Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Mwanakijiji, Rais kakujibu hoja, anawatuma mawaziri wakatembelee nchi wajionee kero za wananchi, another expense...
Kukopa per se siyo dhambi. Miaka ya 50 wamarekani walikopa sana kujenga mtandao wao wa barabara. Lakini inapendeza sana pale serikali inapopata mapato yake (hasa ya kujikimu), kupitia kodi.
Simaanishi kuwa sasa serikali iende ikaongeze kodi, kwani hiyo ni mbaya kama kukopa mabenki. Serikali inaweza ikaongeza kodi kwa kufanya yafuatayo;
1. Weka mazingira ya ku-attract FDI. FDI huwezesha miradi mikubwa ambayo uwezo wetu haufiki. Mfano, mtaji wa kujenga mgodi mmoja unaweza kufikia Dollar billionij moja. Utazitowa benki gani pesa kama hiyo hapa TZ?
Kwa muda mrefu sana TZ tumekuwa tukitoa picha ambayo haiko consistent. Tunaalika FDI, wakija tunawachenjia
2. Makali ya sheria ya TRA yapunguzwe. Uwezo wa TRA ku-block account ya kampuni hufanya wengi kuweka hela zao nje. Hizi hela zingekuwa hapa nchini, zingetumika katika uwekezaji
3. Serikali ipunguze matumizi. Iachane na magari ya kifahari na ipunguze ukubwa wake.
4. In the long term: serikali ifumue kabisa mfumo wa elimu. Ni bora turudi Cambridge system - hii ya sasa inazalisha nguvu kazi isiyo tayari kukabiliana na mfumo wa uchumi tandawazi (hawaajiriki, hawana uwezo wa kutunga sera zinazofaa, hawawezi ku-negotiate mikataba migumu, hawana uwezo wa kuendesha mashirika nk)