Nimemtumia PM mkuu, naamini akiingia atawasiliana nawe haraka tu
Sawa Mkuu ... tuko pamoja katika kustawisha demokrasia.
Nimemtumia PM mkuu, naamini akiingia atawasiliana nawe haraka tu
Lyatonga bwana . . .
Kalalamika kuwa watu wanadai kuwa yeye Mzee . . . kawatolea nje kuwa Bungeni hawaendi kubeba zege. Pia wanasema yeye mgonjwa . . mbona wengi tu wagonjwa . . . yeye yuko fit sana hata mke wake anajua . . . haaaa haaa
Inanikumbusha mambo ya Mzee Kenyattta . . . . Kwamba Muulizelini Mama Ngina . . . Ni nini ninamfanya usiku . . . .
Du! wagombea nao bwana . . .
Kwa haya machache niliyosoma hapa inaonyesha wazi viongozi nchini sii wazoefu kabisa wa Mdahalo. Hawa wote wanazungumza kama vile wao ni wagombea wa kiti cha Urais. Hakuna kati yao anayezungumzia matatizo ya watu na mazingira ktk jimbo lake na ku direct uwezo wake kuwakilisha wanajimbo badala yake zinazungumzwa sera za vyama vyao Kitaifa kama vile kila jimbo litapokea huduma sawa na matatizo yetu yanafanana.
Hii haiwezi kuwasaidia kabisa wananchi wa jimbo husika ikiwa mbunge anashindwa kuzungumzia kero za wananchi wake kuwa ndio sababu yake yeye kugombea. Kinachofanyika ni siasa tupu yaani wanashindwa kuzungumzia matatizo yanayowakabiri wana jimbo na kuna mipango gani ya kuwawezesha wao..