Ombi maalumu kwa dr. Slaa na timu yake

mapambanodaima

Senior Member
Oct 22, 2012
108
170
Nimepata taarifa ambazo sina uhakika nazo kuwa Dr. Slaa na timu yake watakuwa na mkutano katika kijiji cha Kyengege katika tarafa ya Kinampanda wilaya ya Iramba. kama ndivyo naomba sana ziara hii isipite bila kupitia eneo la Kinampanda ambapo kuna wafuasi wengi wanahitaji kupata matumaini mapya kwa chama chao pendwa CDM. hili ni ombi langu kwakuwa nami ni mwanachama hai na pia kwa eneo la Kyengege kuna distance kidogo ambayo itawafanya wanaopenda kumsikiliza Dr. washindwe kuhudhuria. Pia niuombe uongozi wa Wilaya wa Chadema Iramba wajitahidi kupanga ziara eneo la kinampanda ambalo lina wasomi wengi na ambao wanaweza kuwa kitovu cha mabadiliko.Niwatakie maandalizi mema tutakuwa pamoja katika kuimarisha chama.
 
ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,961
1,225
Mnataka kuhalalishiwa gongo? Mbona watu wa iramba tunawaheshimu inakuwaje tena? Zindukeni sasa
 
ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,961
1,225
Ndugu zangu wanairamba,

kama dr slaa atafika ktk ardhi yenu muulizeni km alikuwa seriuos aliposema haya maneno na km bado ana msimamo huo.

Dk. Slaa: Tukishika dola tutaruhusu utengenezaji pombe ya gongo

Saturday, 14 December 2013 · Posted in OMG, Siasa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,439
2,000
Naona walimu wa Kinampnada mna hamu ya mageuzi, ni vizuri akienda kuwasalimia maana wakitoka hapo hao ni walimu nchi nzima na watakachoenda kufanya ni kukitangaza chama nchi nzima.
 
LILENDI

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
1,400
0
Ndugu zangu wanairamba,

kama dr slaa atafika ktk ardhi yenu muulizeni km alikuwa seriuos aliposema haya maneno na km bado ana msimamo huo.

Dk. Slaa: Tukishika dola tutaruhusu utengenezaji pombe ya gongo

Saturday, 14 December 2013 · Posted in OMG, Siasa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.

CHANZO: NIPASHE

lazima utakuwa unatumia nanihii kufikiri. kila uzi unaweka gongo tu halafu you don't bother reading between the line.

usumbue ubongo wako kwenye bold na red.
 
jogofefu

Member
Mar 14, 2013
95
0
Ndugu zangu wanairamba,

kama dr slaa atafika ktk ardhi yenu muulizeni km alikuwa seriuos
aliposema haya maneno na km bado ana msimamo huo.

Dk. Slaa: Tukishika dola tutaruhusu utengenezaji pombe ya gongo

Saturday, 14 December 2013 · Posted in OMG, Siasa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya
kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda
Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya
gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na
wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa
kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa
wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika
mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya
kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato
serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti
na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote
wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha
linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo
wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda
cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi
huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya
kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala,
wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia
wananchi," alisema.

CHANZO: NIPASHE

mipasho tu hiyo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom