Ombi la nafasi ya kazi ya Ualimu katika shule au taasisi yoyote

Mwl Samwel Mfaume

New Member
Feb 19, 2021
3
45
Naitwa Mwl. Samwel Raymond Mfaume, Nilihitimu katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa na kutunukiwa Shahada ya kwanza ya ualimu ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2019 kwa masomo ya Jografia na Kiswahili.

Kwasasa naishi Dar es Salaam, natafuta shule iliyopo mkoa wowote yenye uhitaji wa mwalimu wa masomo ya:

1. Jografia na Kiswahili (Sekondari A-Level),
2. Historia, Uraia, Jografia na Kiswahili (Sekondari O-level),
3. Historia, Jografia, Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, Sayansi ya Viumbe (Baiolojia), Uraia na TEHAMA.

Mimi pia ni mjuzi wa Kompyuta hasa katika programu za: Microsoft (Ms) Word, Ms Publisher, Ms Excel, Ms PowerPoint, SPSS, NVIVO, QGIS, MySQL Programming, Ms Windows, Ms Webs, n.k. Program hizi ninauzoefu nazo kimatumizi na ninauwezo wa kuzifundisha kwa ngazi kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vya kati.

Pia nina uwezo wa madaraja A,B,D katika kuendesha vyombo vya moto yaani magari na pikipiki. Leseni ipo na sijawahi kupatikana na hatia yoyote barabarani hasa inayohusiana na makosa ya dreva.

Pia nimewahi kufanya kazi nje na taaluma yangu hususani viwandani na katika makampuni na katika vikundi vya vijana hasa vinavyoangazia maendeleo ya jamii (Mimi ni miongoni mwa waasisi wa Kikundi cha Mpimbwe Elite's kilichopo halimashauri ya Wilaya ya Mpimbwe-mkoani Katavi).

Katika makampuni: Mathalani katika Kampuni ya Salum Mchele iliyopo Tabora nilifanya kazi kama Meneja msaidizi katika kiwanda chake cha Tofari kilichopo Tabora mjini ambapo pia nilikuwa dreva wa gari katika kampuni hiyo.

Nilishafanya pia kazi katika kiwanda cha Benjamin Mkapa kilichopo Dar es Salaam.

Kwa yeyote anaefahamu taasisi inayohitaji mfanyakazi mwenye vigezo vinavyoendana na mimi kwa namna flani naombeni msaada wa kuniunganisha na mwajiri nipatiwe kazi.

Naweza kuishi mkoa wowote wenye utulivu na amani kwa binadamu hivyo sichagui mahala pa kufanyia kazi.

Kama ipo kazi halali popote unapopafahamu nijulishe kwa sms au kama unaweza kunipigia kwa namba yangu ya simu ya +255620873116
 

Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
1,738
2,000
1. Jografia na Kiswahili (Sekondari A-Level),
2. Historia, Uraia, Jografia na Kiswahili (Sekondari O-level),
3. Historia, Jografia, Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, Sayansi ya Viumbe (Baiolojia), Uraia na TEHAMA.
Ume Specilize Masomo 9 mwalimu.

imezekanaje
 

Mwl Samwel Mfaume

New Member
Feb 19, 2021
3
45
Ume Specilize Masomo 9 mwalimu.

imezekanaje
Masomo niliyoyataja ndiyo niliyofaulu vema kuanzia ngazi ya sekondari hadi elimu ya chuo kikuu. Kwa mfano masomo niliyosema naweza kufundisha A-level ni yale tu niliyosoma chuoni. Niliyosema naweza kufundisha O-level ni yale tu niliyosoma elimu ya kidato cha nne na cha tano lakini masomo mengine niliyosema naweza kufundisha elimu msingi ni yale tu niliyofaulu Mitihani ya kidato cha nne.
Somo la kompyuta lenyewe nililisoma kama kozi nikiwa chuo flani hapa Tanzania japo natumia zaidi uzoefu wangu kwenye masuala ya kompyuta.
Ninahakika utakuwa umenielewa angalau kidogo kwasasa kiongozi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom