Ommy Dimpoz umeharibu wimbo wako kwa kutomuweka Christian Bella kwenye video

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
4,114
11,841
Huyu ndugu yetu Omary Nyembo baada ya kutoka katika 'UguaUgua' ya kansa ya koo hatimaye ameachia dude linaloitwa "Ni Wewe".

Ni wimbo mzuri, ameuimba kwa hisia na huzuni sana, ambapo kwa mtu mwenye machozi ya karibu kama ndugu yetu manengelo ni lazima alie pindi ausikiapo wimbo huo.

Katika wimbo huo, mwisho kabisa kule, inasikika sauti ya Christian Bella (Obama) mfalme kabisa huyu wa masauti. Ajabu katika video ya wimbo huo Bella HAJAONEKANA KABISA hata pua.

Sasa sijajua kama ni management ilikosa hela ya kumlipa Bella atokee kwenye Video au vipi!
Ila kwa ufupi video yako kaka Omary imeharibikia hapo.

Ila audio ni nzuri na ni bora sana.
 
Back
Top Bottom