Ombi: Airtel warudishe kifurushi cha 400MB

Imany John

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
2,937
Reaction score
1,193
"Habari njema kutoka Airtel. Nunua kifurushi cha 500MB kwa sh 3500 tu kitakachotumika kwa siku 10. Tuma neno INTERNET kwenda 15444 na furahia kuperuzi"

Ujumbe tajwa hapo juu,tunaomba hata kama mtafanya elfu 4000 ila muda uwe ni mwezi mmoja. Vigezo vya siku kumi sijajua mmetumia vigezo vipi.

Nawasilisha.
 
Kisirudi na hakina maana, mtandao gani Wa kipuuzi wanatoa huduma kwa kubagua? Mara utasikia laini za zamani zinapata hiyo bando na line mpya hazipati! Stupid sana Airtel.
 
nunua kifurushi kilichopo kulingana na mahitaji yako na mfuko wako..
Source: 100 huduma kwa MAteja
 
Hata hicho kidogo watakipoteza ,ngoja mwezi uishe wafanye tathmini
 
hamia zantel. 1500 tsh. kwa mwezi mzimaaaa. zantel ndio mpango mzima kwa sasa ktk internet.
 
Mimi nimwkwisha hama Airtel. Nilijiunga na Airtel mwaka 2007, nikiwa safarini Sumbawanga, baada ya hapo nikawa natumia Airtel kwa ajili ya intaneti tu.
Sasa wamepandisha bei, ili kufidia gharama za simu, na mimi nimehama mazima.
Ila wakishusha bei nitarudi.
 
hamia zantel. 1500 tsh. kwa mwezi mzimaaaa. zantel ndio mpango mzima kwa sasa ktk internet.

Je nitajiunga vipi? Je vipi kuhusu ubora wa huduma, hususani sis wa simu? Ikiwezekana nakwenda kununua kadi sasa hivi! Huwa natumia voda (100MB kwa mwezi kwa 2,000/-)
 
"Habari njema kutoka Airtel. Nunua kifurushi cha 500MB kwa sh 3500 tu kitakachotumika kwa siku 10. Tuma neno INTERNET kwenda 15444 na furahia kuperuzi"

Ujumbe tajwa hapo juu,tunaomba hata kama mtafanya elfu 4000 ila muda uwe ni mwezi mmoja. Vigezo vya siku kumi sijajua mmetumia vigezo vipi.
Nawasilisha.
Imany John,ikumbukwa kuwa kampuni za simu zinatakiwa kutoa huduma zinazoshabihiana na maisha halisi ya watanzania. Internet ndo huduma inayotegemewa na watanzania wengi katika mawasiliano,nashauri kampuni za simu kufanya huduma ya internet kuwa ni free,
 
Last edited by a moderator:

neno lako la mwisho "free" limeniacha hoi.. Watakula wapi sasa??kama kutuma msj whtsapp, MB 1 inachukua karibia wiki moja kuisha.. Nani wa kupiga simu.. Kodi ya serikali itatoka wapi??
 
Last edited by a moderator:
"Habari njema kutoka Airtel. Nunua kifurushi cha 500MB kwa sh 3500 tu kitakachotumika kwa siku 10. Tuma neno INTERNET kwenda 15444 na furahia kuperuzi"

Ujumbe tajwa hapo juu,tunaomba hata kama mtafanya elfu 4000 ila muda uwe ni mwezi mmoja. Vigezo vya siku kumi sijajua mmetumia vigezo vipi.

Nawasilisha.
nahisi pia wangesema na 500mb tu
 
neno lako la mwisho "free" limeniacha hoi.. Watakula wapi sasa??kama kutuma msj whtsapp, MB 1 inachukua karibia wiki moja kuisha.. Nani wa kupiga simu.. Kodi ya serikali itatoka wapi??
Sajy, kumbuka wakati kampuni hizi zinakuja Tanzania in 90's huduma za SMS ilikuwa ni free na wakati huo wateja wao walikuwa wachache,sidhani kama sasa watashindwa kufanya hivyo kwa kuwa huduma nyingine gharama bado ipo juu,
 
Last edited by a moderator:
Mi tangu waondoe mb 400 kwa mwezi,nlihama,na nlipowauliza wenzangu wakacheka sana ati waligundua na tayari walishatunza airtel moderm kwenye masanduku...mimi na buytime ,wakirudisha tuambiane .
 
Duu wewe bado uko enzi za zamani hivyo??? Hamia Zantel ule rahaaa, achana na karahaaaaa!!! :wink: :wink:
 
Back
Top Bottom