Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,355
Ndugu wanaJF
Kama ilivyo kwa members wengine, jumuiya za wapenda demokrasia na wanachi wote kwa ujumla, mimi ni mojawapo ya walioguswa sana na kifo cha ghafla cha Ndugu Mohamed Mtoi.
Naguswa zaidi nikiangalia picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha Ndg Mtoi akiwa na familia yake, mke na watoto wawili wadogo.
Mtoi ametangulia mbele ya haki katikati ya harakati za kutetea maslahi ya watanzania WOTE kwa nafasi yake. Naamini vijana wengi wapo katika nafasi kama hizo kupitia vyama na forums tofauti, na ni matumaini yangu kuwa hawataogopa au kukatishwa tamaa na kifo cha kijana Mohamed Mtoi.
Najua kuna juhudi nyingi zimefanyika na zinaendelea kufanyika.
Sina uhakika kama wazo langu litaongeza chochote kwenye mipango na juhudi hizo, bali napenda kupendekeza yafuatayo
1. Chama cha Demokrasia na maendeleo, kiratibu zoezi la kushirikisha wanachama na wapenda maendeleo wote kutoa rambirambi, lakini zaidi ya rambirambi mchango utakaowezesha watoto wa Mtoi kupata huduma muhimu za elimu. Sijui economic background ya Mtoi, ndugu wala jamaa zake, lakini naamini kama Mtoi alivyolitolea kutuhudumia kupitia CHADEMA, ni jambo la heri na sisi tukichangia chochote kuiwezesha familia yake.
2. Naomba chama kifungue mfuko maalumu wa elimu ya watoto wa Mtoi, na authorized personnel wa chama kupitia verified IDs watupe maelekezo na kuhamasisha kupitia mitandao ya kijamii jinsi tunavyoweza kutoa michango yetu kwenye mfuko huo
3. Katika kufanikisha hilo, naomba wahusika wafungue uzi maalumu hapa JF utakaotuongoza namna ya kufanya, lakini pia wafungue akaunti maalumu Facebook (ambako Mtoi alikuwa active), itakayotambulika na kutangazwa hapa na kwingine, kwa maudhui yale yale ya kuelekeza na kuhamasisha wadau kuchangia mfuko wa elimu ya watoto wa Mtoi.
Nitangulize samahani kama kwa namna moja au nyingine pendekezo hili litamkera yeyote, na nikaribishe mawazo zaidi kuboresha wazo hili
Asanteni