Uchaguzi 2020 Ombi: NEC iwapime akili wagombea ubunge wa upinzani kabla haijawapitisha ili kupunguza chaguzi ndogo baadae!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Kiukweli katika mabunge yote kuanzia lile la Sapi hili la Ndugai ndio limetutia hasara sana kama taifa.

Pamekuwepo na utitiri wa chaguzi amnazo tulirudia kuchagua wabunge wale wale tuliowachagua 2015.

Kama taifa tumeingia hasara japo husemwa Demokrasia ina gharama zake lakini siyo kama hizi za kumchagua Mwita Waitara mara mbili na shukrani yake imekuwa kulitelekeza jimbo.

Chonde chonde Tume ya Uchaguzi wekeni utaratibu wa kuwapima akili wagombea ubunge wa upinzani.
Wagombea wa CCM kwa kiasi fulani wanajitambua, wakijiuzulu wanachapa rapa hawalambi matapishi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ccm mna kazi sana..... Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.....Babu yangu alinifundisha hivyo.
 
Kanuni zaidi zinahitajika ili mbunge akijiuzulu apoteze sifa ya kugombea nafasi hiyo milele.

Mtu anaweza kufaulu vipimo kabla ya uchaguzi halafu kichaa akakipata akiwa ofisini.

Ni fedheha kwa vyama hivyo kuwa na watu wanaochuuzwa kama mumi au kamongo.
 
Kama tokea tupate uhuru, 1961 mpaka 2015/October hayajawahi kutokea haya tunayoyashuhudia ya kupotea watu/kununuli watu na kuhama vyama kwa wingi hivi/kuuawa watu/kubambikiwa kesi/ kuokota maiti kibao coco beach/ etc etc, hakika kuna haja ya ku hold this regime accountable baada ya kuwapima akili kama haya waliyafanya wakiwa na akili timam. Na je kama wanagombea 2020, ni wazima kushika madaraka!
 
Kanuni zaidi zinahitajika ili mbunge akijiuzulu apoteze sifa ya kugombea nafasi hiyo milele.

Mtu anaweza kufaulu vipimo kabla ya uchaguzi halafu kichaa akakipata akiwa ofisini.

Ni fedheha kwa vyama hivyo kuwa na watu wanaochuuzwa kama mumi au kamongo.
Nimekuelewa bwashee!

Mtu kama Mwambe .....zimo kweli?!!
 
Pia wale wa kuomba mwongozo, kugonga meza na kushindwa kuibanda serikali inaposhindwa kazi.

Maendeleo ya Watu Hayana Chama !
 
Mkuu upo sawa ila si wa upinzani tu hata wa ccm. Na mtu ww kutilia mkazo kupima ni wagombea Urais. Tukiendekeza huchama tutakuta siku moja tunatawaliwa na kichaa bila kujijua.
 
Mkuu upo sawa ila si wa upinzani tu hata wa ccm. Na mtu ww kutilia mkazo kupima ni wagombea Urais. Tukiendekeza huchama tutakuta siku moja tunatawaliwa na kichaa bila kujijua.
Kweli ya america na tz yanathibitisha hilo
 
Back
Top Bottom