Ule mdahalo, kama chombo cha habari kimojawapo kilivyorippti leo kuwa cheche zilizotemwa na akina Warioba, Profesa Kabudi, Mzee Butiku na kijana Polepole, ilikuwa funga kazi.
Ndiyo maana, wabunge wa bunge la katiba, akiwemo Samuel Sitta na Dr Kigwangwala, tokea leo asubuhi, badala ya kujikita kuijadili Rasimu, badala yake wameendeleza mipasho na kejeli, kwa Jaji Warioba na Tume yake.
Ni dhahiri kwa sasa, kila anayeangalia bunge la katiba, anagundua kuwa wabunge hao wameishiwa hoja za kuwashawishi wananchi, sababu za kutosha ni kwa nini wanayakataa maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Tume ya Warioba na badala yake wanataka kuchomeka, sura zao mpya, zilizoandaliwa pale Lumumba.
In this situation, getting a new constitution in our country, at present circumstances, we can dare to call it as a next to impossible mission!