Inshiyetu
Member
- Jan 6, 2017
- 85
- 53
Kwa kupunguza gharama, ni vema watumishi wanaohamia Dodoma toka Dar na mikoa mingine waje kwa kutumia usafiri wa treni na magari ya mashirika ya umma, hii ni pamoja na yale ya Jeshi la Wananchi, Magereza na kadhalika. Hii itasaidia kubeba mizigo.
Tusichukulie kuwa kuhamia Dodoma ndio watu wengi watatoka Dar na kuja Dom. Dodoma pia kuna watendaji wa Serikali, hivyo nadhani watakao kuja ni wale watendaji wakuu kitaifa na sio ki mikoa mfano toka Kinondoni,Temeke ....???.
Ingependeza kama Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), kupima na kutoa mikopo ya viwanja kwa watumishi wa Serikali wanaohamia Dodoma. Hii itawahamasisha kuhamia, pia itawatoa katika midomo ya madalali na gharama ya ununuzi toka mikononi mwa watu.
Pendelezo kwa malipo yafanywe kwa muda ya miaka miwili, ili kuwapa fursa ya kujenga na kuhamia kwa muda mfupi.
Tujikumbushe kuwa kuhamia Dodoma, kunatupa fursa ya kujenga Taifa kiurahisi, yaani hadi vijijini kutafikika kuhurahisi. Dodoma ni katikati na kuna nafasi nzuri tu. Hali ya hewa ni nzuri sana, hakuna vumbi sana kama mnavyofikiria.
Twendeni Dodoma.