Hakuna jema machoni pa wabongo kijana amekwenda kutafuta angali bado ana nguvu anaonekena mbaya,tatizo la watu wanataka aishi maisha ya kuganga njaa wakutane nae mtaani wampige madongo na kumcheka, apewe sapoti jamani suala la yeye na Twanga kule hajafukuzwa ukifika wakati nao wakimlipa fedha anazohitaji bado atakwenda kufanya kazi kumbukeni anatumia nguvu zake mwenyewe. Mimi nadhani ni hatua nzuri katika kujitafutia maisha, na hakuondoka Twanga pepeta ili bendi iyumbe kaondoka kwenda kutafuta maslahi tu.
Mimi sijui analipwa kiasi gani huko aendako kwani ni mambo ya ndani zaidi ila kama kweli zitafika hizo laki nane ukijumlisha fedha zake zote kwa mwezi naomba nikujibu wewe unayesema Laki 8 ndogo kwamba unakosea sasa mshahara wa Laki 8 ni mkubwa ndugu yangu hebu kuwa mmkweli ni ma graduate wangapi wanapokea kiasi hicho kwa mwezi.
Mpeni nafasi kijana atafute.