One day sale: Uongo wa fastjet

One day sale: Uongo wa fastjet

Ngereja

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Posts
798
Reaction score
336
Tangazo liliwekwa kwenye website ya fastjet kwamba kutakuwa na promotion ya 24 hours kuanzia saa 2 asubuhi leo kwa safari zote za ndani kuwa $20 au Tsh. 32,000/= kwa safari za kuanzia tarehe 15-30/September 2014. Hadi muda huu ninapoandika hapa hicho kilichotangazwa hakijatokea. Online booking bado ina bei zilezile za kawaida, wakati huo kwenye website wanasema harakisha tiketi zinakatibia kuisha, lakini ukienda kufanya booking hukuti hiyo bei.

Nimeuliza kwenye ofisi zao hapa DSM kwa simu wanasema hata wao hawajui wamefichwa hawajui kinachoendelea. Huu ni utapeli na tabia hii inasababisha usumbufu kwa wasafiri. Mamlaka zinazohusika ziwachukulie hatua kali kwa kuwadanganya wateja.
 
Mimi nimefanya booking ya Mbeya nikakuta ni 45,000 One way tena ya mwisho wa mwezi huu. Halafu inabidi urudie rudie sana ili request yako iweze kwenda. Sijui mtandao wao una matatizo gani leo?
 
Me nimefanya booking ya Nov Mbeya Dar imekubali bila shida 45, 000. Ila for September inanipa 282,000/-
 
Utakuwa umechelewa, Leo asubuhi Dar-Mwanza nilikuta Tsh 63,000/= hivi, sasa wewe unataka ya Tsh 32,000 kweni Fastjet imekuwa Najmunisa au Zuberi?

Ila na wewe unajua kuwakomalia umewauliza mpaka ofisini kwao? wee inaelekea ni Mzaramo au ni Mngoni au Mgogo au basi tuamini kuwa wewe ni Mpare
 
Tangazo lilisema kuanzia saa mbili kamili asubuhi, na muda huo mimi nikawa tayari niko online, nimeamua leo kukaa ofisini ku-monitor hicho wanachoita 24 hour one day sale, na hadi muda huu hiyo bei sijaipata. Nilipopiga simu katika ofisi zao, mmoja wa customer service personel akaniambia bado makao makuu (London) hawajabadili kwenye system, nikapiga simu tena saa 6 nikaambiwa hata wao hawajui kinachoendelea, lakini watu wengi wamewapigia simu. Kumbuka promo ni kwa ticket za kuanzia tarehe 15-30 September. Hadi muda huu ninapopost hiyo bei haijatokea kwenye booking, ndio maana nasema wanatudanganya.
 
Wakuu kwa punguzo hilo kutakuwa na kugombania na tiketi zenyewe ni 1000 tu.Mimi nimewahi kwenye saa mbili na nusu nimeingia kwenye website yao kama walivyoelekeza na kukuta Dar-Mza 32000 plus kodi 45000 one way baadaye kidogo nikanunua tiketi ya pili kwa bei hiyo hiyo.ila naona wanapromote seat za laki mbili na zaidi hivi,ambayo inakuwezesha kufanya mabadiliko yoyote katika safari yako na kubeba mzigo mkubwa. kwa hiyo ni kweli ipo hiyo promotion kama itafika hadi kesho saa mbili hilo tena sijui.
 
Tangazo liliwekwa kwenye website ya fastjet kwamba kutakuwa na promotion ya 24 hours kuanzia saa 2 asubuhi leo kwa safari zote za ndani kuwa $20 au Tsh. 32,000/= kwa safari za kuanzia tarehe 15-30/September 2014. Hadi muda huu ninapoandika hapa hicho kilichotangazwa hakijatokea. Online booking bado ina bei zilezile za kawaida, wakati huo kwenye website wanasema harakisha tiketi zinakatibia kuisha, lakini ukienda kufanya booking hukuti hiyo bei.

Nimeuliza kwenye ofisi zao hapa DSM kwa simu wanasema hata wao hawajui wamefichwa hawajui kinachoendelea. Huu ni utapeli na tabia hii inasababisha usumbufu kwa wasafiri. Mamlaka zinazohusika ziwachukulie hatua kali kwa kuwadanganya wateja.

Mkuu unasema ukweli kabisa. Swali kubwa nikuwa mamlaka chini ya serikali ipi au sheria za nchi ipi ndugu yangu? Nafikiri utanielewa!! Hawa watu wanakuja kwenye shamba la bibi wanafanya wanavyotaka. Kwao walikotoka kufanya hivi hawawezi kwani ni adhabu kari kabisa. Nchi yangu Tanzania....................
 
terms and conditions apply: "Hurry while stock lasts"
 
Wakuu kwa punguzo hilo kutakuwa na kugombania na tiketi zenyewe ni 1000 tu.Mimi nimewahi kwenye saa mbili na nusu nimeingia kwenye website yao kama walivyoelekeza na kukuta Dar-Mza 32000 plus kodi 45000 one way baadaye kidogo nikanunua tiketi ya pili kwa bei hiyo hiyo.ila naona wanapromote seat za laki mbili na zaidi hivi,ambayo inakuwezesha kufanya mabadiliko yoyote katika safari yako na kubeba mzigo mkubwa.ee kwa hiyo ni kweli ipo hiyo promotion kama itafika hadi kesho saa mbili hilo tena sijui.

Acha uongo wewe!. Mza/ Dsm ilikuwa shs 88,000/ nimefanya ununuzi huo online saa mbili na robo asubuhi kwa trip ya tarehe 19 sept
 
Tangazo liliwekwa kwenye website ya fastjet kwamba kutakuwa na promotion ya 24 hours kuanzia saa 2 asubuhi leo kwa safari zote za ndani kuwa $20 au Tsh. 32,000/= kwa safari za kuanzia tarehe 15-30/September 2014. Hadi muda huu ninapoandika hapa hicho kilichotangazwa hakijatokea. Online booking bado ina bei zilezile za kawaida, wakati huo kwenye website wanasema harakisha tiketi zinakatibia kuisha, lakini ukienda kufanya booking hukuti hiyo bei.
Nimeuliza kwenye ofisi zao hapa DSM kwa simu wanasema hata wao hawajui wamefichwa hawajui kinachoendelea. Huu ni utapeli na tabia hii inasababisha usumbufu kwa wasafiri. Mamlaka zinazohusika ziwachukulie hatua kali kwa kuwadanganya wateja.

Pole sana ndugu yangu. Promotion ya fastjet siku zote huwa ni ya ukweli. Kama wewe hujabahatika, basi wenzio sisi tunafaidi fastjet. Ninawapongeza sana Fastjet na ninawapa BIg up!! Ni airline pekee ninayoiona ya uhakika kwa safari za ndani. Mimi nimefanya booking leo na zote nimepata punguzo.
1. Tarehe 22 Sept - KIA - DAR -shs 69,000/=
2. Tarehe 25 Sept DAR - KIA - shs 45,000/=,
3. Tarehe 26 Sept - KIA - DAR - shs 45,000/=,
4. Tarehe 7 Oct - DAR - KIA shs 45,000/=, na
5. Tarehe 12 Sept - KIA - DAR - shs 45,000/=.
Hebu niambie nime-save kiasi gani safari zote hizo ambazo zilikuwa ni lazima zifanyike kwenye familia yangu? FASTJET IDUMU DAIMA.
 
Mi leo mimekata return ticket ya kia tarehe 23 oct kwa shs 90 k
fastjet ipi unayozungumzia?
 
Nimekata pia 2nd October Mwanza Dar kwa 45000/=
 
Acha uongo wewe!. Mza/ Dsm ilikuwa shs 88,000/ nimefanya ununuzi huo online saa mbili na robo asubuhi kwa trip ya tarehe 19 sept

mkuu huo uongo unatoka wapi tena wakati mimi ndiye nilienunua hizi tiketi za promotion?,wewe yawezekana umepata bei ile ya 56000 ambayo ukiweka na kodi inakuja kwenye 83000,hiyo siyo bei ya promotion ambayo inaanzia 32000.Mkuu ukisikia promotion lazima uzichangamkie vinginevyo utasema ni uongo.kama uliangalia vizuri utakuwa uliona bei mbili,ambazo zote ni promotion, ya kwanza ni 32000 na ya pili ni 280000.
 
Mi leo mimekata return ticket ya kia tarehe 23 oct kwa shs 90 k
fastjet ipi unayozungumzia?

Hiyo ndiyo ya promotion ambayo mimi pia nimekata tiketi mbili asubuhi, ambayo mh.sana Ipogolo anadai hakuiona,naona wengi tu wamekata humu humu JF
 
Wakuu kwa punguzo hilo kutakuwa na kugombania na tiketi zenyewe ni 1000 tu.Mimi nimewahi kwenye saa mbili na nusu nimeingia kwenye website yao kama walivyoelekeza na kukuta Dar-Mza 32000 plus kodi 45000 one way baadaye kidogo nikanunua tiketi ya pili kwa bei hiyo hiyo.ila naona wanapromote seat za laki mbili na zaidi hivi,ambayo inakuwezesha kufanya mabadiliko yoyote katika safari yako na kubeba mzigo mkubwa. kwa hiyo ni kweli ipo hiyo promotion kama itafika hadi kesho saa mbili hilo tena sijui.

Laki mbili wanaruhusu mzigo mkubwa??
Jamani kama wewe safari zako hazieleweki kama mie fast jet haikufai.
Na kama mbeba mizigo kama mie utalia aiport.
 
Mimi nimepata ticket 3 kwa bei ya chini kabisa sh 45,000 each kwa ajili ya mke wangu na mdogo wangu Mwaza-Dar na Dar-Mbeya (return). ASANTE FASTJET nimenunua ticket za ndege kwa nauli sawa na ya Basi.
 
Utakuwa umechelewa, Leo asubuhi Dar-Mwanza nilikuta Tsh 63,000/= hivi, sasa wewe unataka ya Tsh 32,000 kweni Fastjet imekuwa Najmunisa au Zuberi?

Ila na wewe unajua kuwakomalia umewauliza mpaka ofisini kwao? wee inaelekea ni Mzaramo au ni Mngoni au Mgogo au basi tuamini kuwa wewe ni Mpare

Mxuuuu....!
 
Back
Top Bottom