Ombi Maalum kwa Mh Tundu Lissu

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,198
Mheshimiwa Tundu Lissu umetetea kwa nguvu kubwa bungeni kuhusu jengo la Mahakama kuu ya nchi. Hata hivyo inaelekea hukusikilizwa na upo uwezekano Tanzania kama Taifa huru tukajengewa jengo la mahakama kuu - chombo cha juu kabisa katika kusimamia utoaji wa haki katika nchi yetu. Ni aibu na fedheha kubwa hasa kipindi hiki tunaposheherekea miaka 50 ya uhuru kujengewa jengo la Mahakama na mmiliki wa hoteli toka nje ya nchi!

Sasa basi, kwa nafasi ya kipekee uliyonayo kama mbunge na kama mwanasheria naomba utuongeze sisi wananchi wa Tanzania ili TUCHANGE na kujenga jengo la mahakama kwa VIJISENTI vyetu WENYEWE. Uhuru wetu uko hatarini na vizazi vijavyo vitatulaani tukiruhusu kujengewa Mahakama na mwekezaji toka nje! Nina hakika watanzania pamoja na shida zetu wataiitika mwito wa kujenga jengo la mahakama sisi wenyewe. Naomba mwongozo wako.
 
Nikubaliane nawe mkuu kwa suala la kumpongeza Lisu kwa juhudi zake za kutetea kutovunjwa kwa jengo la mahakama ya rufaa.

Kwa mtazamo wangu nilidhani badala ya Lisu kutuongoza kuchangishana vijisenti ili tuweze kujijengea jengo letu wenyewe, ningedhani aanze na kufungua kesi mahakama kuu kupinga kuvunjwa kwa jengo hilo.

Tukizungumzia kuchangisha watanzania wenyewe ili kujenga jengo letu iwe ni last resolution baada ya hii ya kwanza kushindikana, na tuwe tumejipanga vizuri kwa namna ya ukusanyaji wa pesa hiyo na udhibiti wake, manake hawa watu wenye nasaba na magamba wanaweza kuishia kula michango yetu na jengo tusilione. Tunayo mifano halisi ya wananchi kuchangia ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali lakini pesa zikaliwa na mchwa wa magamba.
 
Höngera Lisu.
Naona kabla ya Lisu kuchangisha, kwanza ifunguliwe kesia kupnga kuvunja jengo la mahakama.
 
Höngera Lisu.
Naona kabla ya Lisu kuchangisha, kwanza ifunguliwe kesia kupnga kuvunja jengo la mahakama.

Ndugu yangu, kesi ifunguliwe katika mahakama ipi?, si watashinikiza maamuzi ya mahakama, mahakama ya tanzania sio chombo huru tena.
Wala tusitegemee haki.
 
Tanzania hata lini tutaacha kujizalilisha kwa fedheha yetu wenyewe? Mh Lissu bigup!
 
Hii option ya kwenda mahakamani inaweza isibadilishe hiki kinachotaka kutokea. Mahakama zetu haziko huku kama ilivyo kwenye katiba yetu. Kuna mrokorogo hasi na lazima tutakwama. Kumbuka Symbion wamenunua mitambo ya Dowans huku agizo la makahaka la likikataza kufanya hivyo na hadi leo hakuna yeyote anayesema wametoa wapi nguvu ya kuuziana.

Mimi nadhani kwa mara ya kwanza watanzania tusimamie uhuru wa nchi yetu ili kila kiongozi mwenye dhamana na atakayepata dhamana ya kuongoza ajuwe wazi kuwa kuna mambo hayakubaliki kama hili la kujengewa mahakama.

All we nee is a reference point or a leader, na nadhani Lissu angefaa sana kwenye hili.
 
Kama kuchanga pesa tayari watanzania tushachangia kupitie kodi tunazolipa kila mahali na kuliwa na akina Jairo type
 
jamani humu tupo wasomi acheni kuongea upuuzi hv ww mwananchi uji hurumii utachangia vitu vingapi katika nchi? Na hii serikali ya ****** ni kwanini iuze jengo la nguzo muhimu ya dola kama mahakama kisa hyo parking ya klm hotel? Ok na hzo kodi zetu zinafanya nn hazina? Kama mwelevu hakikisha unajitambua na andika vitu ambavyo umevifanyia utafiti na sio kukurupuka wadau humu kuna wanazuoni wakutosha!
 
Waende mahakama ipi,hizi za kuendesha kesi usiku kinyume na taratibu?mmesahau mgomo wa walimu kesi iliendeshwa mda gani na maamuzi kutolewa saa ngapi?
 
Jambo la kwanza kesi ifunguliwe haraka iwezekanavyo kupinga ujenzi wa jengo la mahakama na mlowezi, then watanzania kwa nia njema kabisa tujitolee kwa moyo kutoa michango yetu wenyewe. Naamini tunaweza tukiamua. Kama tunaweza kuchangia kwenye harusi kwanini tushindwe kwenye jambo la maana.
 
Serikali inaongozwa na binadamu na binadamu huwa anakosea. Tatizo tulilonalo kwa sasa ni kwamba hawa binadamu walio serikalii wanashindwa kutambua udhaifu wa maamuzi wanayofanya kuhusu hii mahakama ya rufaa. Nirudie tena, option ya kwenda mahakamani ina matumaini hafifu sana kugeuza umauzi ambao umeshafikiwa. Lakini kuna haja kabisa ya kuwa MASKINI JEURI ili wana wa nchi wajue mwaka 2011 watanzania walikataa uwekezaji wa fedheha.

Mh Selina Kombani kasema kuwa jengo lile ni dogo, na limekaa kaa kihoteli, sasa tujenge kubwa wenyewe. Kama ambavyo wananchi waliungana kudai katiba mpya wakiongozwa na CHADEMA hili nalo linawezekana kabisa.
 
Jambo la kufungua kesi ni muhimu hata kama kutashinikizwa maamuzi rekodi zitaonesha jitihada zilizofanyika kujaribu kuzuia.
 
Back
Top Bottom