Ondoa macho na masikio kutoka nukta nyeusi katika maisha yako

ramadhani kimweri

Senior Member
Apr 22, 2016
181
179
NUKTA NYEUSI!!!

Siku moja professor wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi wake wajiandae na Test anayowapa muda huo huo.

Wanafunzi walisubiri kwa uoga mno hasa ukizingatia aliwaambia ghafla mno. Professor aliwagawia karatasi za maswali huku upande wa maandishi akiufunika chini na kuwatamkia kwamba yeyote asifunue karatasi mpaka atakapowaruhusu.

Baada ya kumaliza kuwagawia karatasi ya maswali kwa wote, professor akawaambia wafunue karatasi na kuanza kufanya mtihani.

Kwa mshangao, kila mtu akaona ya kwamba hakuna maswali yoyote katika ile karatasi, isipokuwa nukta kubwa nyeusi katikati ya karatasi.

Professor baada ya kuona mshangao kwa kila mwanafunzi, akawaambia hivi, "nataka kila mtu aandike kuhusu anachokiaona kwenye karatasi"

Wanafunzi wakachanganyikiwa, na kuanza kuandika vitu ambavyo hawajazoea.

Baada ya muda kwisha, Professor alichukua karatasi zote na akaanza kusoma majibu ya kila mmoja mbele ya darasa.

Wanafunzi wote walikuwa wameelezea ile nukta kubwa nyeusi, wakaelezea 'position' yake katikati ya karatasi, rangi ya ile nukta n.k.

Baada ya professor kumaliza kusoma majibu ya wanafunzi wote, darasa lilikaa kimya na Professor akaanza kuelezea.

"Sitaenda kuwapa marks kwenye hii Test, nilitaka niwape tu kitu cha kuwafikirisha. Hakuna hata mmoja aliyeandika na kuelezea kuhusu sehemu nyeupe ya karatasi. Kila mmoja wenu amelenga kwenye nukta kubwa nyeusi iliyokuwa katikati ya karatasi.

Hii inatokea katika maisha yetu ya kila siku. Tunasehemu nyeupe ndani ya maisha ya kufurahia lakini tumejikita katika nukta nyeusi. Maisha yetu ni zawadi tuliyopewa na mwenyezi Mungu iliyojaa upendo na kujaliana, tuna kila sababu ya kusheherekea asili hii inayojijenga kila leo. Marafiki tunaokutana kila siku, shughuli zinazotuingizia kipato, familia zetu pamoja na ndugu.

Hata hivyo tumejikita katika kutizama nukta nyeusi, mambo ya afya yanayotusumbua, kukosekana kwa pesa, mahusiano magumu, na kukatishwa tamaa na marafiki, mambo yote haya ni nukta nyeusi katika maisha yetu meupe.

Nukta nyeusi ni ndogo sana ukifananisha na kila kitu ambacho tumejaliwa nacho na Mwenyezi Mungu. Ila ndicho kitu kinachochafua akili zetu.

Ondoa macho na masikio kutoka nukta nyeusi katika maisha yako. Furahia kila Baraka uliyopewa na mwenyezi Mungu, furahia maisha na ishi maisha yaliyojaa Upendo."

13103476_755448937926062_3255095244860882754_n.jpg

Mkuu weka makala nyingi kama hizi, utasaidia wengi, kama kuna uwezekano huo.
 
NUKTA NYEUSI

Hakuna hata mmoja kati yetu anayeangalia sehemu nyeupe ya karatasi iliyopo katika maisha ya wengine. Utasikia huyo mzinzi, huyo mlevi, huyo mgomvi, huyo fisadi, huyo muongo !!!

Je ni kweli kuwa huyo ndugu, rafiki au jirani yako hana jambo jema alilofanya hata siku moja unaangalia nukta nyeusi tu ! Mkeo/mumeo je hana jema lolote zaidi ya nukta nyeusi? , hajawahi kutoa msaada kwa mtu? Hajawahi kuonesha upendo kwa yeyote? Hajawahi kuonesha huruma hata siku moja?

Hii inatokea katika maisha yetu ya kila siku. Tunasehemu nyeupe ndani ya maisha ya kufurahia lakini tumejikita katika nukta nyeusi. Maisha yetu ni zawadi tuliyopewa na mwenyezi Mungu iliyojaa upendo na kujaliana, tuna kila sababu ya kusheherekea asili hii inayojijenga kila leo. Marafiki tunaokutana kila siku, shughuli zinazotuingizia kipato, familia zetu pamoja na ndugu.

Hata hivyo tumejikita katika kutizama nukta nyeusi, mambo ya afya yanayotusumbua, kukosekana kwa pesa, mahusiano magumu, na kukatishwa tamaa na marafiki, mambo yote haya ni nukta nyeusi katika maisha yetu meupe.

Nukta nyeusi ni ndogo sana ukifananisha na kila kitu ambacho tumejaliwa nacho na Mwenyezi Mungu. Ila ndicho kitu kinachochafua akili zetu.

Ondoa macho na masikio kutoka nukta nyeusi katika maisha yako. Furahia kila Baraka uliyopewa na Mwenyezi Mungu, furahia maisha na ishi maisha yaliyojaa Upendo."
 
Mkuu wewe utakuwa unawasema ccm, ila sasa wakija hapa wataacha kujadili hiyo nukta nyeusi na karatasi jeupe wataanza kukutolea mapovu
 
Asante. Pumzi adimu ya u-great thinker hapa JF. Siku hizi post za kitoto zimejaa na mtu unapokumbana na topiki iliyoshiba kama hii una - appreciate. Asante tena na tena!
Bahati mbaya sana wachangiaji kiduchu ila ingekuwa ishu za ubuyu hapa mambo yangekuwa mengine kabisa..ishu zinazohusu maisha binafsi za watu umbea majungu na uongo
 
Back
Top Bottom