
- 2,032
- 3,198
Nipo Kahama hapa Mjini lakini ongezeko la Watu ndani ya Mji huo linatisha!
Nimekuwa nikitembelea Wilaya hiyo kila mara ajabu kila nijapo huwa nakuta ongezeko la Watu.Na hata sasa hali ni hiyo.
Nimejiridhisha pasi na shaka Mji huo unastahiki kabisa kuwa Manispaa lakini sielewi Mamlaka husika zinakwama wapi kuupandisha hadhi Mji huo.
Jambo la pili,ongezeko hilo la idadi ya Watu si dalili njema huko kwingineko hasa Vijiji na Miji baadhi jirani na Kahama.Kuna uwezekano hali ni ngumu huko watokako na hali hiyo huwapelekea hao Watu kukimbilia Kahama Mjini wakidhani hali pengine itakuwa nafuu hasa kiuchumi mara wafikapo ndani ya Mji ule.
Katika yote ni mda mwafaka sasa kwa Mamlaka husika kuupa hadhi ya kuwa Manispaa Mji huo wa Kahama kwani kwalo unastahiki.