Ondoa nta wa masikioni(earwax)kwa njia rahisi inayoitwa wax blockage.

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,022
1,305
Habari wadau wenzangu. Leo nazungumzia kuondoa earwax au nta wa masikioni.
Earwax kitaalam unaitwa CERUMEN. Unapozidi kiwango kinachotakiwa ndani ya mwili wa binadamu husababisha mtu kutosikia vizuri,kuwa kiziwi na pia husababisha kizunguzungu mara kwa mara. Tunauondoaje nta huu?:
Hapa utahitaji ear dropper na moja wapo kati ya hydrogen peroxide,mineral oil au glycerin. Chepesi kupatikana hapa ni glycerin na hiyo dropper. Mathalani chukua matone mawili(ya glycerin,mineral oil au hydrogen peroxide) kwa kutumia dropper uingize sikio la kwanza inama ili iingie halafu kuna nyingine ruhusu itoke. Hii ina maana kwamba ukiona imeingia nyingine inabaki unapoinama,kiwango halisi kimetosha(let the excess glycerine comes out). Ufanye hivyo na sikio lingine kwa siku mbili tatu hivi. Kisha uwe unatembea na pamba za masikioni maana glycerin inakuwa imekusanya nta na unatoka nje ya sikio mwingi sana hivi unautoa kwa urahisi.
Fanya hivi mara kadhaa ili kuondoa uziwi na kutosikia sawasawa na uondokane na kizunguzungu pia.
 
Asante sana kwa somo zuri, Nina tatizo la kumbukumbu je wawezakuwa na ufahamu jinsi ya kuongeza kumbukumbu? Thanks

Well, ingawa ni somo lingine ila nijaribu kukusaidia. Epuka pombe,sukari,msongo wa mawazo,chipsi za mitaani(wengi wanatumia mafuta ya transfoma kwani hayaishi) na jwisi za viwandani zenye kemikali. Tumia mkate wa brown,mchele wa brown,kunywa maji ya kutosha,pata muda wa kutosha kupumzika usiku. Pia kuna mmea unaitwa ginkgo biloba inasaidia damu kusambaa kwenye ubongo. Kausha mizizi yake,twanga,chekecha na uweke kwenye maji ya uvuguvugu unywe. Ila isiwe usiku kwani inasababisha kukojoa sana
 
asante, mm ndo nina kizunguzungu cha tangu utoto mpaka naona giza. niliwah kuanguka mara 2 yawezekana ni kwa sababu ya nta?
 
asante, mm ndo nina kizunguzungu cha tangu utoto mpaka naona giza. niliwah kuanguka mara 2 yawezekana ni kwa sababu ya nta?

Ndio. Kwa sababu mara nyingi nta unakusababishi imbalance(myumbiko wa mwili ambapo unaanza kuhisi maumivu katika paji la uso na giza la ghafla hutokea ndipo mtu anaanguka ghafla. Kwa muongozo zaidi wa mahitaji binafsi waweza ni pm ukiweka namba yako ya simu. Mungu ni mwema atatuwezesha
 
Back
Top Bottom