Ombi maalum kwa polisi: Kesho tunaomba kuwasindikiza viongozi wetu makao makuu ya jeshi la polisi

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Kama mnavyojua viongozi wetu wameamriwa kesho kuripoti jeshi la polisi makao makuu baada ya kukamatwa kwa kosa la kutotii amri ya jeshi tukufu ya kuzuia mikutano ya ndani. Viongozi wetu wanaotakiwa kuripoti makao makuu ya jeshi letu pendwa ni. Freeman Mbowe, Edward Lowassa, Dr Mashinji na Mnyika.

Katika kutii sheria bila shuruti ni kwamba viongozi wetu watatii wito huo wa jeshi letu pendwa. Na kama ilivyo utamaduni wetu waafrika mtu akikwambia niko polisi, mahakamani au hospitali lazima ama umsindikize au uende kumuona. Sisi vijana wa matawi yote ya Dar es Salam tumejipanga kuwasindikiza viongozi wetu makao makuu ya jeshi la polisi.

Mpaka sasa matawi yote ya Chadema Dar es Salaam kuu (Great Dar) wamethibisha kushiriki zoezi hilo la kuwasindikiza viongozi wetu. Je tunaruhusiwa? Tunategemea jibu lenu tafadhari, na kwa sababu si barua rasmi mnaweza kuitisha press conference mkatujibu.

Asanteni
 
Mie nawashauri badala ya kuwasindikiza Polisi nyie muendelee na maandamano, maana wote mkiwa polisi si ina maana maandamano Dar hayatakuwepo?
 
Mie nawashauri badala ya kuwasindikiza Polisi nyie muendelee na maandamano, maana wote mkiwa polisi si ina maana maandamano Dar hayatakuwepo?
Mambo ya UKUTA tuachie sisi, hili ni tofauti na UKUTA
 
Back
Top Bottom