Ombi la Mafunzo

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,392
3,017
Mh Rais Samia Suluhu Hassan, nakusalimu kwa jina la Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Kwanza pole sana na majukumu mazito ya ujenzi wa taifa letu!

Mh Rais! Baada yakuingia madarakani,umemteua Bwana Gerson Msigwa kua Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo,kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu! Ni jambo jema na lenye afya kwa kupokezana vijiti!

Mh Rais,Huyu aliyekuja kuchukua nafasi ya Gerson Msigwa, Bwana Jafari Haniu,naona kama ana makosa mengi sana,kuna wakati font ya barua zinapishana,kuna wakati hata barua yenyewe haisomeki vizuri!

Mh Rais,tunaomba, Bwana Gerson Msigwa,ampige msasa wakutosha bwana Jafari Haniu,ili aweze kukidhi kiu ya watanzania kupata habari mjarabu kama alivyokua bwana Gerson Msigwa! Niombi langu na wala usimtumbue!
 
Back
Top Bottom