Ombi kwako: Mchango wa kumalizia hosiptali Mwanza

clion dismas

Senior Member
Aug 6, 2017
185
170
Habari ndugu

Amani ya bwana Mungu iwe pamoja nawe.

Ninakuja mbele yako wewe unayesoma uzi huu nikikualika katika mchango wa kukamilisha ujenzi wa hosiptali ambayo inasimamiwa na kanisa la waadventista wasabato Mwanza Tanzania.

Ndugu yangu, ujenzi wa hosiptali hii ulianza mwaka 2009 na hadi sasa umefikia katika hatua ya ukamilishaji ambapo kwa sehemu kubwa imejengwa kwa michango ya watanzania wenzetu, kwa aliyekuwa na 200, 1000 na yoyote ile imepelekea jengo limefikia hapa lilipo hadi sasa.

Hosiptali hii kubwa na ya kisasa inajengwa pasiansi jijini mwanza.

Kama mdau wa maendeleo unaombwa mchango wako kwa hali na mali kukamilisha kituo hiki cha afya.

ikumbukwe ya kwamba mbali na watu kuhudumiwa kimwili ambayo ni kazi ya Mungu ya uponyaji lakini pia watu huudumiwa kiroho kwa maadili yanayompendeza Mungu.

Nunakusihi kwa upole kabisa, wekeza katika kazi hii ya Mungu nawe MUNGU atajaza baraka tele katika kile kidogo ulichokitoa. Wekeza hazina yako mbinguni, ongoa roho na siku moja tukiwa mbinguni atakwambia vyema, mtumwa mwema, mchango wako ulioutoa katika hosiptali ile ndio ulifanya watu wale waokolewe wafike mbinguni.

"...NI HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA..."(MATENDO 20:35)

Sina lugha nzuri ya kukushawishi kutoa kwa kazi hii njema ya bwana mungu lakini kadri roho mtakatifu atakavyokuongoza wewe fanya vivo hivyo.

Ubarikiwe na Mungu unapojiandaa kuchangia.

nyamanoro.jpg


Barikiwa na ushuhuda huu.

Miaka kadhaa iliyopita, tabibu akiwa ofisini kwake, mgonjwa alipa hodi na kuingia ndani.

Daktari alimwambia karibu, akamuuliza yule binti aliyemuona kwa umbile akiwa mdogo kabisa, nikusaidie nini?

Yule mgonjwa(binti mdogo) alimjibu daktari, nimeleta wanangu wanaumwa. Daktari hakumuelewa, akamuuliza, wewe ndio umeleta wanako? Wako wapi? Umewaacha nje? Nenda ukawalete basi.

Binti yule akamjibu daktari, wanangu mimi, niko nao hapa, hawako nje, ninao hapa, tena ni wawili, wanaumwa.

Daktari bado hakumuelewa, binti aliyemkadiria ana miaka 14 atakuaje na watoto wawili? Na anasema amesimama nao muda ule pale ndani lakini haoni mtoto hata mmoja.
Wakati daktari akifikiria cha kumwambia yule binti ambaye hajamuelewa anamaanisha nini akaona mbele ya tumbo lake kama vile mguu wa mtoto mdogo ukitikisika, kidogo akaelewa.

Akamkaribisha, akamwambia weka watoto wako kitandani hapa niwaone na unielezee wanaumwa nini.

Yule binti akafungua kanga yake aliyokuwa amejizungushia mwilini mwake, daktari akiangalia kwa makini, binti akatoa watoto 2, mapacha, waliokua dhoofu sana, wembaba sana na jinsi walivyokua wakifanana ni kama vile mbwa asiye na manyoya na aliyelala kwenye majivu.

Daktari akizidi kusimulia, alishangaa na kuogopa, hajawahi kukutana na kitu kile tangu ameanza kazi yake ya utabibu.

Ilibidi amchukue maelezo ya kutosha yule binti. Maelezo yao yalikuwa kama ifuatavyo:-

Daktari: watoto hawa ni wako? Mbona wewe bado ni mdogo.sana?

Binti: Ndiyo, watoto hawa ni.wangu,

Daktari: mama yako na baba yako wako wapi?

Binti: walikufa mda mrefu sana.

Daktari:Unasoma? Na je, unaishi na nani?

Binti: sisomi, nilikua na.ishi na dada wa dada wa bibi yangu mzaa baba. Nikiwa darasa la 5, muda huo, nilikua nakaa na bibi yangu baada ya wazazi kufariki nikiwa mdogo. Bibi yangu hakuweza kutimiza mahitaji ya kila siku, nilikua naenda shule na njaa na pia nilikua sina hata daftari wala kalamu. Nafika darasani nasinzia, wenzangu.wananicheka na maisha.ya.namna hiyo.

Siku moja mwanafunzi wenzangu wa kiume hapo shuleni aliniambia, nikubalie na unipende nitakua nachukua hela nyumbani nakuletea na unanunua mahitaji ya.shule. binti anasema hakuewa na mbadala na wala hakukataa.

Alilala na mwanafunzi huyo, akampa mimba na mwanafunzi yule wa kiume baadaye alitoroka.

Basi ndipo nilipo achia shule muda huo.

Daktari: Pole sana, sasa nikusaidieje?

Binti: muda wote nikiwa na bibi kijijini alishindwa kunihudumia baada ya kujifungua hawa mapacha, akaniambia, nenda mjini, najua hata nauli.sina ta kukupa, ila nenda pale kutoa cha magari, muelezee konda hali yako yote uliyonayo, mwoneshe na watoto hao atakusaidia ufike mwanza. Sitaki hao.watoto wafie hapa. Mwanza kaulizie pale kuna ndugu zako.watakusaidia.

Daktari: sasa hao ndugu zako wamekusaidiaje hadi sasa? Mbona hali ya watoto hawa ni mbaya?

Binti: konda yule nilipo mueleza na kumuomba msaada alinikubalia akanileta bure hadi mwanza. Ndugu niliwatafuta nikawapata lakini kwakweli, maisha ya pale ni mlo mmoja kutwa na mara nyingi ni wa kugombania.

Daktari: pole sana,

Binti: ahsante, na hadi nimekuja hapa ni jirani wa pale niishipo amesema niende kwa wasabato watanisaidia. Nimeulizia hosiptali na ndio maana niko hapa.

Basi daktari akamchukua binti na mapacha wake.wale wawili, akaenda na akawapima uzito kila mmoja. Wa kwanza alikua na gramu 700, wa pili gramu 900. Hali yao ilikua ni mbaya, uzito chini ya kilo moja.kwa kila mmoja.

Basi binti alihidumiwa kwa kadri ya roho alivyomuongoza na gharama zote alizigharamia Mungu wa mbinguni. Ndani ya miezi 6 watoto waliongeza uzito wa kilo 3 kila mmoja.

WITO

NDUGU YANGU, WAHITAJI NI WENGI, WOTE WANAKUTEGEMEA MIMI NA WEWE.

KWA JINSI MUNGU ATAKAVYO KUONGOZA, TUNAOMBA USAIDIE MCHANGO WAKO ILI KITUO HIKI KIKAMILIKE NA WATU.WENGI KAMA BINTI HUYU.WAHUDUMIWE .

(MUNGU KWANZA, MAMBO MENGINE BAADAYE).
 
Back
Top Bottom