Ombi/Wazo: Msaada kwa familia ya Mtoi

Ombi/Wazo: Msaada kwa familia ya Mtoi

Wazo la Tuko linatakiwa kufanyiwa kazi ipasavyo la sivyo litawakatisha tamaa kwa wanaokipigania chama na familia zao kiujumla kama Mh. Mtoi (Raha ya Milele umjalie eBwana na Nuru ya daima imuangaze, hastarehe kwa amani)
 
Naunga mkono hoja.

RIP Kamanda


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwa dhati kabisa,uongozi wa CDM toeni mwongozo.
 
Kwa maoni yangu naonelea mfuko huo uwe maalumu kwa wahanga wanaofariki katika harakati za ukombozi, na isiwe kwa mtu mmoja. Jana ilikuwa Mtoi, siku nyingine atakuwa kamanda mwingine ambaye familia yake itakuwa katika mazingira na mahitaji sawa na ya hayati Mtoi. Ni wazo langu tu.


Hili ni wazo bora kabisa.
 
Sisi huku shinyanga tulimpoteza kamanda wetu shelembi chama kikaahidi kumalizia nyumba yake na kusomesha watoto wake lakini hilo halijafanyika hata kidogo
 
hivi yule mjane wa mwangosi vipi,bado anasaidiwa na chama chenu? na pia vipi wale wajane wa jamaa waliouawa kule arusha bado chenu kinawakumbuka kwa chochote?
 
Ni jambo jema tushirikiane kwa majanga kama haya ili kuwaenzi wote wanaofia kwenye mapambano
 
Itapendeza baada ya mda na kupata maoni toka kwa wajumbe hapa jukwaani Moderator atusaidie kuwasiliana na wakina Makene ili tuelewe muafaka wake maana sio wapenzi wote wa mabadiliko ni wanachama wa hivi vyama...!

Upumzike kwa Amani ndugu na rafiki yangu Mohamed Mtoi.
 
Last edited by a moderator:
Dah maisha haya,, yaani Bosnia kaamua kumpiga SHAKIZI Mohamed Mtoi bila hata kujali kuwa ni kijana mdogo mwenye familia changa kisa maslahi ya ubunge

RIP Mohamed Mtoi
 
Naamini pia JamiiForums kwa nafasi yake wanaweza ku mobilize mfuko huu kwa member wake... at least kumchukulia kama distinguished member
 
Last edited by a moderator:
Wazo zuri sana.
Kulikuwa na Regia Mtema Foundation, ambayo nayo ilikuwa na lengo kama hili kwa kiasi kikubwa. Sijui iliishia wapi, au inaendeleaje?

Cc: Invisible Moderator
 
Last edited by a moderator:
Wazo lako ni zuli sana naliunga mkono asilimia mia! Ila tuwe makini na wakwale wakaiba hii aidea nzuri kabisa wakaenda kujikusanyia pesa kwa njia za panya! Wakajifanya wao ni wanandugu wenye uchungu na mpendwa wetu!
 
Mimi mwana CCM wa zamani na nimehamia upinzani, na siasa si uadui,lakini kwa kuguswa na msiba wa mwana JF mwenzangu tafuteni namba ya kuchangia nami nitatoa rambi rambi.RIP Mtoi.
 
Back
Top Bottom