Ndugu zangu Watanzania wenzangu, katika vitu vinavyo niumiza akili yangu ni hili la Omba omba wa wanawake kutumia watoto wao wachanga kupata huruma kwa wapita njia barabarani.
Hii hali imekuwa ikindelea kuongezeka kila siku hapa jijini na Serikali yetu imelinyamazia kimya hili swala, Mtoto mchanga kabebwa mgongoni na mama yake anatembezwa barabarani mchana kutwa jua lake mvua yake, haki ya huyu motto ni nini hasa? Ustawi wa jamiii kazi yake nini katika Nchi yetu hii. Hawa watoto nani atawasaidia ili waweze kupata haki zao za msingi kama watoto?
Watunga sheria kwanini wasitunge sheria inayowahusu hawa watoto wanaotumiwa kama mradi na wazazi wao, Ukisimama barabarani anakuja mama na mototo wake mgongoni anaomba msaada, hana kilema cha aina yeyote, ukimuuliza baba wa mototo yupo wapi utasikia amekufa, au alinipa mimba akanitelekeza kumbe uongo mtupu baba zao wapo na wanaishi pamoja. Kuna Yule mama mwingine kule ocean road anayeshinda na kulala pale ufukweni alianza na mototo mmoja na sasa wamefika wane(4) hivi hii ni bahati mbaya kweli, kuna kituo cha redio kimoja waliwahi kumchangishia hela ya mtaji ili arudi kwao Kigoma akafanye biashara ndogondogo imfae na wanae hakwenda kokote mpk leo yupo, aliwahi kushauriwa awapeleke watoto ustawi wa jamii wapate kulelewa na wasome amegoma akijua wale ndio mtaji wake wa kujiingizia pesa.
Hii ni haki kweli, wale watoto wakikuwa watafanya nini au na wao ndio wawe ombaomba au ndio vibaka wajao?
Mimi nadhani Sheria ingechukua mkondo wake kwa kuwafikiria hawa watoto na future yao wakikuwa.
Njia rahisi ni kila mama anayeingia barabarani na mototo mgongoni kuombaomba Serikali/Ustawi wa jamiii wampokonye mototo na akalelewe kwenye vituo maalulu vya kulelea watoto.
Hii itasaidia kama mtu anataka kuwa omba omba aache motto nyumbani atangetange peke yake
.. hii haingii akilini mtu mungu kakuumba na viungo vyako kamili kwa nini ukae barabarani na motto kuomba. Kwa nini usitafute biashara ndogo ndogo ufanye uweze kulea motto.
Huu ni uzembe na serikali yetu kwa ujumla inachangia hili kwa kuwafumbia macho hawa wazazi.
Sijui wenzangu mnalionaje hili swala kwa upande wenu.
Nawakilisha.
Huu uzi umetoka mda kidogo but tokana na sababu zilizokua nje ya uwezo wangu sikua jamvini
Namshukuru alotoa Uzi huu kwani ni moja ya maeneo ambayo hunigusa saana (watoto hasa katika vulnerable positions..).. Namshukuru pia na mwana JF mwenzangu aloni PM uzi huu kwa kutambua kabisa kua nitakua interested na kutaka tubadilishane mawazo
Domo kaya huwezi amini nilikua naanda kitu kinafanana na this thread ili nipost nione Watanzania kupitia JF members wanalichulia vipi hili suala but hamna kilichoharibika ila tu nimesikitika saana kwamba ukweli wa Jamii Forums kama jamvi la Great Thinkers ni kwamba tunakoelekea tutachakachuliwa/kujichakachua na kupoteza kabisa maana halisi ya GT
watoto ambao ndo future generation hawawi considered kabisa katika jamii yetu tokana na ukweli kua sie Watanzania ni wachongaji saana mdomo kwa mambo ambayo hatufaidi directly na hatuna kabisa uzalendo
Tungekua wazalendo ni mambo mengi ambayo tungezingatia na kutafakari hasa katika suala zima la Watoto.. Mfano mdogo hapo Zambia, Lusaka au Ndola wana mabango kubwa (whether you like it or not unaliona) ambalo serkali limeweka kuhamasisha kua hamna kuwapa watoto wa mtaanai msaada wowote
Vivyo hivyo na Malawi pia
WAZAZI/WALEZI WANAOWATUMA WATOTO
Hawa kwa kweli ilitakiwa wawe wanachukuliwa hatua kabisa for hawafai wala kuwaonea huruma watoto hao ambao mara saa ingine hata wakuwazaa wenyewe
hata hivyo naomba nisiwaongelee saana hawa niwaongelee watoto wenyewe ambao wanahusika moja kwa moja na tabia ya kuomba omba aidha kwa kutumwa ama mwenyewe kuamua kufanya hivyo..
Na kabla sijaenda mbali... naomba ujue Domo Kaya kua akina mama tunafanya kazi kubwa saana kulea familia zetu hivyo naomba mtambue hilo na pia muappreciate nguvu zetu hizo
naamini unajua kua idadi kubwa ya single parents Tanzania kubwa ni akina mama tena hawana hata support na kuwalea wanae kwa kile kidogo/kikubwa apatacho; as a result of ujane or sababu nyingine nyiiingi!
Katika huo mfano ulotoa wa huyo mama wa watoto wanne, Yule ni special case na anapenda position aliyopo kwani kajaribu kusaidiwa na kushawishiwa atoke pale ikiwemo na serkali yenyewe but hurudi pale pale na anapenda saana wanaume (in her own words
) nilibahatika kusikiliza siku moja interview radion akiwa anahojiwa na Dina Marios
it was so disappointing and cannot go into that right now
.
JINSI GANI JAMII INACHANGIA HILI TATIZO..
Watoto wa mtaani kwa sasa wanaongezeka kwa kasi ya ajabu.. na inaniuma saana kua hao watoto na wakike wamekua wengi katika hilo kundi.. jamani mtu yoyote aki comprehend hiki kitu kwa umakini ataona the way ilivyo serious; hapa inatakiwa kuobserve si tu madhara ya papo hapo ambayo pia ni meeengi but kama haitoshi there future is really really bleak
Watanzania ama niseme wanajamii kwa ujumla ni moja ya sababu kubwa saana kwa kuongezeka idadi ya hao watoto wa jinsi hio mtaani.. Hi ni sababu watu wanatoa msaada kadri awezavyo wakiamini as much as they can help at least wasadie na the little they have
hii ndio mbaya kabisa! Bahati nzuri sifanyi kwa assumptions, maana katika masomo ya elimu ya juu nilibahatika kufanya project inayohusisha watoto wa mtaani
katika kutaka kupata majibu ni kwa nini watoto ni wengi hapa Jijini (Dar) na hali panaongoza kwa vituo vingi vya kulelea watoto hizi ni baadhi ya majibu
- Pamoja na kusema watoaji wanatoa pesa ndogo ndogo kama Ths 100/=, Ths 200/=, Tsh 500/= wengine hata zaidi ya hapo; mwisho wa siku hao watoto hufikisha pesa nzuri kama alfu 2/3/4 mpaka hata alfu saba and in rare cases hata zaidi
(na hio information kwa hao watoto unapata kwa kuwahonga
you buy them food talk to them patiently and promise them money to tell the truth
huku ukichukulia aweza kukudanganya but once umewasiliana na wengi unaunganisha moja na moja unapata jibu..)
- Wazaza/walezi wa watoto hao huwatuma hao watoto kufanya shuguli ya kuomba.. hao watoto wakikusanywa kula baada ya muda na vituo vya watoto yatima au wa mtaani
baada ya siku mbili tatu wanarudi tokana na ukweli yuko huru zaidi kufanya atakalo
baada ya time kujiingiza katika mitihani mbali mbali ambayo imetawala katika miji yetu ya sasa katika ulimwengu ulochafuka!
- To mention but a few reasons
SERKALI
Kama kawaida Serkali yetu on paper inamalengo mazuri na Watanzania in most cases.. the problem lies with implementation of those rules, guidelines or policies whatever they call them
Serkali yoote na wizara zake kwa mtazamo wangu naona wame concertrate katika siasa and all the propaganda happening mpaka wanasahau utendaji na bahati mbaya saana hawana hawa watoto hawana watetezi
Hata hivyo napenda ni acknowledge Non Governmental Organisations ambazo naona kama zaongezeka kwa kaasi kuhusiana na welfare za watoto kama Save the Children, Tanzania children Trust Fund, SOS Childrens Village (kama sikosei
), Railway Children Africa, Save the Children, Feed your Children.. to mention but a few
Wimbi kubwa la children related Organisations ni evident kua serkali yetu ililega saana na kushindwa control hio issue mpaka imetoka out of hand na sasa kama kawaida forces from outside imekuja kututatulia hii issue
.